Ndimile Kilatu: Malighafi ya kutengenezea Sabuni ndiyo chanzo cha Kusambaa kwa Mapovu Morogoro

Heparin

Senior Member
Sep 24, 2021
128
421
Ofisa Afya Manispaa ya Morogoro, Ndimile Kilatu amesema maofisa wa idara hiyo walifika eneo la Tubuyu B, Morogoro kufutilia chanzo cha mapovu katika korongo linalopitisha maji wakati wa mua na kuyapeleka Mto Ngerengere na kubaini ni malighafi ya kutengenezea sababu, iliyomwagika Januari 17, mwaka huu kwenye maegesho ya malori katika eneo la Nane Nane.

"Mvua iliyonyesha siku mbili hizi imesafisha mabaki ya kemilikali hiyo na kuipelekwa kwenye vyanzo vya maji katika Mto Ngerengere na kutokana na maporoko ya maji, imezalisha povu. Tunafanya uchunguzi wa kimaabara tutatoa majibu," alisema Kilatu akiliambia gazeti la Mwananchi.

JamiiCheck, Jukwaa la uhakiki wa Maudhui linaloendeshwa na JamiiForums lilitolea ufafanuzi wa Madai haya mapema Januari 21, 2024 ambapo katika ufafanuzi wake baada ya kufanya ufuatiliaji wa kina, lilibainisha kuwa hayo hayakuwa mawingu kama ilivyodhaniwa na wakazi wa Morogoro, bali kemikali za kutengenezea sabuni zilizodondoshwa na magari yanayopita eneo hilo.

Soma: UZUSHI - Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha zasabanisha kudondoka kwa Mawingu Mkoani Morogoro
 
Back
Top Bottom