mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,076
- 4,113
Mvua zinazoendelea kunyesha nchini zimezidi kuleta athari kubwa kwa wananchi, uchumi na miundombinu. Mamlaka ya hali ya hewa imetangaza uwepo wa mvua mikoa ya Morogoro Iringa, Ruvuma, Songwe, Mbeya na Njombe nk, hivyo kama raia wema ni vyema kupeana taarifa barabara korofi ambazo zimekumbwa na mafuriko ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.
Taarifa nilizonazo, maeneo ya Mikese, Kwa Mangwair, Makunganya, Silwa na Mtanana, kote maji yanakatisha barabarani. Hivyo kama una safari itakayokuta kupita njia hizo vizuri ukaenda kwa tahadhari. Usidharau kabisa maji yanayokatisha barabarani.