Tabia zilizojificha: Chanzo cha migogoro kwenye mahusiano

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,867
d987097e8c8575a51ef34a66fc0ba71e.jpg

Binadamu ana hulka ya kutosema ukweli hulka ya kutosema mabaya/madhaifu yake. Wengi wetu huvutiwa na lugha za watu hasa mnapoonana kwa mara ya kwanza.

Mapenzi kabla ya ndoa si kipimo halisi cha tabia utakazokutana nazo ndani ya ndoa hasa mihemko na Masham sham vinapoisha. Uwe makini na kuwa tayari kukabiliana na ukweli mchungu kuwa yule kabla ya ndoa hawezi kwa asilimia mia kuwa huyu baada ya ndoa.

Hizi tabia hazionekani mapema bali hujifunua taratibu kadiri muda na kuzoeana kunapoongezeka..na hii yaweza kuchukua hata miaka.

Watu wengi sana wameshindiwa hapa kwamba yule mtu uliyempenda na kumwamini sana kumbe ni;
Mlevi mbwa
Malaya kupindukia
Mnafiki sana
Muongo
Bahili
Ana roho mbaya
Mbinafsi
Mchonganishi
Kigeugeu n.k.

Ndani ya mahusiano ya muda mrefu ndio tabia kama hizi hujifunua, ni ngumu kwa baadhi ya hizi tabia mtu kusema ukweli wake ni ngumu sana.

Moyo wa mtu ni kiza kinene sana, wengi wetu humu tuko kwenye mahusiano ya kindoa au kimapenzi tu, wengine wameshatendwa na wanaugulia maumivu
Jiepushe na maumivu jiepushe na kuvunjika kwa mahusiano kwasababu kuna gharama zake kubwa tu... imagine una invest muda raslimali na hisia zako kwa mtu kwa zaidi ya miaka mitano halafu unaishia divorce...!!! Gharama na hasara si haba.

Tambua kwamba kuna tabia za kuchukiza na pengine zisizovumilika.. jiandae kuzikabili na kuzikubali.. .. hakuna mkamilifu kila mwanadamu ana roho ya kishetani ikiwemo WEWE

Asikudanganye mtu kuwa hizo tabia zinarekebishika, huko ni kujidanganya na kujitafutia maumivu zaidi.

78d839dc3add7eb5673093f810dba387.jpg
 
Mambo huwa magumu zaidi kama tayari mna watoto na unagundua tabia isiyovumilika hapo una chaguzi mbili tuu aidha kuishi na maumivu kwa ajili ya watoto au kuamua kujitoa kwenye mahusiano
Kama mahusiano hayajafika mbali sana ni bora kukubali maumivu ya maramoja kuliko maumivu ya wakati wote it's never too late you can start all over again though with bitter experience
 
Ukitaka kujua tabia za mtu unaeanzisha nae mahusiano moja ya kitu unachotakiwa kuepuka ni kumwambia akwambie vitu anavyopendelea na asivyopendelea..Hapa mara nyingi drama ndipo zinapoanza.. Vile vitu utakavyosema huvipendi ntajaribu kuvificha hata kama ninavyo ili mradi nikupate..Hayo maigizo kumaintain ni kazi..Itafika kipindi mtu anashindwa kuficha tabia yake..Kipindi zinafumuka unajikuta tayari upo ndani ya ndoa na huyo muigizaji na hakuna mlango wa kutokea.

Mara nyingi ni vizuri kumsoma mtu ujue ni mtu wa aina gani bila yeye kukwambia kisha ujipime kama unaweza kuwa nae au vipi
 
Mara nyingi hua nawaambia wale wanaochelewa au kukawia kuingia kwenye ndoa kwa kisingizio cha kuwasoma wachumba/wapenzi wao wanapoteza muda bure. Ni kweli kuna baadhi ya tabia watazigundua lakini kuna zingine hata muwe kwenye mahusiano karne nzima, huwezi kuzigundua hadi uishi na huyo mhusika.

