radika
JF-Expert Member
- Jul 15, 2014
- 20,427
- 32,196
Inasemekana bwana mkubwa hakufarahishwa na kitendo cha balozi wetu kwenda kumuona ndugu lissu na kumuona ni msaliti akaenda mbali zaidi na kusema hali kama hiyo aliipitia ndugu Lazaro Nyalundu alipokwenda kumuona lissu kwani wabunge wa ccm walizuiwa kwenda na ndicho chanzo kikuu cha Nyalandu kuamua kuachia ubunge wake na kujitoa ndani ya chama cha mapinduzi ( ccm) kwa kuwa hakuridhishwa na namna ya hilo jambo lilivyokuwa likiendeshwa na mwenyekiti wao.
Kahitimisha kwa kusema kwamba wanachama wao kwa sasa wanahali ngumu mno katika vipindi vyote ambayo wapo ndani ya chama hicho kikongwe.
My take:
Kwa upande wangu naona hili jambo si zuri hasa kwa sisi Watanzania tulishazoea kuishi kwa upendo kwani siasa sio uadui lakini inashangaza bwana mkubwa anapogeuza siasa ni uadui hasa kwa yale majibu yake ya kuomba aachwe afanye atakavyo aje kuulizwa mbele hii kitu inatia shaka mno,
Inakuwaje mtu anasema siasa nazifungia kwa kuwa natukanwa huku nikiwajengea barabara je hizo pesa ni za hisani toka mfukoni kwake? Nakumbuka wanafunzi wa udom waliitwa vilaza sijui kama anakumbuka hizi kauli za kuudhi.
Ukipenda kusifiwa kubali kunakukosolewa hata shilingi ina pande mbili.