Featured content

CAS: Uamuzi wa Rufaa ya Senegal utatoka haraka iwezekanavyo
Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) imetangaza kuwa itatoa uamuzi wa rufaa ya Senegal "haraka iwezekanavyo" kufuatia hatua ya nchi hiyo kupinga kuvuliwa taji la Mataifa ya Afrika (AFCON), uamuzi uliofanywa na Shirikisho la Soka Afrika (CAS) mnamo Machi 18, 2026. Awali, Januari 18, 2026, Senegal ilitwaa ubingwa kwa ushindi wa goli 1-0, na baada ya maamuzi ya Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika (CAF), Morocco ilipewa ushindi wa mezani wa Magoli 3-0 kwa maelezo Senegal kukiuka Kanuni za
Je, mchakato wa kuhakiki taarifa kwenye vyombo vya habari unaendana na kasi ya kuenea kwa taarifa potoshi?
Shiriki nasi katika Mjadala huu kupitia Instagram Live ya JamiiForums, utakaoongozwa na mwandishi wa habari, Imani Luvanga, wazungumzaji ni Nuzulack Dausen wa Nukta Africa pamoja na Mpoki Thompson, Mhariri Mkuu Mwananchi Communication.
UN yapitisha azimio la kutambua utumwa wa Waafrika kama Uhalifu dhidi ya Binadamu
Hatua hiyo iliidhinishwa kwa kura 123 za kuunga mkono kuwa biashara ya utumwa wa Waafrika na mfumo wa kuwafanya kuwa mali ulikuwa miongoni mwa uhalifu mkubwa zaidi dhidi ya Ubinadamu na madhara yake ambayo yanaendelea kuathiri maisha ya watu hadi leo. Hata hivyo, nchi tatu ambazo ni Argentina, Israel na Marekani zilipinga azimio hilo, huku nchi 52 zikijizuia kupiga kura.
Usimamizi wa 'Mikopo ya Dharura kupitia simu' nchini Tanzania
Utangulizi Kuwa kwa kasi kwa huduma za kifedha za kidijitali nchini Tanzania kumeleta mapinduzi makubwa katika upatikanaji wa mikopo na huduma za malipo kwa mamilioni ya wananchi. Miongoni mwa ubunifu huu ni kuibuka kwa huduma za mkopo wa dharura kupitia simu za mkononi, zinazojulikana kwa majina tofauti ya kibiashara ikiwemo Songesha. Huduma hizi huwezesha watumiaji kukamilisha miamala hata wanapokuwa na salio pungufu kwenye pochi zao za simu, hivyo kutoa mkopo wa muda mfupi papo kwa hapo...
TANZIA | Waziri William Lukuvi afariki Dunia
Mwanasiasa mkongwe William Lukuvi amefariki Dunia, asubuhi ya Machi 25, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa mshtuko wa moyo. Taarifa ya msiba wa William Lukuvi, aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) na Mbunge wa Jimbo la Isimani, imetangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka. Lukuvi, alizaliwa Agosti 15, 1955 na amewahi kuwa Mbunge kwa vipindi saba tangu mwaka 1995.
Wakili: Bado kuna kesi za waliokamatwa kwa tuhuma za uhaini Oktoba 29
Wakili wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), William Maduhu ameeleza licha ya Rais Samia kutoa agizo kwa DPP kufuta kesi za uhaini zinazowakabili vijana kufuatia matukio ya Oktoba 29, 2025, bado kuna mashauri Mahakamani ya waliokamatwa kwa tuhuma za uhaini. Amesema hayo Machi 19, 2026 katika mahojiano na Jambo TV, akidai Dar es Salaam mpaka sasa wamebaki watu 8 katika Mahakama ya Kisutu, Arusha watuhumiwa 9, Mwanza na Dodoma wamebaki watuhumiwa 4.
Kenya hatarini kupoteza Haki ya kuandaa AFCON 2027 kwa kushindwa kulipa ada ya uandaaji
Kenya ipo hatarini kupoteza haki ya kuwa mwenyeji wa Michuano ya AFCON 2027 kutokana na kuchelewa kulipa ada ya uenyeji ya Dola Milioni 30 (takribani Tsh. Bilioni 77) kwa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF). Katibu Mkuu wa Wizara ya Michezo, Elijah Mwangi, ametahadharisha kuwa nchi hiyo inatakiwa kukamilisha malipo hayo ifikapo Machi 30, 2026. Hali hii inatia wasiwasi kwani washirika wenza katika zabuni ya "East Africa Pamoja," yaani Uganda na Tanzania, tayari wameshalipa fedha.