Hivyo ukishaona kuna baadhi ya vitu mnaendana na mwenzio na mnapendana, ni kufanya maamuzi huku ukitegemea na kujiandaa kukabiliana na mambo mageni kutoka kwa mke/Mme ambayo haukuwahi kabisa kuyafaham.
 
Ukitaka kujua tabia za mtu unaeanzisha nae mahusiano moja ya kitu unachotakiwa kuepuka ni kumwambia akwambie vitu anavyopendelea na asivyopendelea..Hapa mara nyingi drama ndipo zinapoanza.. Vile vitu utakavyosema huvipendi ntajaribu kuvificha hata kama ninavyo ili mradi nikupate..Hayo maigizo kumaintain ni kazi..Itafika kipindi mtu anashindwa kuficha tabia yake..Kipindi zinafumuka unajikuta tayari upo ndani ya ndoa na huyo muigizaji na hakuna mlango wa kutokea.

Mara nyingi ni vizuri kumsoma mtu ujue ni mtu wa aina gani bila yeye kukwambia kisha ujipime kama unaweza kuwa nae au vipi
Kweli kabisa.
Na vile vile namna pia ya kuepukana na hizi drama ni vema kabla ya kuanza kudate lazima muwe karibu au muwe na mazoea
Yaani kila mmoja awe anamfahamu vema mwenzake katika hali ya kawaida....

Mnapokuwa normal friend ni rahisi zaidi kumfahamu mtu kwa vile anakuwa hajifich au hafich Tabia zake.

Ukianza kwa kumuoneshea nia yako. Lazima atajibadili meinendo Yake ili aonekane Si tatizo....

Couple za best friend au watu waliowahi kuishi kama marafiik Wa kawaida kwa muda mrefu nadhani changamoto kama hii kidogo inapungua. Kwa vile mnakuwa mnafamiana A to Z....
 
Nakuunga mkono kwa 100%. Unakuwa na mahusiano na msichana na unamuona muelewa. Unaona ana nia ya dhati ya kujemga familia..mnalianzisha na unaona anakuwa msaada kwako mwanzoni. Baadae unaanza kuona element ya ubinafsi anataka chako kiwe chenu lakini yeye chake anaficha. Unaanza kushangaa ma kujiuliza ni kwanini. Hana mke mwenza na huna mchepuko.Unajiuliza hiyo yote ya nini! Mna watoto unawasomesha shule nzuri na nyumbani unatoa matumizi. Yeye kila analofanya ni kwa kificho. Ikifika hapo unaanza kuwaza labda mwenzangu ana mpango uliojificha. Unabaki huelewi...Ukweli nakubali tabia zinajificha na mara nyingi huwa tunadanganyika hapo mwanzoni.
 
Kweli kabisa.
Na vile vile namna pia ya kuepukana na hizi drama ni vema kabla ya kuanza kudate lazima muwe karibu au muwe na mazoea
Yaani kila mmoja awe anamfahamu vema mwenzake katika hali ya kawaida....

Mnapokuwa normal friend ni rahisi zaidi kumfahamu mtu kwa vile anakuwa hajifich au hafich Tabia zake.

Ukianza kwa kumuoneshea nia yako. Lazima atajibadili meinendo Yake ili aonekane Si tatizo....

Couple za best friend au watu waliowahi kuishi kama marafiik Wa kawaida kwa muda mrefu nadhani changamoto kama hii kidogo inapungua. Kwa vile mnakuwa mnafamiana A to Z....
Busara za bazazi..Umeongea nukta mkuu
 
Mara nyingi hua nawaambia wale wanaochelewa au kukawia kuingia kwenye ndoa kwa kisingizio cha kuwasoma wachumba/wapenzi wao wanapoteza muda bure. Ni kweli kuna baadhi ya tabia watazigundua lakini kuna zingine hata muwe kwenye mahusiano karne nzima, huwezi kuzigundua hadi uishi na huyo mhusika.

