Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,208
- 4,405
1)mbona unakunja uso,kabla ya mimi kunena.
Ukishanyimwa mnuso,wa kwanza toa laana.
Pole huo ni mguso,kile kimezindukana.
Kikiliwa cha legea,kitumikapo cha nuka.
2)kione kwanza kilivyo,pata pata tapu tapu.
Kwa nje kilivyo sivyo,tope tope chuzi supu.
Kwanza hilo ni hovyo,futafuta paka pupu.
Kikiliwa cha legea,kitumikapo cha nuka.
3)kipya kimya cha tulia,cha zamani shume pepe.
Hirizi cha zingulia,popo kopo mua jipe.
Kione cha chungulia,nani jinga akilipe
Kikiliwa cha legea,kitumikapo chanuka.
4)watajakifanya mua,ganda nalo waliteme.
Wabisha umeamua,kukikuza kwa umeme.
Suli kulisisimua,kitune panya kidume.
Kikiliwa cha legea,kitumikapo cha nuka.
5)moshi mavumba utele,hayafuti kuanguka.
Kwenye tambarare ile,kuteleza washituka.
Ukona piga kelele,mbuzi umeshaibika.
Kikiliwa cha legea,kitumikapo cha nuka.
6)kumbe wavua samaki,kwenye dimbwi la dunia.
Tumia ndo yako haki,mwenyewe wajitakia.
Pole hiyo ni riziki,ulishajitengezea.
Kikiliwa chalegea,kitumikapo cha nuka.
Shairi=KIKILIWA.
mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.