Laiti ungejua maji yaliingia kupitiwa wapi na ni kwanini yaliingia; laiti ungejua kwamba hapo maji yalipopitia palishafanyiwa 'mradi hewa' wa kupaziba kwa pesa za serikali! Laiti ungejua jinsi wenye migodi walivyowazembe pia kwa upande wao; laiti ungejua jinsi ambavyo Tanzanite One nayo ilizembea kwa sababu zao. Laiti yote yangefanyika kwa wakati mwafaka kabla na hata mara baada ya tukio. Pasingekuwa kuwa na vifo vingi hivyo vya vijana wana-apollo, na wala tusingekuwa tunasubiria sasa hivi kufukuliwa kwa maiti zilizoharibika vibaya. Nikipata wasaa siku moja nitaandika niliyoyaona kwa macho yangu. For now, everything remains a wish. And If wishes could have been horses, even beggars would ride!
JJ
Tatizo ka kushindikana muafaka Zanzibar - Kazi ya Mungu
Jinsi tulivyokwapuliwa BoT - Kazi ya Mungu
Ditopile alivyomtwanga jamaa risasi - Kazi ya Mungu
Tatizo la njaa kwenye nchi ya maji ya kutosha - Kazi ya Mungu
Tatizo la nishati - Kazi ya Mungu
Hivi huyu Mungu anayefanya kazi hasi namna hii kwanini tumuamini? Yaani amekula njama dhidi ya Tanzania na watu wake?
I think poor management, safety and security checks, obsolete technology should come first and foremost, kabla ya kumbebesha lawama Sir God. Mvua isiponyesha tunamtupia lawama god, ikinyesha na kusababisha disaster kama hizi tunamlaumu God, wapi na wapi wandugu?? Sisi wenyewe ndio chanzo cha matatizo.
Hata hivyo lililonigusa ni lile la kusema kuwa "tumekuja hapa kutafuta chochote, lakini hatukutegemea haya, sisi tunapanga na Mungu anapanga".. Kwa kadiri nilivyomuelewa ni kuwa yaliyotokea Mererani ni kazi ya Mungu
na aliahidi kuwa baada ya uchunguzi na utafiti wa kina basi machimbo hayo yatafunguliwa mara moja.
Maisha yako so cheap Tanzania.
JK Ka orrder siku 3 za rescue, baada ya kukaa kwenye kikao cha CCM apparently alichofikiri kina umuhimu zaidi ya rescue work, kwa siku kadhaa.
Wachimbaji wanadai wapewe hela zaidi (40,000 instead of 10,000 per body), hawa ni watu waliokuwa wanafanya nao kazi!
Hapa ndipo tulipofikia. Nilikuwa naangalia blog ya photojournalist mmoja kampiga picha kijana mmoja mdogo tu, anasema huyo kijana "alishapasua" akawa na hela sana kiasi akawa anakodisha ndege na kuzunguka nayo sana mbugani huko akitanua na ku spend, halafu kamaliza hela karudi tena shimoni in the hopes za kupasua tena. Kazi ya hatari kama hii.Hii ndiyo desperation tuliyo nayo kutokana na elimu ndogo tunayowapa watu wetu, no investment no hopes of taking things to the next level, just subsistence existence, hand to mouth with the paltry millions, shortchanged by the government, shortchanged by the market, caught up in the life, sheer desperation.
One more reason to unseat CCM and Kikwete.
Maafa yametokea, Waziri Mkuu ametuma mawaziri watatu haraka sana, na hatimaye rais mwenyewe ameenda, ametopa poel na ameahidi uchunguzi kujua chanzo cha maafa, unless kuna something I am missing, hivi amekosea nini hapo wakuu?
Naomba kuelimishwa kidogo?
Maafa yametokea, Waziri Mkuu ametuma mawaziri watatu haraka sana, na hatimaye rais mwenyewe ameenda, ametopa poel na ameahidi uchunguzi kujua chanzo cha maafa, unless kuna something I am missing, hivi amekosea nini hapo wakuu?
Naomba kuelimishwa kidogo?
FMES, tatizo ni kwamba huwa marais na viongozi wanatumia tragedy kama hizi to make a statement yaani kuhakikisha kwa mfano that things get done. Issue ya safety kwa mfano ingeweza kuibuliwa na angeweza kuja na statement ya kuwa katika siku za hivi karibuni watatangaza conditions mpya kwa wamiliki wa mgodi ambayo ni lazima wafuate kuhusiana na usalama kwa wafanyakazi wa migodini. Ni lazima azungumzie responsibility ya wamiliki. Unafikiri vitalu vile havina wenyewe? Vina wamiliki ambao ni watanzania wenzetu wengine wanatanua na ma VX na ma Vogue Dar na Arusha na wanawatumia vijana wetu kuchimba. We have to talk about this, siyo siku zote tunawasema tu akina AFGEM! Na this tragedy is a good reason to start that discussion, siyo kusema eti Mungu!Maafa yametokea, Waziri Mkuu ametuma mawaziri watatu haraka sana, na hatimaye rais mwenyewe ameenda, ametopa poel na ameahidi uchunguzi kujua chanzo cha maafa, unless kuna something I am missing, hivi amekosea nini hapo wakuu?
Naomba kuelimishwa kidogo?
Haya njoo kwenye vivuko vyetu hapo, tukiwa tunakumbuka ajali ya kivuko kule kilombero, leo mavivuko yetu katika Tanzania yetu ni mabovu kupindukia tena sana, lakini serikali inafanya usanii kwenye hili mpaka watu watakapozama ndio watasema mapenzi ya Mungu.
Na hapo ni hao 60 wamekufa kwa pamoja ndio maana hata kikwete kaenda, lakini kwenye jiji la Dar es Salaam, watu kila siku ya mungu wanakufa kwa ajali za barabarani tena wengi tu, nazo wanasema ni mapenzi ya Mungu.
Haya pamoja na haya yote, serikali hata haina jinsi ya kuwaokoa watu wake wakipatwa na majangaa kama haya, ebu fikilia Mgodi kama ule eti hauna hata First aid Kits za kusaidia wachimbaji wadogo wadogo, pili hata machine za kutolea maji hakuna!! LOOO
Nah....bad parallelism....because your concept is predicated on a conspiracy theory...