Senegal wapokwa ubingwa wa AFCON 2025 na CAF, apewa Morocco
Morocco imetawazwa kuwa mabingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika la 2025 baada ya uamuzi wa CAF siku ya Jumanne kueleza kuwa ushindi wa bao 1-0 wa Senegal kwenye fainali umebatilishwa. Senegal ilishinda mechi hiyo kwa bao la Pape Gueye katika muda wa nyongeza, ushindi ulipatikana katika mazingira yenye utata baada ya wachezaji wa Senegal kutoka nje ya uwanja wakigoma wakati wa dakika 90 za kawaida za mchezo.
Mafwele, wengine 42 kutoa ushahidi kesi ya askari wanaodaiwa kughushi vibali vya silaha
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Faustine Mafwele ni miongoni mwa Mashahidi 43 wanaotarajiwa kutoa ushahidi katika kesi ya askari wanaotuhumiwa kughushi vibali vya kumiliki silaha. Kesi hiyo inawakabili Watu tisa, wakiwemo maofisa sita wa Jeshi la Polisi, inasikilizwa na Hakimu Mwandamizi, Geofrey Mhini, na inatarajia kuanza kusikilizwa Aprili 2026.
Je, uwanja huu ulitumika Gabon kwenye AFCON 2017 na sasa umetelekezwa? Uhalisia upoje?
Wadau mbalimbali wametaka kujua uhalisia wa picha zinazosambaa mitandaoni zikionyesha hali ya viwanja vya michezo vilivyotumika katika mashindano ya AFCON nchini Gabon mwaka 2017 vikiwa katika hali mbaya ya uharibifu na kutelekezwa. Stade Omar Bongo ni moja kati ya viwanja vilivyopangwa kutumika katika AFCON 2017 lakini haukuweza kutumika kwa sababu hadi kufikia mashindano kuanza haukuwa umekamilika, hivyo haukukidhi vigezo.
Mkurugenzi DUWASA: Kama umechimba kisima tumia na familia yako usiwape wengine
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma, Mhandisi Aron Joseph, amesema Watu wanaochimba visima vya maji wanapaswa kuvitumia na familia zao pekee na wasitoe huduma kwa Wananchi wengine. Kauli hiyo ameitoa Machi 16, 2026, kupitia Clouds TV kwenye kipindi cha Clouds 360 akidai sababu ya hatua hiyo ni maji ya chini ya ardhi kubadilika sifa zake kila siku, na wengi kutopima ubora wake kabla ya kuyatoa kwa wengine ambapo yanaweza kuathiri mtaa mzima.
Mahakama yatupilia mbali shauri la TLS  kupinga amri ya IGP kuzuia watu kutoka nje Oktoba 29, 2025
Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar, imetupilia mbali shauri la kikatiba lililofunguliwa na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) dhidi ya Inspekta Jenerali wa Polisi kupinga amri ya kutotoka nje iliyotolewa Oktoba 29, 2025. Mahakama imebaini dosari za kisheria katika hati ya kiapo ya Rais wa TLS, Boniface Mwabukusi. TLS ilidai amri hiyo ilikiuka Katiba ya mwaka 1977 na haki za wananchi, na kuomba kuundwa kwa tume huru ya kuchunguza vurugu zilizosababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali
Sahara Media Group yafilisiwa na kufungwa rasmi kwa kushindwa kulipa madeni
Mahakama Kuu, Divisheni ya Biashara, imeamuru kufilisiwa na kufungwa rasmi kwa Sahara Media Group Limited baada ya kubainika kuwa kampuni hiyo imepata ukata wa fedha, kushindwa kujiendesha pamoja na kulipa madeni. Uamuzi huo umetolewa na Jaji Dkt. Mwajuma Kadilu kufuatia ombi la kampuni kutaka kufilisiwa baada ya ripoti ya Afisa Mkuu Steven Diallo kuonesha kampuni imepata hasara ya zaidi ya Tsh. Bilioni 3.9 mwaka 2023 na kuwa na deni la kodi la takribani Tsh. Milioni 97.7 kwa TRA.
