Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) yapiga marufuku matumizi ya "Drones" bila kibali maalum

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania imepiga marufuku taasisi au mtu binafsi kurusha angani vifaa ya kielektroniki visivyo na rubani (Drones) bila kupata kibali/idhini maalum kutoka Wizara ya Ulinzi na Usalama pamoja na Mamlaka hiyo.

Taarifa ya TCAA imefafanua kuwa uendeshaji wa shughuli zote za anga nchini uko chini ya Mamlaka hiyo kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo.

image.jpeg

19961217_1950751635161321_8173695641503678304_n.jpg

Picha inayoonesha Drone​
 
Kwa ujinga wa serikali yetu hii tusiwalaumu wasanii wakienda kushuti video zao nje ya nchi. Na wakifanya hivyo nchi itakosa vingi sana...
Don't ask me why


Brawn Shao
Bado tuko dhama za mawe za kale. Baada ya kuja na vigezo vinavyoruhusu kupiga picha na drone tunaleta makatazo.

Hawa ndio wasomi wetu

sent by me
Hawajakataza huo upigaji picha.. Ila ni lazima uwe na kibali maalumu. Kama una kampuni ya upigaji Picha iliyosajiliwa sidhani kama watakunyima kibali ukiomba kutumia drone kwenye shootings zako..
 
Kwa ujinga wa serikali yetu hii tusiwalaumu wasanii wakienda kushuti video zao nje ya nchi. Na wakifanya hivyo nchi itakosa vingi sana...
Don't ask me why


Brawn Shao
Mkuu hawajakatazwa moja kwa moja. Wameambiwa waombe kibali wizara ya ulinzi na pia mamlaka ya anga. Kasome vizuri huo waraka waliosema upo ktk tovuti yao TCAA na sheria za kurusha hizo drone kwa mujibu wa taratibu za anga za ICAO na TCAA. Sio kudandia hoja kisha kulaumu bila kufuatilia kwa undani. Waende tu wakatengeneze huko nje kuliko kuzembea mambo ya usalama.
 
Kwa ujinga wa serikali yetu hii tusiwalaumu wasanii wakienda kushuti video zao nje ya nchi. Na wakifanya hivyo nchi itakosa vingi sana...
Don't ask me why


Brawn Shao
Mkuu brawn shao sidhani kama kila kitu ni cha kuwa na kuilaumu serikali.Mambo mengine tunapaswa kutenga muda na kujadiliana kwa staha ili kuipa serikali mawazo mbadala badala ya kutukana na kuikashifu tu.Sisi ndio serikali,yaani mimi na wewe....Toa mawazo ya "Way Foward"

Kwanza kwangu,hili katazo la hizi RPA (Remotely Piloted Aircraft) limechelewa sana.Na hawa mamlaka ya usafiri wa Anga ni kama wamechelewa kutoa katazo la aina hii.

Nchi zingine kuwa na hii RPA ni lazima uwe na leseni au kibali toka Idara za Ulinzi na Mamlaka za Anga,sababu hiki chombo ni "Aircraft".

Kuna sababbu za Safety and Security za kuhakikisha vifaa hivi vinathibitiwa.Hii ni dunia ya "Cyber Attacks",watu wanatumia drones kuzituma nchi za watu kusaka habari za kishushu,drones nyingine zinakuwa "weaponized".

Siku hizi mpo kwenye mkutano wa kisiasa,unaona drones inapita juu,hamajajiridhisha ina nini,mtu anaweza aka-weaponized mkutano mzima mkafa

Mikutano ya Rais pia,mtu anaweza kutumia drones kumlipua Rais au hasimu wake wa kisiasa.

Kumbuka Rada haiwezi kuona kitu chenye 1pixel Echo.Lakini watu wanarusha tu hovyo angani,unaweza kukuta drones inakuwa sucked na injini ya ndege yanye abiria 300 wakati inatua au kuruka.Huu ni msiba mkubwa kwa dunia.Drones ikiwa sucked kwenye injini ya ndege kama ni Emirates au Swiss,ni aina ya Cyber Terrorism,na TCAA lazima watawajibika kwa kutukutunza anga lao kwa ndege zinazotumia

.Kuna baadhi ya maeneo marubani wameripoti kuona drones nyingi juu ambazo ni hatari kwa usalama wa anga,sasa TCAA kama regulator wa usalama wa anga,hili ni jukumu lake.Tusipinge tu kila kitu bila kuwa na facts

Wenzetu waliliona hili zamani...Wasomi wao wakaliandikia na kutoa mapendekezo.Soma hapa http://www.birmingham.ac.uk/Documen...te-warfare/executive-summary-october-2014.pdf
Cc FisadiKuu
 
nadhani lengo hapa ni kutambua uwepo wa hizo drone, pia kuwajulisha limitation za matumizi ya hizo drone, maeneo yanayokatazwa zisioperate kwa ajili ya usalama n.k. Hizi ni assumption zangu.

Ninavyofahamu ukiwa maeneo ya airport mfano unaweza sababisha ajali za ndege, maeneo ya jeshi, balozi na makazi ya viongozi kwa kutokujua ama kwa kujua unapopiga picha hizo tayari unaharibu protocal za ulinzi na usalama
 
Haka kadude Jana tu kamesumbua sana Mitaa ilipo wizara ya ulinzi. Naungana sana na Serikali kwa hili maana hata wahalifu wanaweza kutumia drones kukusanya taarifa au kushambilia sehemu yeyote na vikiwa angani ni ngumu kujua kipi ni cha adui na kipi ni salama. Naipongeza sana Serikali kwa hili. Japo nadhan wangeenda mbali kwa kutaka wanaomiliki wamiliki kwa vibali maalum.

Sent from my Lenovo A1000 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom