Zaidi ya watanzania 100 wafariki Mererani

nakubaliana na Neno kazi ya Mungu...ila kwa hali ya mererani kwa sasa ni ngumu sana kuwaunganisha vijana au wachimbaji wadogo wadogo waweze kujiunda vikundi wakatafuta pesa wa ma bank ili waweze kuchimba kwa utaalamu kidogo na kutumia njia za kisasa....ili kuepukana na majanga kama hayo..ingawa ukiongea nao wanakuwa hawakuelewi hata wanasema inachukua miaka 10 au zaidi ndipo majanga yanapotokea...ni bahati mbaya tu........ukisema wajiunge..kila mchimbaji mdogo anakuwa mbinafsi na hawana muda kupoteza kufuatilia urasimu uliopo hadi waweze kuanzisha na kupewa fund............
 
Njia rahisi ya kukwepa wajibu na kuficha uvivu wa kufikiri ni kumsingizia Mungu kwa kila jambo baya linalotokea.
 
Sikubaliani na maneno ya jangala kikwete msanii wa sanaa za maonyesho ya kikundi cha ccm kwa sababu Mungu hapangi vifo vya maangamizi kwa binadamu. Siku zote binadamu (hasa waafrika)huwa tunatafuta sababu kuhalalisha kushindwa kwetu kuonekane kosa sio letu. Yeye akiwa kama rais anapaswa kuangalia mambo kwa njia za kisayansi na sio kujifanya yeye ni mzee wa dini.
 
Mkjj:
Of course uvivu wa kufikiri unatulazimu tuseme ni kazi ya Mungu hata kama mtu akiona treni linakwenda spidi ya maili 100 kwa saa na akiamua kujitupa mbele yake kwa maksudi au kwa uzembe wake!

Ni makosa kabisa kwa rais kudhani kuwa mikasa ya ajali kama hizi zinazozuilika kwa kuwa na sheria na taratibu nzuri za usalama katika seeeeemu za kazi.

Hapa alitakiwa asisitizie kwa nguvu kabisa kuwepo na sheria, na zifuatwe katika shughuli za uchimbaji wa madini.

Boti mbovu au panakuwepo na ukiukwaji wa taratibu za kiasi cha wasafiri; inaua watu - eti kazi ya Mungu?

Kazi ya Mungu ni pale ambapo utakuwa umejiridhisha kabisa kuwa umefanya kila linalowezekana katika uwezo wako kulinda usalama wa wananchi wako; pakitokea ajali, unaweza ukasema 'Kazi ya Mungu' haizuiliki.
 
Ni pointi nzuri Mwkjj!
How much blame to we assign Muumba wetu, and how much to ourselves? Mimi nadhani the best is to take full responsibility, kwani siyo tu serikali bali all players lazima waangalie walikuwa na nafasi gani katika kupelekea hali hii ya kuhatarisha hivyo maisha ya hawa vijana.
I think invoking God is the easy way out! But we should know better.
Lakini kuwalaumu wachimbaji hawa wadogo pekee si sahihi, wajiunge kwa sababu gani? Hata wakijiunga katika vikundi watapata wapi mkopo wa benki? Mabilioni ya Kikwete? Ni mazingaombwe. Mi nadhani kwamba kama kungekuwa na njia ya wajasiriamali wa kitanzania kuanzisha makampuni ya maana ya migodi na kuchukua mikopo ya Benki ya Dunia etc na kuendeleza vitalu vyao, maafa yasingetokea. Naomba kuuliza maafa haya yalitokea kwenye vitalu vya AFGEM au Tanzanite ONe? Na kama siyo, basi nani wamiliki wa vitalu hivyo? Ninavyofahamu wamiliki wa small scale mines ni matajiri wa kibongo wanaodai kuwa 'small scale miners' kama akina Mengi. They should do better. Inabidi wawajali wachimbaji wao. (I stand to be corrected kuhusu umiliki wa vitalu kama nimekosea)
 
Mkjj:
Of course uvivu wa kufikiri unatulazimu tuseme ni kazi ya Mungu hata kama mtu akiona treni linakwenda spidi ya maili 100 kwa saa na akiamua kujitupa mbele yake kwa maksudi au kwa uzembe wake!

Ni makosa kabisa kwa rais kudhani kuwa mikasa ya ajali kama hizi zinazozuilika kwa kuwa na sheria na taratibu nzuri za usalama katika seeeeemu za kazi.