TPA yasogeza hadi Julai 1, 2026 kuanza kwa Ada ya Uendelezaji wa Miundombinu ya Bandari
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetoa wito kwa Wadau wa bandari kukamilisha masharti na marekebisho ya mikataba waliyonayo na Wateja wao wa ndani na nje ya nchi ndani ya muda uliobaki kabla ya kuanza kutumika kwa Ada ya Uendelezaji wa Miundombinu ya Bandari (PID), Julai 1, 2026 Nyongeza hiyo inalenga kuwapa nafasi wateja na Wadau ikiwemo kampuni za usafirishaji wa meli, mawakala wa forodha na usafirishaji, wasafirishaji wa mizigo, waagizaji, wauzaji nje na ndani ya nchi.
Mdau: Fao la Kujitoa limerudishwa kisheria, kwanini NSSF hamtangazi?
Mdau amehoji kuhusu utekelezaji wa mabadiliko ya Sheria ya Mfumo wa Hifadhi ya Jamii upande wa Fao la Kukosa Ajira baada ya kurejeshwa kwa Fao la Kujitoa Desemba 2025. Anasema NSSF haijaeleza taarifa ya mabadiliko hayo kwa umma, badala yake wanaendelea kupewa mafao yao kwa mfumo wa asilimia 33, jambo linaloathiri uchumi wao na kuzua maswali kuhusu uwazi wa utekelezaji wake.
Mwigulu: Muuguzi aliyemfanyia mgonjwa upasuaji  nyumbani kwake afukuzwe kazi
Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba ameagiza mamlaka husika kumfukuza kazi Muuguzi wa Mkoa wa Tabora aliyedaiwa kumfanyia mgonjwa upasuaji wa Tumbo nyumbani, kwenye Kochi kwake badala ya hospitalini. Akizungumza Machi 4, 2026, amesema mbali na kufukuzwa kazi, muuguzi huyo pia afikishwe kwenye vyombo vya sheria kwa hatua zaidi za kisheria, pamoja na kufutiwa leseni yake ya uuguzi.
Mwigulu: Wanaokaa vikao kwamba huyu tumfanyeje, niwaambie hamnifanyi kitu
Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba, amewaambia baadhi ya Watendaji wanaodaiwa kukaa vikao kupanga njama dhidi yake, kuwa hatishwi na vitisho vya aina yoyote. Amedai maisha yake yamejengwa katika mazingira ya kuhangaika tangu utotoni, akianzia kuchunga Ndama wa Baba yake, na hata kukutana na Wanyama wakali kama Simba na Chui ambao hawakumfanya chochote
Joseph Butiku: Tukubali tunaye Rais, ameunda Tume itusaidie kujua yaliyotokea
Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere, Joseph Butiku Machi 4, 2026 wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Maridhiano (Maridhiano Day) yaliyofanyika Wilayani Ilemela amewataka Watanzania kukubaliana na uhalisia kwamba nchi tayari ina Rais aliye tayari kwa maridhiano. Akizungumza katika hafla hiyo, amesema kuwa tume iliyoundwa na Rais Samia imeongezewa muda hadi mwezi Aprili, na kuwataka wananchi kuwa na subira ili iwasaidie kujua yaliyotokea Oktoba 29, 2025.
Trump: Sijali kama Iran itashiriki Kombe la Dunia 2026
Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema ‘hajali’ kama Iran itashiriki katika michuano ya Kombe la Dunia la 2026, ambalo litaandaliwa kwa ushirikiano wa mataifa matatu; Marekani, Mexico na Canada itakayoanza Juni 11 hadi Julai 19, 2026. Akizungumza Machi 3, 2026 na tovuti ya Politico, Trump alisema anaona Iran ni nchi iliyoshindwa vibaya. Hata hivyo, kiongozi wa shirikisho la soka la Iran, Mehdi Taj, amedokeza mashaka yake kuhusu uwezekano wa kushiriki mashindano hayo.
Possi: Tanzania inapinga madai ya Washirika wa Kimataifa kuhusu Oktoba 29, wamefumbia macho chanzo
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa (UN), Dkt. Abdallah Possi, katika Kikao cha 61 cha Baraza la Haki za Binadamu, amejibu kauli za Jumuiya ya Ulaya, Uingereza, Uswisi, Sweden, Ireland, Ubelgiji na Norway pamoja na Human Rights Watch na Amnesty International kuhusu matukio ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania. Akizungumza mjini Geneva Machi 2, 2026, Possi alisema Serikali imesikitishwa na kauli hizo alizodai zimechagua matukio bila kuzingatia muktadha.
Back
Top Bottom