ROBERT MICHAEL
JF-Expert Member
- Oct 23, 2012
- 5,056
- 2,850
Hamna kitu yule mama, Maalim hakuongelea viti maalum aliongelea majembe yaliyochaguliwa na wananchi.
Ivi kuna mtu kweli anaweza kufungua TV kumsikiliza huyu mama? angekuwa na thamani angesimama kuitetea Zanzibar yake iliyomezwa ni Tanganyika miaka nenda miaka rudi, badala kujenga hoja anasema yeye anaunga mkono tu maoni ya wengi
Kwa maana hii ina maana hapatakuwa tena na uchaguzi wa Kiongozi wa Zanzibar bali mgombea Urais atakuwa na mwenza wake ambaye kama watashinda basi mwenza atakuwa moja kwa moja kiogozi wa serikali ya upande wa pili.Ilitokana na sababu za mfumo wa vyama vingi ambavyo vilileta mkanganyiko ufuatao:
1. Inaweza kutokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka chama kimoja na Rais wa Zanzibar chama kingine
2.Ikitokea Rais wa Jamhuri ameugua , kufariki au kufukuzwa kazi, Rais wa Zanzibar ataongozaje nchi nzima wakati amechaguliwa na watu wa Zanzibar tu?
MH. Hatib amenukuu viongozi mbalimbali wa CUF akiwemo SEIF SHARIF HAMAD waliposema kuwa kuondolewa kwa Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa Jamnhuri ni pigo kwa Zanzibar na kusema sasa nafasi hiyo imerudishwa na rasimu inayojadiliwa na Wapinzani watafute kisingizio kingine.
Mjumbe wa bunge la katiba,John Chilighati amesema kufufua Tanganyika ni sawa na kufufua maiti iliyokufa miaka 50 iliyopita.Chilighati alienda mbali zaidi kwa kusema kazi ya kufufua maiti aliiweza Yesu tu.
MY TAKE:
Hivi nikisema huyu mtu karopoka nitakuwa nakosea?Hivi huu si ushahidi wa kuwa na viongozi wabovu na wasiothamini hata historia ya nchi yetu.
Nahakika kwa kauli hii ya Chilighati hata wazanzibari wanatudharau tena sana.
Mods naomba msiunganishe huu uzi ili watanzania wampime mtu huyu.
Ivi kuna mtu kweli anaweza kufungua TV kumsikiliza huyu mama? angekuwa na thamani angesimama kuitetea Zanzibar yake iliyomezwa ni Tanganyika miaka nenda miaka rudi, badala kujenga hoja anasema yeye anaunga mkono tu maoni ya wengi
Kama ambavyo wewe huna tofauti na mafisadi.Mi naona CCM ,UKAWA wote walewale tu
Wanajali matumbo yao na ubinafsi
Wametumia Bil 21 na sasa mchakato wameuharibu makusudi
wanataka ili baadae wale pesa zetu tena
Wale wa dodoma nao wamekuwa wabishi kisa laki tatu kwa siku.
Wanatakiwa watumie tu common sense
Wanafanya hivyo vikao kwa manufaa yapi sasa.
Watu tunakatwa mamilioni ya PAYE alafu wao wanazitumia bureee tu
Jana Kepteni John Chiligati amedai Tanganyika ni maiti, Tanganyika ilishakufa hivyo Tanganyika haipo. Sasa najiuliza Nchi yetu ni maiti??
Kwa hiyo sisi ni mizimu? Yani Zanzibar imejiunga na maiti? So Jamhuri ya Muungano ndio mochwari? Afu Kumbe tunaposherehekea uhuru wa
Tanganyika tunasherehekea marehemu?
Akaongezea eti tukitaka Tanganyika ifufuke tumsubiri Yesu arudi maana yeye ndiye mwenye miujiza ya kufufua wafu? Viongozi wa aina hii wanatupeleka wapi?.