Zumarid anaonewa, wakamatwe na kina Mwamposa

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
24,504
28,693
ZUMARID anaonewa na kosa lake kubwa ni kutojihusisha na kusifia au kuwa karibu na serikali, hilo ni kosa kubwa ambalo kalifanya kwa makusudi au kujisahau .

Zumarid havunji sheria ya nchi, anawa-brainwash wajinga na kupiga mamilioni na maisha yamemnyookea vizuri tu.

Zumarid hana tofauti kubwa na kina Mwamposa, Mwingira, Gwajima, Frank, Mama Rwakatare, GeorDavie, Malisa, na wanaojiita manabii na mitume hapa TZ. Mzee wa Upako (huyu ni wa muda mrefu na siku hizi analalamika wanaokuja wanajiita mitume na manabii hivo wanamuharibia biashara).

Narudia hana tofauti nao kubwa, wote Objective yao ni kupiga hela, Mwamposa anauza keki, maji, mafuta, leso n.k kwa mwamvuli zina upako, na anapiga hela, ila ni mjanja yupo karibu na utawala.

Waulize hata kina Kakobe, Gwajima, Mzee wa Upako wamefikaje hapo bila bugudha; walijiweka karibu na utawala, hivo wakaaminika na kutumia janja zao na mazingaombwe (miujiza fake), kwasasa wana ukwasi mkubwa sana. The same kwa kina Mama Rwakatare, Mzee wa Upako hadi barabara alijengewa, Gwajima kabla ya misa zake atamuombea JPM na makatibu wote wa wizara, na amekuwa akiisifu sana serikali siku hizi.

Hii kwa Zumarid alisahahu, ndio maana Serikali imemfikia, ila hana tofauti yoyote na kina Mwamposa au Gwajima , wanatofautiana tu taratibu za kupiga hela, ila mazingaombwe (miujiza fake) ni ile ile.

Zumarid yupo hapo Isenyi kwa karibu miaka 3, havunji sheria ya nchi, anachokifanya ni kile kile wanachofanya kina Mwamposa, kuwa-brainwash watu na kupata fedha nyingi bila kuilipia kodi.

Naomba double standard isitumike kwa Zumarid Diana Bundala), wakamatwe na hawa wanaowauzia watu maji, mafuta, keki na leso, na kudanganya wanatibu HIV kama anavyojinadi Nabii Frank .

Simtetei Zumarid, ila kama mmeshindwa kuwakamata hawa manabii na mitume waliojazana hapa Dar, Iringa, Mbeya, singida, Arusha, n.k

Basi muacheni Zumarid ale maisha, maana ameshafanikiwa kuwa-brainwash kama Mwamposa alivyofanikiwa.

Asionewe peke yake Zumarid; Gwajima, mwamposa mnawaachaje?


Soon Zumarid ataachiwa na ataendelea na shughuli zake, hakuna sheria aliyovunja.
 
Unajichanganyua ujue, mara akina Mwamposa wakamatwe mara Zumaridi hajavunja sheria.....kwahio akina Mwamposa ndio wamevunja??

Soma uelewe, kama Zumarid kakamatwa, Mwamposa anaachwaje?
Zumarid kakamatwa kwa kosa gani?
Maana hakuna tofauti kubwa kati ya Zumarid na kina Mwamposa , Mwingira, na hawa wanaojiita manabii.
 
Soma uelewe , kama Zumarid kakamatwa , Mwamposa anaachwaje?

Zumarid kakamatwa kwa kosa gani?

Maana hakuna tofauti kubwa kati ya zumarid na kina mwamposa , Mwingira ,na hawa wanaojiita manabii
Amekamatwa na kufungiwa kwa kosa la kuendesha huduma bila ya usajili. Ayekuwa anatumia mwavuli wake amemtema kwa kuona anaenda kinyume na imani iliyompa kivuli. Hilo ndilo kosa kubwa. Cha kufanya afuaye utaratibu wa kusajili huduma yake tu.
 
Amekamatwa na kufungiwa kwa kosa la kuendesha huduma bila ya usajiri. Ayekuwa anatumia mwavuli wake amemtema kwa kuona anaenda kinyume na imani iliyompa kivuli. Hilo ndilo kosa kubwa. Cha kufanya afuaye utaratibu wa kusajiri huduma yake tu.
Alikuwa anafanya huduma gani?
 
Amekamatwa na kufungiwa kwa kosa la kuendesha huduma bila ya usajiri. Ayekuwa anatumia mwavuli wake amemtema kwa kuona anaenda kinyume na imani iliyompa kivuli. Hilo ndilo kosa kubwa. Cha kufanya afuaye utaratibu wa kusajiri huduma yake tu.
Miaka yote minne walikuwa wapi , Leo ndio wameshtuka hana kibari?
 
Akiachiwa na akaisifia “awamu ya tano” bila shaka tutajua ni nini kilimuweka ndani....
Nakuhakikishia soon atarudi na kuendelea na shughuli zake za kitapeli

Alichokosea kutojiweka karibu na serikali

Kuna rafiki yangu nimesoma naye , juzi amekuwa nabii anajiandaa kuanza kula hela za wajinga , nimemshauri ajiweke kwanza karibu na Serikali
 
Bado mtume CONTROLA nakuja,nawalia tu taimingi

lazima maandiko yatimie yani...

Chidi benzi alihojiwa kuhusu skendo za nandy akasema amemwambia nandy

"nandy unazihitaji hizi sana,ikibidi kama unaweza vua hata chupi ukienda chooni piga picha post,yani unazihitaji sana hizi nandy"

swali : anazihitaji nini??
Jibu : Kiki naization

so zumaridi kwa pesa aliyonayo hii tunaifananisha na tukio la mlela na ebitoke namimi nasema hiviii

Zumaridi unai hitaji sana hii mama yani ukitoka tu huko ulipo media zote zipo kwako + waumini YES umetimiza ulilopanga,na hata mimi niliekua sikufahamu nimekufahamu sasaa.

unanipa wakati mgumu sasa niende kwa mwamposa au nikupandie kipepeo nije kwako? watu mna marketing tamu asee
 
Back
Top Bottom