Yaliyojiri Mkutano wa Kihistoria wa CHADEMA Mwanza, Ulirushwa live kwenye TV na Radio

Utakuwa mkutano mkubwa wa aina yake kuwahi kufanyika kwa siku za hivi karibuni katika shughuli za kisiasa nchini.

Mkutano huo utakaofanyika Jumatano, Julai 22, 2015 kuanzia majira ya saa 8 mchana utahudhuriwa na Viongozi wakuu wa Chama wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Dk. Slaa, Makamu Mwenyekiti Bara Prof. Abdallah Safari.

Viongozi wengine waandamizi watakaokuwepo ni; NKMZ John Mnyika, NKMZ Salum Mwalimu, Mjumbe wa KK Prof. Baregu, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Arcado Ntagazwa na Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa Halima Mdee, ambao wote watahutubia taifa kutokea Uwanja wa Magomeni jijini Mwanza.

Waliokuwa wabunge wa CCM, wapiganaji Mzee James Lembeli na Easter Bulaya watakuwepo Uwanja wa Magomeni. Tusimalize utamu hapa kuhusu watakachosema.

Mkutano utatangazwa live kwa masaa 3 kupitia ITV na Radio One.

Wakati Watanzania wengine watapata fursa ya kufuatilia matangazo ya moja kwa moja kupitia tv na radio, wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa watawakilisha kwa kufika kwa wingi uwanjani hapo kusikia hotuba zitakazotoa mwelekeo wa taifa hasa tunapoelekea kwenye Uchaguzi mkuu.

Wametangulia na kufuli, tutakuja na ufunguo.

Makene


Updates...

Maandamano ni makubwa mno. Haijawahi kutokea. Kutokea Uwanja wa Ndege wa Mwanza kuelekea mjini ambapo ni mwendo kama wa dakika 10 hivi hadi sasa msafara umetumia masaa mawili na bado haujafika mjini.

Mji mzima unanukia CHADEMA, Kanda ya Ziwa at its peak for changes.

Clear signs of quest for changes for the better future under safe hands of the committed and responsible leaders.

Tutaanza kuwawekea picha punde. Hapa hapa




attachment.php

attachment.php

attachment.php

attachment.php

attachment.php

attachment.php

attachment.php

attachment.php

Mapokezi ya mapadlocks mbona pikipiki zilikuwa chache sana...au wafuasi wake hawana pikipiki...???
 
Nashangaa watu wanasema ni mtendaji mzuri...kwa lipi hasa?

Eti Barabara? Zipi....

Morogoro Road(BRT)??? Nyembamba gari kubwa mbili haziwezi kwenda pamoja?

Wanaomshabikia magufuli ni malimbukeni ambao hawajui nchi nyingine wana barabara za aina gani...mtu anatoka mwenge, mbagala, mbeya, Arusha....basi anaona dili? Wakati nchi za wenzetu wana njia tano hadi sita upande mmoja tu...hata Kenya, Ethiopia kwa mfano tu.

Magufuli sio dili hata kidogo....coz akiingia CCM ni ile ile tu...ukoo wa panya.

Naomba kudeclare interest....baba yangu ni mjumbe wa NEC ya CCM ila namuambiaga hivi hivi na anakubali CCM ni Kiwanda cha ufisadi kuwamaliza waTanzania....ila hana jinsi.

Nikweli tumesoma, tunaishi vizuri ila inaniuma sana coz waTanzania wenzangu ni binadamu na wana haki yakuishi vizuri pia. Watu hawana uhakika wa mlo mmoja kwa siku? A very big sin

I hate many people suffering coz of few people....better few people suffer coz of many....

Natamani ningezaliwa nje ya CCM hii dhambi isinikute

Mungu naomba Huruma yako.

Regards, to Tanzanians
 
ccm kwisha kanda ya ziwa


wewe unadhani kanda ya ziwa ni kama kanda nyingine ,
kawaulize cdm kilichowapa kiarusi cha muda na kuja mwanza wakati bado hata mgombea wao hawana na kutudanganya kwamba watamtangaza mgombe kumbe ni uongo tu,


magufuli ni noma,
 
Sijui mtaficha wapi sura zenu siku Magufuli anatangazwa kuwa ndio rais wenu?
Hapo ndipo mtakapo jidharau kuwa usijivunie kuni la watu wanapokuja kwako sio wote wanakupenda

Mkuu kwa lile goli la mkono alilolisema Nape wala sina wasiwasi kwamba Magufuli atatangazwa Rais....
 
Mkuu jokaaKuu wewe ni Mwandamizi humu...sasa unapoandika ''Magufuli na CCM ndiyo waliopitisha sera mbovu ya madini iliyopelekea dhahabu ya kanda ya ziwa ivunwe na makampuni ya nje huku wananchi hao wakibaki mikono mitupu'' halafu wakati huo huo unampinga Tundu Lissu kusema Magufuli ni FISADI tukueleweje?Kumbuka Pombe ni member of Cabinet vipindi vyote vya toka kuuza nyumba za umma mpaka bunge la katiba mpaka juzi kati Escrow.....unawezaje kumtenga huyu na mafisadi?Prof.Safari ameonyesha jinsi Magufuli asivyoheshimu mamlaka, jinsi alivyomtoa rushwa huko Igunga kuwaambia wananchi wachague CCM ndio wapewe mahindi ya msaada. Sasa utamwita nani huyu
 
Last edited by a moderator:
Leo akirudisha kadi ya CCM ktk mkutano wa CHDEMA uliorushwa live na ITV akiambatana na Ester Bulayo wa CCM,Lembeli aliimba hivi,
Kataaaa kata
Kata
kata usiogope
Kata
Kataaa mafisadi
Kata
Kataaa CCM
Kata.
Sasa naomba tuimbe wote,moja,mbili,tatu anza kazi

Sijawahi kuona mzee ana njaa km hyu! Na mwaka huu ataisoma namba.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom