Bendera za ACT zapepea Makao Makuu CUF Z’bar

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015
Harakati za ubadilishwaji wa bendera katika matawi mbalimbali ya Chama cha Wananchi (CUF) kisiwani Pemba zinaendelea asubuhi hii na kupandishwa za ACT- Wazalendo huku wakitaka bendera hizo haraka kisiwani humo.

Katika wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba matawi mbalimbali yanaendelea kubadilishwa bendera hizo na wananchi walio wengi wanaonekana ni wenye kufurahia hatua hiyo.

Shughuli hiyo ya ubadilishwaji wa bendera inaongozwa na Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Micheweni, Rashid Khalid Salim akiwa pamoja na waliokua viongozi wa chama chao awali.

Kwa mujibu wa Salim wanachokifanya sasa ni kubadili bendera maeneo yote na kufungua matawi mengine mapya ya ACT- Wazalendo kwenye wilaya yao.

Amesema kwa sababu jambo hili limetokea kwa kipindi kifupi na baadhi ya walio wengi hawakuwa wamejipanga kufanya hivyo ndio maana maeneo mengine kuna ukosefu wa vifaa zikiwemo bendera na rangi.

Kutokana na hali hiyo Salim aliwataka viongozi wakuu wa chama hicho kuhakikisha wanawapatia bendera za ACT-Wazalendo haraka.

Kwa upande wake aliyekua mwakilishi wa CUF Jimbo la Micheweni, Thubeit Khamis Faki amesema hawana muda wa kupoteza na kujadiliana kuhusu kumuunga mkono Profesa Ibrahim Lipumba kwa sasa wanachokiangalia ni kusonga mbele.

Alipoulizwa kuhusu majengo ya ofisi za CUF wanaamuaje kufanya mabadiliko amesema majengo mengi ya ofisi za chama ni ya wananchi wenyewe waliojitolea hivyo si miongoni mwa mali za chama hicho.

Bendera za ACT zapepea Makao Makuu CUF Z’bar
 
Bendera za ACT zapepea Makao Makuu CUF Z’bar

Siku moja baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kutangaza rasmi kujiunga na Chama cha ACT- Wazalendo, iliyokuwa makao makuu ya CUF Mtendeni mjini Unguja visiwani Zanzibar imeanza kupepea bendera ya ACT- Wazalendo.

pic+makao+makuu.jpg


BY Muhammed Khamis, Mwananchi mkhamis@mwananchi.co.tz
IN SUMMARY
Iililokua jengo la makao makuu ya Chama cha Wananchi (CUF) Mtendeni mjini Unguja visiwani Zanzibar asubuhi ya leo Jumanne limeanza kupepea rasmi bendera mpya ya chama cha ACT- Wazalendo


Advertisement
Unguja. Siku moja baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kutangaza rasmi kujiunga na Chama cha ACT- Wazalendo, iliyokuwa makao makuu ya CUF Mtendeni mjini Unguja visiwani Zanzibar imeanza kupepea bendera ya ACT- Wazalendo.
Uwepo wa hali hii umeibua maswali kwa baadhi ya wananchi na kujiuliza iwapo jengo hili lilikua mali ya chama au ya mtu binafsi.
Baadhi ya wanachama wa CUF kisiwani hapa wakizungumza na Mwananchi walisema hawafahamu kuhusu jengo hilo.
Majda Awadhi amesema anachokifahamu yeye hapo ni makao makuu ya chama na walikua wakiingia na kutoka tu.
“Inawezekana ilikuwa mali ya chama au pia inawezekana walikuwa wanakodi pia, yote ni sawa tu” amesema.
Soma zaidi: Maalim Seif: Shusha tanga, pandisha tanga safari ianze
Naye Said Hassan amesema kinachoonekana sasa ni matukio mazuri zaidi kwao kuliko kubaki kwenye mgogoro aliodai hauna tija kwao.
Amesema anaamini hali hiyo viongozi wanaifahamu na watakua wamejipanga vyema kutetea iliyokuwa makao makuu ya chama hicho iwapo upande wa Profesa Ibrahim Lipumba utadai ni sehemu ya mali ya chama.
Alipoulizwa na Mwananchi aliyekua Mkurugenzi wa habari wa chama cha CUF, Salim Bimani upande wa Maalim Seif, amesema kwa sasa si suala la kujadili na muda ukifika kila kitu kitajulikana ukweli wake.
Amesema kwa sasa wananchi wafahamu kuwa iliyokua jengo la makao makuu ya CUF imegeuka rasmi kuwa ofisi ya ACT- Wazalendo Zanzibar.
Soma zaidi: CUF Pemba wataka bendera za ACT
"njaa kali" Lipumba kabaki na gunia tupu, huku Maalim akiondoka na mbuzi wake kiroho safi kabisa.

majuto!!
 
Back
Top Bottom