Hapa alitakiwa asisitizie kwa nguvu kabisa kuwepo na sheria, na zifuatwe katika shughuli za uchimbaji wa madini.

Boti mbovu au panakuwepo na ukiukwaji wa taratibu za kiasi cha wasafiri; inaua watu - eti kazi ya Mungu?

Kazi ya Mungu ni pale ambapo utakuwa umejiridhisha kabisa kuwa umefanya kila linalowezekana katika uwezo wako kulinda usalama wa wananchi wako; pakitokea ajali, unaweza ukasema 'Kazi ya Mungu' haizuiliki.

Kazi na asante ya CCM na msaada kwa wahanga ndiyo imeishia hapo .Hivi makampuni makubwa na mashine zao si wako hapo poa walizitumia kumwaga maji nje na kuokoa maisha ya baadhi yao ama ni kazi ya Mungu pia kupata vyombo vya uokoaji ?Tujifanye mambo haya yamewakuta wazungu wawekezaji JK si angeeda LIVE kwenye TV na Radio ama kukimbilia huko kuliko alivyo fanya kwa hawa wahanga ? Vyombo vya habari Tanzania vimetoa nafasi kiasi gani kwa hawa wahanga ?
 
Njia rahisi ya kukwepa wajibu na kuficha uvivu wa kufikiri ni kumsingizia Mungu kwa kila jambo baya linalotokea.

Kwa kweli, tunawaombea heri kwa Mungu marehemu wote. Lakini kwa ujumla ya maafa ya Mirerani kama umepata wasaa wa kujua yalivyotokea basi utakubaliana nami kwamba si kazi Mungu. Ni kazi ya binadamu! Swali la kujiuliza tu ni kwanini Mwenyezi Mungu anaruhusu binadamu kuwa wazembe kiasi cha kupoteza maisha ya binadamu wenzao?

JJ
 
Mkjj:
Of course uvivu wa kufikiri unatulazimu tuseme ni kazi ya Mungu hata kama mtu akiona treni linakwenda spidi ya maili 100 kwa saa na akiamua kujitupa mbele yake kwa maksudi au kwa uzembe wake!

Ni makosa kabisa kwa rais kudhani kuwa mikasa ya ajali kama hizi zinazozuilika kwa kuwa na sheria na taratibu nzuri za usalama katika seeeeemu za kazi.

Hapa alitakiwa asisitizie kwa nguvu kabisa kuwepo na sheria, na zifuatwe katika shughuli za uchimbaji wa madini.

Boti mbovu au panakuwepo na ukiukwaji wa taratibu za kiasi cha wasafiri; inaua watu - eti kazi ya Mungu?

Kazi ya Mungu ni pale ambapo utakuwa umejiridhisha kabisa kuwa umefanya kila linalowezekana katika uwezo wako kulinda usalama wa wananchi wako; pakitokea ajali, unaweza ukasema 'Kazi ya Mungu' haizuiliki.

Mimi siamini katika mungu na naamini mungu anatumika kama scapegoat, kama carpet tunalotumia kufunika aibu yetu ya kutojua majibu ya msawali magumu ambayo hatuwezi kuyajibu.

How did we get here, kazi ya mungu, usiulize, utakufuru bure.

Kwa nini watu wanakufa kwa sababu zinazoweza kuzuilika, kazi ya mungu haina makosa.

Kwa nini hatupati mvua, kazi ya mungu, let us pray for rain.

Mwisho tutasema kwa nini watoto wana utapiamlo, kazi ya mungu.

Tunakosa tofauti na wale watu walioishi in the pre-scientific era waliofikiri radi ni hasira ya mungu.

Tutaacha kufanya kazi kwa bidii na kusema kwa nini tu masikini, kazi ya mungu.

Hamna cha kazi ya mungu wala nini, hatuna safety standards wala quality control.Now do not get me wrong, I believe in chances, fallibility of science and probability and one not being completely able to control the future, it is idiotic not to believe so, but I also believe one can control a lot, including the probability of tragedies occurring and the overall numbers of casualties.

Hata kama mtu haamini mungu, lakini ukienda sehemu yenye safety standards za hali ya juu halafu watu wanakufa kwenye ajali (ajali zitakuwepo tu kutokana na the power of entropy and the uncontainable effects of the arrow of time coupled with the unforeseen) kwa hiyo my thing ni kuwa kuna situations nyingine mtu unaweza ku tolerate "kazi ya mungu tu" kama euphemism ya "bwana haya mambo mengine ni mambo ya probability tu, na mambo ya entropy, kwamba it is against the second law of thermodynamics for any system not to be prone to disaster and inefficiency 100%, kwa hiyo kama alivyosema Kalamu na wengine hapo juu, naweza kusamehe hizo kauli za "kazi ya mungu" kama sisi tumeshafanya kazi yetu ipaswavyo tukamuachia "mungu" (in my case probability and entropy and the unknown the unforeseen and the unpredictable)

They say god help those who help themselves.

