Juma Wage
Member
- Sep 8, 2023
- 60
- 201
ALIYEKUWA Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dkt.Wilbroad Slaa amesema pamoja na kutokushiriki katika siasa za jukwaani lakini hataacha kushirikisha uzoefu wake kwa vijana ili wautumie katika harakati zao.
Slaa amezungumza hayo leo katika mahojiano maalum na Mwandishi wa JAMBOTV nyumbani kwake, Mbweni Jijini Dar es Salaam.
"Nina uzoefu wa zaidi ya miaka 40 katika siasa, je niende nao kaburini? Katika kipindi cha mapambano makali ya kutafuta demokrasia kama hiki? hapana" amesema Dkt. Slaa.
Kuhusu kutokuonekana katika maandamano ya hivi karibuni ya Chadema licha ya yeye mwenyewe kushiriki kuhamasisha Dk.Slaa amesema yeye ni mpanga mikakati ambayo ni muhimu zaidi kuliko yeye kuonekana mbele.
"Vita siyo kuwepo mstari wa mbele bali ni mikakati hata Zelensky kule Ukraine unamuona ameenda vitani?" amesema Dk.Slaa.
"Kitendo cha Mbowe na watoto wake kwenda kwenye maandamano ni ujinga uliokubuhu, Kamanda awe kwenye mikakati zaidi kuliko kujitokeza mbele kwa sababu akiuwawa mmekwisha wote" amesema Dkt Slaa.