Elections 2010 Zama Mpya: Blogu Yamu-endorse Dkt Slaa

Mzalendo_Mwandamizi

JF-Expert Member
Dec 12, 2007
1,117
4,764
Blogu hii ya KULIKONI UGHAIBUNI inafungua ukurasa mpya na kuweka historia ya kipekee katika fani ya habari nchini Tanzania kwa kutangaza hadharani kuwa inam-endorse mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema,Dokta Wilbroad Slaa.

Kuna sababu lukuki za kufanya hivyo lakini hapa nitaziorodhesha chache.Kwanza,blogu hii inataka kuachana na unafiki unaojidhihirisha katika baadhi ya vyombo vya habari vyetu ambapo wahusika wanadai hawafungamani na upande wowote lakini matendo yao yanawasuta kwa kupendelea chama tawala huku wakivibinya kwa nguvu baadhi ya vyama vya upinzani.Hapa simsimangi mtu bali nadhani ni vema kuweka msimamo wazi ili kama chombo cha habari ni wakala wa CCM na JK basi ni vema wasomaji wakafahamishwa bayana.

Pili,blogu hii inaamini kuwa kila Mtanzania mwenye uchungu wa dhati kwa nchi yetu anapaswa kumsapoti Dkt Slaa.Katika utumishi wake kwa umma,mgombea huyo wa Chadema ametuthibitishia kuwa ni mtetezi halisi wa haki za wanyonge na ustawi wa taifa letu.Ni nani asiyefahamu namna Dkt Slaa alivyohatarisha maisha yake kwa “kuwavua nguo mafisadi hadharani” alipotangaza ile “list of shame”?Walitishia kumpeleka mahakamani lakini hakuna mmoja wao aliyediriki kufanya hivyo,na sanasana baadhi yao wakaishia kuburuzwa mahakamani na serikali katika “kujikosha”.Blogu hii inaamini kuwa Dokta Slaa ni mkombozi na suluhisho mwafaka la matatizo lukuki yanayotukabili.

Tatu,binafsi naamini kuwa mgombea wa CCM,Jakaya Mrisho Kikwete,ameshindwa kabisa kutimiza matarajio ya Watanzania licha ya ahadi lukuki alizozitoa wakati wa kampeni zake mwaka 2005 na anazoendelea kuzitoa hadi leo.Ungetegemea kuwa mwezi huu wa toba Kikwete angemwogopa Mola wake na kutubu kwa Watanzania kwamba kuna maeneo mengi tu ambapo yeye na chama chake wamewaangusha Watanzania.Lakini kama ilivyo jeuri ya wanasiasa wengi wa Kiafrika,JK ameendeleza wimbo wa “mafanikio ya Awamu ya Nne”.Yani hata kushamiri kwa ufisadi na “uchakachuaji” wa kura za maoni ndani ya CCM ni mafanikio!

Sababu ya nne inashabihiana na hiyo ya tatu.Naamini kuwa afya ya mgombea wa CCM,Jakaya Kikwete,inapaswa kuwekwa kwenye darubini na wapiga kura wanapofanya maamuzi ya kumchagua rais wa awamu ya tano.JK ameshaanguka hadharani mara tatu na kila mara tunapewa excuse moja baada ya nyingine.Mwaka 2005 tuliambiwa “swaumu na uchovu wa kampeni”.Alipoanguka Mwanza tuliambiwa uchovu wa safari (kana kwamba safari hizo ni zile za Wamachinga wanaotembea juani kwa mguu!).Na jana kaanguka tena jukwaani halafu tunaambiwa sababu ni swaumu.Kwani Makamba hajafunga?Au Rais Karume naye “kobe”?Kuna tatizo zaidi ya swaumu au uchovu lakini kwa vile viongozi wetu wamezowea sifa na sio kasoro basi kuweka hadharani kinachomsibu kiongozi huyo inaonekana ni sawa na uhaini.Blogu hii imaanimi kuwa ili Tanzania ijikwamue katika lindi la umasikini wa kutupwa,sambamba na kukabiliana na janga la ufisadi,tunahitaji kiongozi mwenye afya timilifu,kimwili na kiakili.Hatujui JK ameshaanguka matra ngapi asipokuwa hadharani lakini haihitaji hata cheti cha short course ya utabibu kumaizi kuwa JK ana matatizo ya kiafya yanayofichwa,aidha kutokana na uoga wa wanaopaswa kuujulisha umma kuhusu hilo au maagizo yake mwenyewe kuwa “yuko fiti”.All in all,uzito wa matatizo yanayoikabili Tanzania unahitaji mtu aliye fiti kweli,na sio kwa anavyodhani yeye au anavyotaka umma uamini hivyo ilhali ni kinyume na hali halisi.

Kama nilivyoandika mwanzoni,kuna sababu nyingi zilizopelekea blogu hii kuamua kum-endorse Dkt Slaa lakini chache zilizotajwa hapo juu zinawakilisha hizo nyingine.Nawakaribisha ndugu zangu wa Chadema kuitumia blogu hii kufikisha habari kwa Watanzania pasipo hofu ya kuwa habari hizo zitachujwa,kuminywa au “kuchakachuliwa”.

