Ameniambia tupo kwenye mahusiano lakini hana 'feelings' na mimi

marigy

JF-Expert Member
Aug 13, 2017
341
402
Kwanza nishukuru jukwaa la MMU kwa kunijenga, kunifundisha na kunielimisha kuhusu mahusiano kwani nimekuwa msomaji wa mda mrefu wa jukwaa hili hivyo michango mingi inayotolewa hapa kuitumia kuishi na mpenzi wangu.

Ni story ndefu kidogo lakini itakuwa kifupi;

Nilikutana na huyu mpenzi nikiwa kidato cha tano hivyo nikanzisha harakati za kummiliki, baada ya kumwambia ya moyoni alisema ye kuna jamaa kamtongoza tayari hivyo mimi nimechelewa, sikukata tamaa nikaendelea kufwatilia lakini nikabaini kweli anadate na jamaa ilinibidi nikaushe,

Baada ya muda kupita kwenye likizo ya mwezi wa tisa hapo tupo kidato cha tano binti alinitafuta na kuniambia ameridhia kuwa namimi sababu na mimi nilikuwa nampenda sana huyo binti basi kwangu ilikuwa furaha sana.

Toka hapo tukawa wapenzi rasmi na kurudi shule baada ya likizo couple ikawa inafahamika sana sababu nae ni binti ambaye kaumbika vizuri halafu mweupe, basi mimi nikajua sababu yeye ndo alinambia karidhia basi mambo yatakuwa rahisi.

Ajabu ikawa ngumu sana hasa kwenye kusex lakini sababu nampenda pamoja na michango ya JamiiForums niliendelea kuwa na subra huku vizawadi vya hapa na pale vikikolea, ikapita takribani miezi nane bila hata romance dah hatari hii yeye yupo hosteli mi day.

Baada ya kumaliza kidato cha sita nikaaproch sex japo kwa mbinde sana akaja kukubali, basi hiyo siku nirifurahi sana tukaenda lodge tukafanikisha kuvuana nguo naku sex.

Baada ya hapo nikawa nahitaji sana sex lakini alinambia mimi mpaka miezi miwili ipite ndo tutasex tena nikasema sawa, nami kama kawaida vigift viliendelea ili asijisikie vibaya kwamba nmebadilika bada ya kunipa penzi.

Pamoja na hayo binti akawa amepunguza ile kunimiss sana ikawa kawaida hali ambayo mi ilikuwa inanikera na huku mda wa kungonoka tena ukikaribia ilibidi nianze kumwandaa kisaokolojia mapema, basi kwenye kuchati nikakumuliza mbona siku hizi unavijtabia fulani hivi, akanambia tatizo sio yeye alafu akauliza swali umewahi kuwa kwenye mahusiano na mtu ambaye huna hisia nae?

Basi akaongezea kwamba yeye akidate na boy inafika kipindi ananza kumchukia sana na mtu ambaye anamchukia kwanza ni boy wake wa kwanza anasema wanavyosema boy wa kwanza huwezi msahau lakini mi kwangu huyo ndo mtu ambaye namchukia sana alindelea kwamba baba yake na mama yake hawaishi pamoja pia kitu ambacho kinamfanya asiwe na imani na boy yeyote sababu hata baba yake hamwamini.

NB:
Ni binti ambaye shule alikuwa anaonekana kawatosa sana hata walimu na mimi nilisumbuka sana kwa binti huyu mpaka kumpta na kusex baada ya kunambia hivyo mi nimefuta namba zake, picha pamoja na conversation zote za whatsApp lakini bado nampenda huyu mpenzi wangu sababu tuliadiana vitu vingi sana na jana kabla ya kunambia hivi aliweka status WhatsApp ilikuwa encourage distance love sababu wiki ya tatu leo sipo karibu nae.

Nifanyeje jamani? Naamini nitapata chochote licha ya mamuzi niliyoyachukua, maswali yatajibiwa na ufafanuzi ukihitajika utatolewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah umenishtua kama tulikupa ushauri wa kwenda kufanya ngono kutoka humu JF...form five!!!!

Anyway, hakuna mahusiano yanayoanza na ngono yanayodumu. Kama akili yako unaishi kuwaza ngono hutapata hata mawazo ya kumfahamu mtu.

Pili, usiwe na mahusiano na mtu ambaye bado hajasamehe yaliyomtokea nyuma. Huyu binti, kwa bahati mbaya sana yuko kidato cha tano na tayari washamtoa bikra, ila anajutia kitendo alichokifanya. Mpaka siku atakapoweza kujisamehe kosa alilofanya hatokaa aweze kumpenda mtu. Wote mtakaopitia mikononi mwake mtakuwa wahanga wake. Usithubutu kujaribu maana alichokuambia ndicho kweli anachojihisi na nimekutana na binti wengi sana wa hali hii. Wengine watu wazima lakini bado wana machungu na chuki juu ya wanaume wao wa kwanza (na wengine hata wa pili/tatu/nne...yeyote yule ambaye eyye alimpenda na kumuamini lakini akamvunja moyo).

Inahitajika neema ya Mungu kutoka kwenye laana hiyo.

Ushauri wangu kwako uache zinaa uache kuwa mahusiano mdogo wangu. Natamani ungenisikiliza mara hii moja tu. Biblia inasema, "Kila aziniye na mwanamke hana akili kabisa tena aiangamiza nafsi yake (mitahi 6:32)" Huo mstari haukuwekwa kwa bahati mbaya. Ukianza kuzini, 90% ya akili yako itakuwa inawaza hayo.

Umri wako sasa ni wa kuhusiana na wasichana kwa ajili ya kujenga networks za shule, kujenga social skills nk sio kujenga mahusiano ya ngono. Hayo yatakuja ukioa (sitaki hata kukushauri kuwa uanze mahusiano ya ngono ukiwa chuo..maana nitakuwa mnafiki).

Kwa ufupi tu kama hutaona umuhimu wa ushauri wangu basi jibu fupi kwa kisa chako: achana na binti yeyote ambaye ameumizwa na hajasamehe na kujisamehe. Mbeleni utakapoanza mahusiano tena jitahidi sana kufahamu hili.

Soma threads hizi mbili (zote ni thread hiyo hiyo moja):

- 40 Things a Man Must Know About Life, Love and Women

- 40 things a man must know about life, love and women

Zingatia sana #8.

Kweli nakuombea neema ya Mungu uweze kuepuka ngono. Wewe mwenyewe unahitaji kusamehe na kujisamehe maana bitterness haipo kwa wadada tu. Uache zinaa. Utie bidii katika elimu. Zoeana na hao mabinti hata kama mke wako atakuwa katika hao unaosoma nao lakini utafurahia sana baadaye kwa urafiki mzuri mliokuwa nao kuliko ngono mlizozifanya.
 
TUMIA HZO JUHUDI KULIMA MATIKITI NA KUIELEWA 'FOREX' AHAHAHA

ANYWAY, HUYO DEMU KWA KUWA AMEKUELEZA HANA HSIA NA WEWE, MPGE CHNI ENDELEA NA MAMBO YAKO, NA UKWELI NI KUWA ANAYE MWANAUME ANAMPENDA SANA NA YUKO MBALI NA YEYE ILA SYO WEWE. KWA HYO STATUS HAIKUHUSU
 
Back
Top Bottom