Dkt. Nchimbi: Rais Samia anaungwa Mkono na wana CCM wote

abdulatifujr

New Member
Mar 20, 2024
1
2
#HABARI: Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, amesema kuwa Watanzania wote kwa ujumla wao wanajivunia uwezo mkubwa wa kiuongozi, anaouonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan ndani ya miaka 3 ya uongozi wake, ukijidhihirisha kwa namna anavyoiongoza nchi, kwa ajili ya maendeleo ya watu, ustawi wa jamii na kuimarisha utaifa nchini.

Akizungumza mbele ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 11 wa Makatibu Wakuu wa Vyama Rafiki vya Ukombozi wa Kusini, unaoendelea katika siku yake ya pili, kwenye Mji wa Victoria Falls, nchini Zimbabwe, Jumanne, Machi 19, 2024, Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk. Nchimbi, amesema Chama Cha Mapinduzi pia kinajivunia uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa jinsi anavyoendelea kuiongoza Serikali katika kutafsiri kwa vitendo utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 – 2025, akisisitiza kuwa CCM na wanaCCM wanamuunga mkono bega kwa bega.

“Kabla sijaanza kuwasilisha hapa…kwa ruhusa yako Mwenyekiti wa Kikao, imekuwa kama bahati nzuri zilizogongana leo…naomba niwataarifu Wajumbe wa Mkutano wa Kumi na Moja wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Ukombozi wa Kusini mwa Afrika kwamba leo ni maadhimisho ya mwaka wa tatu tangu Mhe. Samia Suluhu Hassan aliposhika Madaraka ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania miaka mitatu iliyopita.

“Kwa kweli ninajivunia sana Rais Samia Suluhu Hassan, si kwa sababu tu mimi ni mpigania haki za wanawake, bali kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa uongozi mzuri anavyoendelea kuiongoza nchi yetu ya Tanzania.

Kutokana na hilo, Chama Cha Mapinduzi kinajivunia sana uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, na Watanzania kwa ujumla wetu tunajivunia sana kuongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa uwezo wake mkubwa ambao ameuonesha ndani yah ii miaka mitatu,” amesema Katibu Mkuu Balozi Dk. Nchimbi.

Dk. Nchimbi pia alitumia nafasi hiyo kuwahakikishia wajumbe kuwa kutokana na kuwa mwanamajumui wa kweli wa Afrika, Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ana dhamira ya dhati kuimarisha na kuboresha uhusiano wa nchi na vyama rafiki katika ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika na kwamba anafuatilia mkutano huo wa 11 wa Makatibu Wakuu wa vyama hivyo kwa ukaribu, huku pia akiwaomba wajumbe kuungana nae kumtakia kila la heri Mhe. Samia na kumuunga mkono, ombi ambalo lilipokelewa na kukubaliwa na wajumbe.

1710925652133.png
 
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amesema wananchi wote wa Tanzania kwa ujumla wake wanajivunia uwezo mkubwa wa kiuongozi anaouonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ndani ya miaka mitatu (3) ya uongozi wake, ukijidhihirisha kwa namna anavyoiongoza nchi kwa ajili ya maendeleo ya watu, ustawi wa jamii na kuimarisha misingi ya utaifa.

Akizungumza mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa 11 wa Makatibu wakuu wa vyama rafiki vya ukombozi wa Kusini mwa Afrika unaoendelea kwenye mji wa Victoria Falls nchini Zimbabwe Machi 19.2024, Balozi Dkt. Nchimbi amesema CCM inajivunia uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jinsi anavyoendelea kuiongoza serikali katika kutafsiri kwa vitendo utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 – 2025 akisisitiza kuwa CCM na wanachama wake wanamuunga mkono.

"Kabla sijaanza kuwasilisha hapa kwa ruhusa yako Mwenyekiti wa kikao, imekuwa kama bahati nzuri zilizogongana leo, naomba niwataarifu Wajumbe wa Mkutano wa 11 wa Makatibu wakuu wa vyama vya ukombozi wa Kusini mwa Afrika kwamba leo ni maadhimisho ya mwaka wa tatu tangu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan aliposhika madaraka ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania miaka mitatu iliyopita" -Dkt. Nchimbi

“Kwa kweli ninajivunia sana Rais Samia Suluhu Hassan si kwa sababu tu mimi ni mpigania haki za wanawake, bali kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa uongozi mzuri anavyoendelea kuiongoza nchi yetu ya Tanzania, kutokana na hilo CCM inajivunia sana uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, na wananchi wote wa Tanzania kwa ujumla wetu tunajivunia sana kuongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa uwezo wake mkubwa ambao ameuonesha ndani ya hii miaka mitatu." -Balozi Dkt. Nchimbi

Dkt. Nchimbi pia ametumia nafasi hiyo kuwahakikishia wajumbe kuwa kutokana na kuwa mwanamajumui wa kweli wa Afrika Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ana dhamira ya dhati kuimarisha na kuboresha uhusiano wa nchi na vyama rafiki katika ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika na kwamba anafuatilia mkutano huo wa 11 wa Makatibu wakuu wa vyama hivyo kwa ukaribu, huku pia akiwaomba wajumbe kuungana nae kumtakia kila la heri na kumuunga mkono, ombi ambalo lilipokelewa na kukubaliwa na wajumbe.

Chanzo: Jambo Tv

================================
For English Audience

Ambassador Dr. Emmanuel John Nchimbi, the Secretary-General of CCM, expressed immense pride in President Samia Suluhu Hassan's exceptional leadership over the past three years. He highlighted her dedication to advancing Tanzania's development, improving societal welfare, and fortifying national foundations.

Dr. Nchimbi underscored CCM's unwavering support for President Samia Suluhu Hassan's leadership and her commitment to fostering stronger ties with neighboring Southern African countries, as evident during the 11th Meeting of Secretaries General of Liberation Parties.

Addressing delegates in English at the event in Victoria Falls, Zimbabwe on March 19, 2024, Dr. Nchimbi reiterated CCM's endorsement of President Samia Suluhu Hassan's leadership and her steadfast implementation of the party's 2020-2025 election manifesto. He emphasized CCM's full backing of her administration and noted the significance of her third anniversary as President of Tanzania.
 
Sababu kubwa inayombeba Mama yetu Malkia wa Mazingira Africa

Ni kuwa Msikivu, Mwadilifu, Mpenda maendeleo na Ndiye kiongozi mwenye nia ya dhati ya kuhakikisha taifa letu linakuwa na Usawa kwa watu wooote.

Huyu ndiye Dr Samia Suluhu Hassan, kiongozi pekee anayejali na Kuthamini Jamii kwa kujitoa.

Hongera kubwa MHE RAIS WETU.
 
hilo ni kweli kabisaa,
liko bayana kabisa kwamba katika kila kona na viunga vya Tanzania bara na visiwani mama Rais comrade Dr SSH anapendwa na anakubalika sana 🐒
 
Back
Top Bottom