kuna taarifa kuwa leo zitto katoa tamko rasmi kuwa ana mpango wa kugombea urais wa tanzania mwaka 2015 na akawaomba wananchi wampe kura nyingi ili apate hadhi ya kuweza kugombea urais wa nchi hii.
Kila la heri mkuu zitto, walau una nia!
Siamini km kweli kuna baadhi ya watu bado wanamwamini zitto.............anaonekana ni mtu anayefanya kitu fulani kwa malengo fulani....mimi binafsi sijawahi kumuamini tena kwa mara ya pili pale nilipositukia kuwa kumbe alinunuliwa na wazee wanne (lowasa,rostam,kikwete,hosea) wa richmond ili atumie kukubalika kwake kuwashwishi watz kununua mitambo ya richmond..................yaani pale tu ndipo nilipomuona zitto ni kijana wa aina gani.........kwa maana nyingine zitto hayupo kwa maslahi ya taifa ni mtaka sifa fulani tu na mvurugaji na wakati wowote anaweza kuhamia ccm kwani hana msimamo huwa anaangalia upepo unavyovuma....ni kweli anaweza kugombea 2015 lakini naamini ana vision kali sana kwani anajua lazima atahamia ccm............
Mkuu unamdisregard Zitto very unfair.Zitto hajui kuwa ktk siasa usiangalie mbele na kuruka kihunzi kilichopo mbele yako sasa. Badala ya kulenga ktk kushinda ubunge kwenye uchaguzi ujao yeye anaanza kutangaza nia za mwaka 2015.....to me that demonstrates poor judgment. Hafai kuwa raisi huyu kwa sababu nyingi tu.....
Hivi niwaulize wana JF mlisha kaaa mkajiuliza hawa watu na kuangalia back ground zao.(Lowassa,Rostam,Kikwete,Hosea,Mbowe,Zitto) hizi kesi ni danganya toto nawambieni
Mkuu unamdisregard Zitto very unfair.
kwa hiyo unasema mwaka 2015 akisimama Zitto hautampa kura yako hata kama CCM wamesimamisha jiwe? na vyama vingine havitasimamisha wagombea
just to say!!!
It si true kwa nini TBC waone hiyo ndiyo habari na kuacha mambo mengine, mbona hawarushi habari nyingi za mikutano ya Slaa, wenyewe wakiona kitu controversial kwa Chadema ndiyo inakuwa habari ili waonekane wanaripoti habari za Chadema. Ni sawa na gazeti la Habari Leo wao wanachoona ni mambo ya ndoa ya Slaa tu huo si uandishi bora ni bora uandishi.Jamani
Mimi naona msubiri kidogo kumhukumu Zitto. Yeye kawauliza watu waliohudhuria mkutano, na wao wakajibu "urais", TBC wakadaka ili kukuza mpasuko ndani ya Chadema. Mimi naona suala hili linakuzwa na vyombo vya habari tu. Mwacheni Zitto apambane kurudi mjengoni, mengine tuwaachie wananchi. Kutokuwepo Jangwani, ni wengi hawakuwepo.
Zitto ana wafuasi wengi sana KIgoma. Kama kweli Zitto kasema hayo maneno yatamaliza Dr Slaa kwa wana Kigoma na kumjenga Kikwette.Wafuasi wake wengi wataona ni bora wamchague Kikwette ili Zitto apate nafasi ya kugombea 2015Mkuu unamdisregard Zitto very unfair.
kwa hiyo unasema mwaka 2015 akisimama Zitto hautampa kura yako hata kama CCM wamesimamisha jiwe? na vyama vingine havitasimamisha wagombea
just to say!!!
Huyu Zitto huyu na mambo yake yenye kuacha maswali mengi;
-Alipendekeza mitambo ya Dowans itaifishwe, baadae akasema inunuliwe.
-Alipendekeza liundwe jopo la majaji kuchunguza Richmond...Rostam naye ali support
-Atafanya maamuzi makubwa ambayo hayajawahi kufanywa na mtu yoyote Tanzania
-Kusifia uongozi wa Kikwete kila kukicha.
-Alisema atamsaidia mgombea wa NCCR kwenye kampeni.
-Role models wake wote ni ccm.
This guy is a time bomb just waiting to go off
It si true kwa nini TBC waone hiyo ndiyo habari na kuacha mambo mengine, mbona hawarushi habari nyingi za mikutano ya Slaa, wenyewe wakiona kitu controversial kwa Chadema ndiyo inakuwa habari ili waonekane wanaripoti habari za Chadema. Ni sawa na gazeti la Habari Leo wao wanachoona ni mambo ya ndoa ya Slaa tu huo si uandishi bora ni bora uandishi.
Conclusion yako butu, unamaana wafuasi wa Zitto wakimpa kura Kikwete ndipo Zitto atapata nafasi ya kugombea 2015, mbona havina uhusiano.Zitto ana wafuasi wengi sana KIgoma. Kama kweli Zitto kasema hayo maneno yatamaliza Dr Slaa kwa wana Kigoma na kumjenga Kikwette.Wafuasi wake wengi wataona ni bora wamchague Kikwette ili Zitto apate nafasi ya kugombea 2015