Sasa sisi tumeshajisaidia vipi wenyewe mpaka tumpe lawama huyu mungu?
 
Bahati nzuri tu ni kwamba Mungu si binadamu......ila pangekuwa hapatoshi watu kumsingizia kazi ambazo hajafanya. Ni bahati mbaya kama ambavyo watu wanaweza kuita....ila mi maono yangu ni uzembe wa hali ya juu!!! Kwani hiyo ni mara ya kwanza kutokea Tanzania?...Utasikia wenye mamlaka wanasema tunajufunza kutokana na makosa....sasa hapa wanajifunza nini tena?

Hisia zangu!
 
Tatizo ka kushindikana muafaka Zanzibar - Kazi ya Mungu
Jinsi tulivyokwapuliwa BoT - Kazi ya Mungu
Ditopile alivyomtwanga jamaa risasi - Kazi ya Mungu
Tatizo la njaa kwenye nchi ya maji ya kutosha - Kazi ya Mungu
Tatizo la nishati - Kazi ya Mungu

Hivi huyu Mungu anayefanya kazi hasi namna hii kwanini tumuamini? Yaani amekula njama dhidi ya Tanzania na watu wake?
 
I think poor management, safety and security checks, obsolete technology should come first and foremost, kabla ya kumbebesha lawama Sir God. Mvua isiponyesha tunamtupia lawama god, ikinyesha na kusababisha disaster kama hizi tunamlaumu God, wapi na wapi wandugu?? Sisi wenyewe ndio chanzo cha matatizo.
 
Hajaumnganisha haya na hotuba zake za mwezi ? Je kwa yeye kuchelewa kufika katika eneo la janga nako ni kazi ya Mungu ?
 
Maisha yako so cheap Tanzania.

JK Ka orrder siku 3 za rescue, baada ya kukaa kwenye kikao cha CCM apparently alichofikiri kina umuhimu zaidi ya rescue work, kwa siku kadhaa.

Wachimbaji wanadai wapewe hela zaidi (40,000 instead of 10,000 per body), hawa ni watu waliokuwa wanafanya nao kazi!

Hapa ndipo tulipofikia. Nilikuwa naangalia blog ya photojournalist mmoja kampiga picha kijana mmoja mdogo tu, anasema huyo kijana "alishapasua" akawa na hela sana kiasi akawa anakodisha ndege na kuzunguka nayo sana mbugani huko akitanua na ku spend, halafu kamaliza hela karudi tena shimoni in the hopes za kupasua tena. Kazi ya hatari kama hii.Hii ndiyo desperation tuliyo nayo kutokana na elimu ndogo tunayowapa watu wetu, no investment no hopes of taking things to the next level, just subsistence existence, hand to mouth with the paltry millions, shortchanged by the government, shortchanged by the market, caught up in the life, sheer desperation.

One more reason to unseat CCM and Kikwete.
 
Pundit you have said it all .Mie sina la kusema ila nangoja wadanganyika kuamka na kuiondoa CCM n.
 
Kwa kweli, tunawaombea heri kwa Mungu marehemu wote. Lakini kwa ujumla ya maafa ya Mirerani kama umepata wasaa wa kujua yalivyotokea basi utakubaliana nami kwamba si kazi Mungu. Ni kazi ya binadamu! Swali la kujiuliza tu ni kwanini Mwenyezi Mungu anaruhusu binadamu kuwa wazembe kiasi cha kupoteza maisha ya binadamu wenzao?

JJ
Kaka hakuna mtu ambaye hatokufa, ni mapenzi ya mungu kuwa kila binadamu ataonja umauti.swala la uzembe wa mtu hakuna hapo labda uwe ni uzembe wa marehemu.wao waliona hali mbaya ya hewa wakadai kuingia hivi hivo.Na jana wamemuomba JK kuwa waruhusiwe kuingia tena .wanaharaka ya nini????hapo imani zao zina wapa watapata madini mengi zaidi.
 