Hivyo ukishaona kuna baadhi ya vitu mnaendana na mwenzio na mnapendana. In kufanya maamuzi huku ukitegemea na kujiandaa kukabiliana na mambo mageni kutoka kwa make/Mme ambayo haukuwahi kabisa kuyafaham.
True story; mwaka 2011 binti mmoja aliolewa na jamaa mmoja 'handsome sana' kijana mtulivu asiye na mambo ya michepuko kabisa
Huyu jamaa alikuwa na jamaa yake mmoja walikuwa hawaachani they were more than best friends, kwahiyo hata ilipotokea kutokuelewana ndani ya nyumba jamaa ndio aliitwa kama msuluhishi
Siku moja mwaka 2013 binti akawa anaenda kwenye kikao mahali nyumba akimwachia mumewe na shemeji naye alikuwepo
Akiwa keshapanda bus akapigiwa simu kwamba kikao kimeahirishwa hivyo hakuwa na namna zaidi ya kushuka na kutafuta usafiri wa kurudi nyumbani, kufika hm akaingia moja kwa moja sebuleni mlango ulikuwa umeegeshwa tu lakini hakuona mtu hivyo akaongoza chumbani...
Ni huko chumbani alimkuta mumewe wa ndoa anapumuliwa kisogoni na yule best friend wake...binti alizindukia hospitali na kwa miaka miwili mfululizo hakuwa sawa kabisa
Ndoa ile ilivunjika lakini huyo jamaa kaoa tena na mkewe wa sasa inasemekana anaijua fika tabia ya mumewe lakini kaikubali
Huyo jamaa ni mc maarufu sana na FB hakauki
 
Na ndio maana pastor mmoja alitufundisha kuwa, ukiingia kwenye mahusiano, ni vizuri mkaelezana madhaifu yenu yote. Na niliuzingatia sana ushauri huo. Nimekuwa simwelezi mpenzi wangu kwa maneno, bali kwa tabia, na hapo nilianza tukiwa mwezi wa tatu wa mahusiano.
 
Mmh ila kuna tabia nyingine hazielezeki kabisa mfano
Umbea
Udokozi
Uchimvi
Rohombaya nknk
Hizi hujifunua taratibu mno na kuna wakati kupitia kwa wengine. ..mfano unakuta wasichana wa kazi hawakai au ugomvi na majirani hauishi
 
Na ndio maana pastor mmoja alitufundisha kuwa, ukiingia kwenye mahusiano, ni vizuri mkaelezana madhaifu yenu yote. Na niliuzingatia sana ushauri huo. Nimekuwa simwelezi mpenzi wangu kwa maneno, bali kwa tabia, na hapo nilianza tukiwa mwezi wa tatu wa mahusiano.
Kweli kabisaa hapa utakuwa umetatua kidogo tatizo. Na ni vema umueleze kabla hamjaingia kwenye dating.ili apime kama anaweza kuvumilia
Kuna udhaifu unaelezeka mkuu....nadhani ni ule unaovumilika....
What if unaudhaifu Wa kuwa mwongo, mzinzi, plus mbinafs plus kiburi
 
Ukitaka kujua tabia za mtu unaeanzisha nae mahusiano moja ya kitu unachotakiwa kuepuka ni kumwambia akwambie vitu anavyopendelea na asivyopendelea..Hapa mara nyingi drama ndipo zinapoanza.. Vile vitu utakavyosema huvipendi ntajaribu kuvificha hata kama ninavyo ili mradi nikupate..Hayo maigizo kumaintain ni kazi..Itafika kipindi mtu anashindwa kuficha tabia yake..Kipindi zinafumuka unajikuta tayari upo ndani ya ndoa na huyo muigizaji na hakuna mlango wa kutokea.

Mara nyingi ni vizuri kumsoma mtu ujue ni mtu wa aina gani bila yeye kukwambia kisha ujipime kama unaweza kuwa nae au vipi
Kaboom
Nakubaliana na wewe 85% lakini mimi tabia yangu lazima nataka kujua nini anapendelea na nini hapendi. sawa na mimi humuelezea pia ninacho penda na nisicho kipenda. Kuna demu wangu nilimuacha kwasababu nishamwambia sipendi kitu hichi na yeye ndio alichokifanya.
 
Back
Top Bottom