kwa kusema ukweli kutoka moyoni mimi sio mshabiki wa CHADEMA ila kama ZITTO KABWE angekuwa ametimiza umri wa kugombea urais na angeteuliwa na chama chake kugombea mi naona angefaa kwa mtazamo wangu
Unamshauri akaoe nani?Zito au docter?Namshauri akaoe kwanza.
Kuna taarifa (toka TBC1) kuwa leo Zitto katoa tamko rasmi kuwa ana mpango wa kugombea urais wa Tanzania mwaka 2015 na akawaomba wananchi wampe kura nyingi ili apate hadhi ya kuweza kugombea urais wa nchi hii.
Kila la heri mkuu Zitto, walau una nia! Je, katiba itabadilisha
UKWELI UKO WAZI,KULIKO KMPA ZITTO URAIS BOORA LOWASA...
kwa kweli huyu kijana nimemfuatilia kwa muda mrefu na kugundua ni miongoni mwa viongozi wa chache ambao wana nia ya dhati ya kuwakombania wananchi wa nchi hii ya Tanzania
pia ni kijana mwenye maono na uwezo wa kujenga hoja, ni mtu mwenye kujiamini na kuwa tayari kuusimamia na kuutetea msimamo wake
ni mtu asiendeshwa na emotion kama viongozi wengine, ni kiongozi pekee karibu vyama vyote vya siasa na wasiokuwa na vyama wanamuheshimu na kumpenda
kwa kweli zitto anafaa Lowassa pia ni mchapa kazi na ana maono ya mbali. Kama ndiyo vigezo vyako ni hivyo.
Nilikuwa pale kijiweni maeneo ya kariakoo kuna wajamaa fulani walikuwa wanajadili kuhusu fununu zilizotanda kuwa Zitto amewahi kusema jukwaani kuwa.."nikija tena 2015 sio tena ubunge bali nakuja kuomba kura za urais.." mimi sikumbuki kuwahi kusikia kauli kama hii hivi ina ukweli wowote? je ni kweli Zitto anataka kuwania urais? na imani kuwa Mh Zitto upo humu jamvini hebu tujuze mkuu.
Kwa maana naandaa documentary juu ya mbio za urais 2015 kuhusu Tanzania inahitaji mtu wa namna gani? sasa ili nisije kukuonea au kukupendelea Mh Zitto naomba uniambie hapa mbele ya wanajamvi hivi kuna ukweli juu ya fununu hizi? au ni mambo ya kuzusha tu?
hawez kuwa raiskamuulize mwenyewe!