Laiti ungejua maji yaliingia kupitiwa wapi na ni kwanini yaliingia; laiti ungejua kwamba hapo maji yalipopitia palishafanyiwa 'mradi hewa' wa kupaziba kwa pesa za serikali! Laiti ungejua jinsi wenye migodi walivyowazembe pia kwa upande wao; laiti ungejua jinsi ambavyo Tanzanite One nayo ilizembea kwa sababu zao. Laiti yote yangefanyika kwa wakati mwafaka kabla na hata mara baada ya tukio. Pasingekuwa kuwa na vifo vingi hivyo vya vijana wana-apollo, na wala tusingekuwa tunasubiria sasa hivi kufukuliwa kwa maiti zilizoharibika vibaya. Nikipata wasaa siku moja nitaandika niliyoyaona kwa macho yangu. For now, everything remains a wish. And If wishes could have been horses, even beggars would ride!

Mnyika unaonekana kuna mengi hapa na mimi nilijua haya hebu saidia kuweka picha maan magazeti ya nyumbani naona hayaoni kama hii ni habari .
 
I think poor management, safety and security checks, obsolete technology should come first and foremost, kabla ya kumbebesha lawama Sir God. Mvua isiponyesha tunamtupia lawama god, ikinyesha na kusababisha disaster kama hizi tunamlaumu God, wapi na wapi wandugu?? Sisi wenyewe ndio chanzo cha matatizo.

Na wale walioiba BOT ni kazi ya shetani!! kwaiyo tuyaaache yapitE kwa kuwa sasa wamesafishika tumuachie mungu...

kikwete naomba kazi..check nilivyo weka msala vizuri..LOL
 
Hajaumnganisha haya na hotuba zake za mwezi ? Je kwa yeye kuchelewa kufika katika eneo la janga nako ni kazi ya Mungu ?

nimecheka sana kusoma hii.... I love jamboforums kwa kweli! Hivi kikwete ameanza lini kumsukumia mungu lawama kiasi hiki?!
 
Maiti ikitolewa shimoni leo mchana zilitoka tano bado 20 kwenye shimo hili! Maji ni mengi n amchanga umefunika wengine Mungu saidia watatoka. Ni shimo la Germstone resources Limited.

Kwenda chini ilikuwa lazima Nyoka na wanaapolo wavae vizuia haufu lakini wengine waliingia hivyohivyo
.

Polisi wakilinda kuimarisha ulinzi katika moja ya migodi watu walikuwa wengiwakitaka kusaidia na wengin kupata riziki si mnajua watoto wa mjini! Walidhbitiwa na vijana wa kamanda Tossi.

Wanaapolo wakiwa wamejipumzisha baada ya kazi ngumu huku wakisubiri majibu ya ndugu zao waliofariki dunia mgodini.

Hapa ndio sehemu ya machimbo ya Merelani Block B ambako watu karibu wote waliuawa.

Jamani hata kama ni washikaji lakini serikali imeshimndwa kuleta gloves hawa wavae kuopoa maiti, maiti zenyewe ziko kweny emaji halafu hiyo harufu, imagine hawa wameingia kavukavu!

Hawa jamaa wana apolo kiboko siwafafanui lakini soma meseji zao ubaoni!

Ndugu wa marehemu wakishindwa kuhimili harufu ya miili inayoopolewa sidhani kama hili zoezi litafika siku mbili!

Mwanaapolo akivaa gloves kwenda kuokoa miili ya wenzake waliofunikwa katika moja ya mashimo hapa Mererani. Niliamua jana kuja kuona mambo kw amacho yangu!

Wachimbaji( wanaapolo) wakiopoa mwili wa mmoja wa wachimbaji wenzao, jamani hata gloves hawana harufu ni kali imenikumbusha nilipoenda kupigapicha za maiti wa ajali ya treni Dodoma.Kamati ya maafa iko huko!

Wanaapolo wakiingiua mgodini kuokoa wenzao waliofukiwa na kifusi baada yamaji kujaaa, jamani inatisha najilaumu kwanini nimerudi Mererani tena
.

Hapa ndio mbali na duniani chini ya shimo baada ya washikaji kufa nimekumbuka nilienda kama 450m underground kupata picha hizi lakini washkaji wote wako shwari.

Jamaa huyu wa mbele nilimwadikia makala anaitwa Kambi (Macharii wa AR watakuwa wanamfahamu) aliwahi kupata jiwe( Tanzanite) ikatisha! Alikuwa anakodi ndege kwa siku kadhaa kuzunguka sehemu mbalimbali sasa hivi karudi tena shimoni kuangalia kama atapata tena
.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom