JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

On JF:

Mzee Mwinyi alijiuzulu Uwaziri Mambo ya Ndani mwaka 1977 na Nafasi yake kuchukuliwa na Mzee Natepe. Natepe alipoingia tu ofisini alimtaka Waziri Mzee Mwinyi kutoka katika nyumba ya Waziri arudi kwao Zanzibar ili yeye aweze kuishi hapo kama Waziri. Ilikuwa shida kidogo maana Mzee Mwinyi bado alikuwa anatafuta makazi lakini alitakiwa haraka kutoka. Nasikia Mzee Mwinyi ilibidi atoke hivyo hivyo bila kujiandaa lakini siku anatoka pale nyumbani alizuiwa na Mzee Natepe kuchukua mabati na mifuko ya simenti aliyokuwa amenunua kwa pesa zake mwenyewe kwa ajili ya ujenzi wa nyumba binafsi. Natepe alimkatalia kuvichukua akidai ni mali ya Serikali. Kweli Mzee Mwinyi akaviacha akaondoka. Baada ya miaka kadhaa tu Mzee Mwinyi akateuliwa kuwa Rais wa...
Nimeona taarifa mtandaoni ikisema watumishi wa Umma na Binafsi ambao wamechangia kwa zaidi ya miezi 108 yaani miaka 9 katika NSSF au PSSSF sasa rukhsa kutumia michango yao kama dhamana ya kuchukulia mkopo wa kujenga, kuboresha au kununua nyumba nchini Tanzania. Kanuni namba 141 za Mwaka 2024 zimeanza kazi tangu Machi 8, 2024. JamiiCheck tusaidieni kujua ukweli wake.
Wakuu, Nimekutana na taarifa imepostiwa na Times FM ikiwa na maneno yanayodaiwa kutamkwa na Kiongozi Mkuu wa Korea Kaskazini Kim kuwa anashangaa jinsi wazungu walivyofaulu kuwaaminisha Waafrika kwamba mitala ni dhambi lakini LGBTQ+ ni haki ya binadamu. Waafrika wanapaswa kujifunza jinsi ya kufuata dini zao. Hadi siku Waafrika wakifuata utamaduni wao wenyewe, dini za kigeni wakizikumbatia hawataweza kamwe kujiendeleza. Naomba kufahamu ukweli wa taarifa hii, maana nimependa sana haya maneno nataka niitumie sehemu.
Katika mitandao ya kijamii nimeona video inayohusishwa na Rais Mpya wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, akikemea Ufaransa kuwa ni wakati wa kuondoka bara la Afrika. Video hiyo inamuonesha Rais Faye akiimbia Ufaransa kuwa "Inakuwa wakati wa Ufaransa kuinua magoti yake kutoka shingoni mwetu na kumaliza ukandamizaji huu usio wa haki. Karne nyingi za mateso, biashara ya binadamu, ukoloni, na ukoloni mamboleo vimesababisha mateso yasiyohesabika. Ni wakati wa kumaliza mzunguko huu wa ukandamizaji," Wachangiaji wengi kwenye video hizo zinazozunguka mitandaoni walionesha furaha kwamba Rais Faye ameonesha msimamo imara dhidi ya Ufaransa kulikandamiza bara la Afrika. Video hiyo inanipa mashaka.
Nani asiyemjua mbabe Simba mfalme wa nyika? Yaani ukutane naye paaah! Utamzame machoni aone aibu na kuondoka? Bado siamini hili jambo naona hawa vijana wa ovyo wanataka kuniingiza chaka siku nikikutana naye mbashara nisichukue njia nyingine za kujiokoa eti nimtizame. Hivi kweli Simba huyu kweli wa kumwonea aibu binadamu kisa kumuangalia machoni ana kwa ana kwa ujasiri. Wakuu naombeni taarifa sahihi kuhusu hili jambo, huenda mada ikawa kichekesho lakini hili jambo linasemwa sana mtaani.
Matumizi ya tumbaku ni moja ya maafa ya afya ya umma yanayojulikana sana. Licha ya ripoti nyingi kuhusu afya ya umma, matumizi ya tumbaku yanazidi kuongezeka katika nchi zinazoendelea na zilizoendelea. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), takriban watu Bilioni 1.3 duniani wanavuta sigara ambapo 80% kati yake wanatoka kwenye nchi zenye uchumi mdogo na uchumi wa kati. Aidha, takriban watu Milioni 7 hupoteza maisha kutokana na athari za moshi wa sigara unaotokana na kuvuta sigara moja kwa moja au pia kuvuta moshi uliotolewa na mvutaji wa Sigara. Tumbaku huathiri karibu kila kiungo na mfumo katika mwili, ikisababisha matatizo mbalimbali kama vile saratani, Magonjwa ya mfumo wa upumuaji, Ugonjwa wa Mishipa ya Moyo, Kiharusi...
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…