Susuviri
JF-Expert Member
- Oct 6, 2007
- 3,713
- 888
Wakuu Rufiji, Susuviri, na Pundint,
Heshima mbele na nimewasikia, naomba kuuliza tena, hivi kweli sheria ikifuatwa inavyotakiwa huko kwenye migodi ya wazawa kuna hata mmoja utakaobaki wazi? Sasa what that will do kwa ajira za wananchi wanyonge?
Maana wakuu mkumbuke kuwa hii ni bongo, sio majuu, mimi ninaaamini ukiamua kufuata sheria hasa za kila sekta, huenda itabidi ku-close bongo nzima sasa itakuwaje?
I respectfully disagree, sheria ni lazima ifuatwe! Kama huna uwezo usifanye shughuli hizo. Naomba kuuliza: kama mimi leo nikiamua kujiingiza katika taaluma ya udaktari na nikaanza kutibu watu nyumbani na kuwapasua ubongo nikisema 'natafuta kula'itakuaje? Na migodi nayo ina sheria zake na ni kwa ajili ya kulinda afya na uhai ya wafanyakazi wa migodini. Hakuna mjadala! Kama huna uwezo nayo, find another line of business. Mimi nakwambia matajiri wa Merarani wana pesa ya kutosha na siyo wao wanaoingia migodini. Badala ya kuwanunulia mahawara wao magari na nyumba wange-invest kwenye migodi.