JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Zipo imani na madai ya mbalimbali ya kijamii yanayobainisha namna ambavyo mama anaweza kumdhoofisha (kumbemenda) mtoto wake baadhi ya madai hayo ni: 1. Baba na Mama hawapaswi kujamiiana wakati kipindi cha unyonyeshaji kwa sababu kufanya hivyo hupelekea mtoto wao kudhoofika (kumbemendwa). 2. Lazima mama aoge ajioshe na sabuni kwanza baada ya kujamiiana ndipo amnyonyeshe mtoto wake ili asimbemende. 3. Mama akipata ujauzito wakati bado ananyonyesha anaweza kumbemenda mtoto wake. 4. Mzazi akijamiiana nje ya ndoa akishiriki tena tendo na mwanamke wake anayenyonyesha anambemenda mtoto.
Nimeona taarifa mtandaoni ikisema watumishi wa Umma na Binafsi ambao wamechangia kwa zaidi ya miezi 108 yaani miaka 9 katika NSSF au PSSSF sasa rukhsa kutumia michango yao kama dhamana ya kuchukulia mkopo wa kujenga, kuboresha au kununua nyumba nchini Tanzania. Kanuni namba 141 za Mwaka 2024 zimeanza kazi tangu Machi 8, 2024. JamiiCheck tusaidieni kujua ukweli wake.
Wakuu, Nimekutana na taarifa imepostiwa na Times FM ikiwa na maneno yanayodaiwa kutamkwa na Kiongozi Mkuu wa Korea Kaskazini Kim kuwa anashangaa jinsi wazungu walivyofaulu kuwaaminisha Waafrika kwamba mitala ni dhambi lakini LGBTQ+ ni haki ya binadamu. Waafrika wanapaswa kujifunza jinsi ya kufuata dini zao. Hadi siku Waafrika wakifuata utamaduni wao wenyewe, dini za kigeni wakizikumbatia hawataweza kamwe kujiendeleza. Naomba kufahamu ukweli wa taarifa hii, maana nimependa sana haya maneno nataka niitumie sehemu.
Katika mitandao ya kijamii nimeona video inayohusishwa na Rais Mpya wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, akikemea Ufaransa kuwa ni wakati wa kuondoka bara la Afrika. Video hiyo inamuonesha Rais Faye akiimbia Ufaransa kuwa "Inakuwa wakati wa Ufaransa kuinua magoti yake kutoka shingoni mwetu na kumaliza ukandamizaji huu usio wa haki. Karne nyingi za mateso, biashara ya binadamu, ukoloni, na ukoloni mamboleo vimesababisha mateso yasiyohesabika. Ni wakati wa kumaliza mzunguko huu wa ukandamizaji," Wachangiaji wengi kwenye video hizo zinazozunguka mitandaoni walionesha furaha kwamba Rais Faye ameonesha msimamo imara dhidi ya Ufaransa kulikandamiza bara la Afrika. Video hiyo inanipa mashaka.
Nani asiyemjua mbabe Simba mfalme wa nyika? Yaani ukutane naye paaah! Utamzame machoni aone aibu na kuondoka? Bado siamini hili jambo naona hawa vijana wa ovyo wanataka kuniingiza chaka siku nikikutana naye mbashara nisichukue njia nyingine za kujiokoa eti nimtizame. Hivi kweli Simba huyu kweli wa kumwonea aibu binadamu kisa kumuangalia machoni ana kwa ana kwa ujasiri. Wakuu naombeni taarifa sahihi kuhusu hili jambo, huenda mada ikawa kichekesho lakini hili jambo linasemwa sana mtaani.
Salaam Wakuu, Nimekutana na stori mtaani zinadai kwamba mnamo mwaka 1990 Bondia Maarufu Muhamedi Ali alienda nchini Iraq kuzungumza na rais wa nchi hiyo wakati huo Sadam Hussein kuwaachia mateka wa Marekani na kufanikiwa. Je, kuna ukweli wowote kuhusu sakata hili? Tunaombeni ufafanuzi ====== Muhammad Ali alizaliwa mnamo 17 Januari 1942 na alifariki 3 Juni 2016. Muhammad Ali alikuwa mwanamasumbwi kutoka nchini Marekani. Awali alijulikana kama Cassius Clay, lakini alibadilisha jina lake baada ya kujiunga na jumuia ya Kiislamu ya Nation of Islam mnamo mwaka wa 1964. Baadaye akabadilisha dini na kuwa Mwislamu kunako mwaka wa 1975 Ndipo alipobadili jina na kuanza kufahamika kama Muhammad Ali. Alipata kuwa bingwa wa uzito wa juu mara...
Back
Top Bottom