Natambua bayana kuwa baadhi ya wasomaji wa blogu hii sio wafuasi wa Dkt Slaa au Chadema lakini napenda kuwakikishia kuwa endorsement hii haimaanishi kashfa,matusi,dharau au mambo yasiyofaa dhidi ya wagombea wa vyama vingine.Kuweka wazi msimamo wangu haimaanishi chuki dhidi ya vyama hivyo na wagombea wake bali ni imani yangu kuhusu nani anayeweza kuipatia Tanzania “uhuru wa pili” (mapambano dhidi ya Watanzania wenzetu wanaotafuna raslimali zetu zaidi ya alivyofanya mkoloni).

Mwisho,nawahamasisha bloga wenzangu na vyombo vingine vya habari kwa ujumla kuweka bayana misimamo yao ili kuepuka lawama zinazoweza kujitokeza pale habari za vyama flani zinaponyimwa fursa katika vyombo hivyo.Endorsement ya mgombea au chama ni jambo la kawaida katika nchi za Magharibi lakini hii ni mara ya kwanza kwa chombo cha habari cha Kitanzania kufanya hivyo,na kwa hakika najivunia kuweka historia hiyo
 
Yup, blogu hii imewasili katika wakati sahihi, na sijaona kitu tofauti na ukweli kumhusu Slaa!

Kwa mtu kama JK huwezi kuandika kwa ufasaha habari zake coz he keeps changing overnight!
Leo Atakwambia sihitaji kura za wafanyakazi, kesho anasema hakumaanisha hivyo..oooops!..
 
Asante KU, nimetembelea blog yako lakini sijaona sehemu ya ku log in au ni mtu yeyote tu anaweza kupost bila hata kuwa member, kitu kingine jaribu kuweka back ground ya page rangi nyingine sidhani kama rangi nyeusi pale inafaa,

another thing mbona nimeona kuna topic moja tu je kama unataka kupost topic tofauti utafanyaje, ni hayo kwa sasa, but it is a good idea to be open, kuliko kubaki unasena media yangu haifungamani na itikadi yeyote ilhali matendo ni tofauti kabisa, kwa hilo nakupongeza.

nakumbuka hata kwenye uchaguzi uliopita wa UK gazeti moja mashuhuri nchini humo 'THE SUN' kwenye dakika za mwisho liligeuka ghafula na kum endorse Cameron na chama chake na kuwaacha watu wakishangaa akiwemo ex PM Brown, shukran.
 
Mazee blogger,

How do you say "endorse" in Swahili ? If you want to tell people that you are knowledgeable and influential enough to officially endorse a presidential candidate, you should at least have a working command of their language.
 
Yup, blogu hii imewasili katika wakati sahihi, na sijaona kitu tofauti na ukweli kumhusu Slaa!

Kwa mtu kama JK huwezi kuandika kwa ufasaha habari zake coz he keeps changing overnight!
Leo Atakwambia sihitaji kura za wafanyakazi, kesho anasema hakumaanisha hivyo..oooops!..
hakumaanisha hivyo = alikuwa ANATANIA
Ahahahaaaa!!!

 
Mazee blogger,

How do you say "endorse" in Swahili ? If you want to tell people that you are knowledgeable and influential enough to officially endorse a presidential candidate, you should at least have a working command of their language.

In short it has been understood, disregarding that word on the heading!...anyone very conversant with swahili version please do the needful!
 
Nafarijika kuona kuna wenye ujasiri wa kumuunga mkono mgombea wa kambi ya upinzani kupitia chombo chake cha habari.

Naomba rangi ya background isiwe nyeusi, inaumiza macho.
 
Kuunga mkono ni "support" ambayo si sawa na "endorse". Kufagilia ni slang/ colloquial, na hata ukiikubali ni support zaidi ya endorse.

Nipeni mji.

Neno moja linaweza likawa na maana zaidi ya moja kutegemea na muktadha wa matumizi.

Hivi ku endorse check ni sawa na kum endorse candidate?

Hebu ona hapa:

for 'endorse': 1

-ridhia verb Root -ridhi accept, endorse, support, back up, agree, concur, consent, approve, agree to

-ridhi verb consent, approve
kuridhia infinitive Stem -ridhia

Halafu kuna sehemu nimeona maana yake ni ku "idhinisha"....Sasa wasemaje bwana Kiranga....

 
Kuunga mkono ni "support" ambayo si sawa na "endorse". Kufagilia ni slang/ colloquial, na hata ukiikubali ni support zaidi ya endorse.

Nipeni mji.

Mkuu unaonaje ukitutafsiria, sounds like you know the word in question ila unasubiri kupewa mji!
 
Mkuu unaonaje ukitutafsiria, sounds like you know the word in question ila unasubiri kupewa mji!

Tafsiri ya moja kwa moja sidhani kama utapata inayoridhisha na ndio maana nikasema ni muhimu sana kuangalia muktadha la sivyo vitu vitakuwa lost in translation...
 
Back
Top Bottom