Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,498
- 113,604
Wanabodi,
Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa huja na makala zangu elimishi za Kwa Maslahi ya Taifa, ambazo zinachapishwa kwenye gazeti la Nipashe kila siku za Jumapili.
Leo naendelea na sehemu nyingine ya Ijue Katiba ya JMT kwa jicho la mtunga katiba. Sehemu ya kwanza nilifundisha katiba ni nini na katiba ni ya nani Ijue Katiba ya JMT Kwa Jicho la Mtunga Katiba: Watanzania Tusishabikie Uhaini!. Hukuna Uhaini wa Kauli na Maneno, Uhaini ni Mipango na Matendo!.
Sehemu ya pili nikazungumzia Mtunga katiba alimaanisha nini aliposema Katiba ni Sheria Mama Ijue Katiba kwa Jicho la Mtunga Katiba: Mtunga Katiba alimaanisha nini aliposema "Katiba ni Sheria Mama"? Ni kweli Katiba ni Sheria Mama? leo nazungumzia jinsi Bunge letu Tukufu, linavyotunga sheria batili zinakwenda kinyume cha katiba na nyingine sio tuu Bunge letu limetunga sheria batili, bali ubatili huo ukachomekewa (kiubatili) mpaka ndani ya katiba yetu ya JMT ya mwaka 1977 ndio maana hitaji la katiba mpya ni hitaji very bonafide genuine kwa Watanzania kuweza kusonga mbele kimaendeleo kwa kuwapata viongozi able people wenye uwezo, ability, capacity and capability ya kututoa hapa tulipo na kutufikisha kule tulipaswa kuwepo kama Singapore, Taiwan, Malaysia, Indonesia, ambazo tulipata nazo uhuru wakati mmoja, sisi tukiwa with everything wao wakiwa with nothing!, lakini angalia leo wenzetu walipo compared na sisi tulipo!, the magic is, the right people and the right strategies, hatua ya kwanza is to get the right people!.
Bandiko hili ni la swali
Sii wengi wanafahamu Bunge letu Tukufu linaporidhia mkataba wowote wa kimataifa, mfano ile IGA ya ajabu ajabu ya DPW, maana yake hicho kilichoridhiwa kwenye huo mkataba ulioridhiwa na Bunge, kinakuwa ni sehemu ya sheria zetu za ndani, under local laws!. Ina maana Bunge ni linatunga sheria zetu za ndani kupitia miswada ya sheria inayoletwa bungeni na kupitishwa kuwa sheria, na Bunge linaporidhia mikataba ya kimataifa, maana yake ni Tanzania tume imports sheria hizo za nje na kuzi domesticate kuwa ni sheria za ndani, hivyo hivi tunapozungumza ile IGA ya DPW na Bandari zetu ni sheria yetu halali!.
Kwa mujibu wa sheria yetu ya Rasilimali za Taifa, ile IGA ya DPW na Bandari zetu ni batili!, lakini kwa mujibu wa katiba yetu, mamlaka pekee ya kutangaza ubatili wa katiba au sheria yoyote ni Mahakama Kuu ya JMT. Mahakama Kuu imeibariki IGA ile licha ya mapungufu yote ya kisheria ya ile IGA.
Kuna upungufu mmoja mkubwa ambao hakutajwa sana, huu ni upungufu wa illegality. IGA ile ya DPW na Bandari zetu, ina illegalities mbili.
Ya kwanza ni illegality ya the capacity of Dubai to contract an international Treaty, kwasababu Dubai sio nchi, haina sovereignty hivyo haina the capacity to enter into an international Treaty with a nation kama Tanzania, mwenye uwezo huo ni UAE tuu na hakukuwa na POA (power of attorney) kutoka UAE kuiwezesha Dubai kuingia an international Treaty!.
Illegality ya pili, mkataba ule una kipengele kilicho kinyume cha sheria zetu, hivyo it's an illegal contract, lakini Bunge letu Tukufu limeipitisha hivyo hivyo.
Hii sii mara ya kwanza kwa Bunge letu kutufanyia mambo ya ajabu kama haya!.
Leo naomba niwaletee mifano Bunge letu Tukufu kutunga sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba ya JMT. Kwa kuonyesha Katiba inasema nini, hiyo sheria batili ikasema nini, na mwisho kuonyesha sheria batili hiyo, imekinzana wapi na katiba ya JMT.
Kama wewe sio mpenzi wa kusoma mambo marefu na huna interest na kujua vifungu vya katiba na sheria, unaweza ku skip sehemu hii, ukaibukia kule kwa Mchungaji Mtikila
Kwa vile mimi ni Mtanzania na nawafahamu vizuri Watanzania walio wengi hawako deep kusoma makitu marefu, hivyo kwa wale wa short and clear mnaweza kuishia hapa and jump kwenye A way forward na conclusions, wale wa deep tuendeleeni
Katika kesi hiyo, Mchungaji Mtikila aliomba mambo mawili makuu
Kama nilivyowahi kushauri humu, ukosoaji wenye kujenga, huandamana na ushauri wa nini kifanyike kurekebisha kasoro hizi ili kuundoa ujinga huu unaoendelea nchini mwetu kwa sasa kwa viongozi wa umma kuhama vyama na kupoteza uongozi wa umma.
Mambo ya ajabu kulihusu Bunge letu ni mengi nineisha wahi kuyaulizia humu na miongoni mwake ni haya,
Tanzania tumebarikiwa kumpata rais mpenda haki na mtenda haki, ni tumuombe tuu kutumia mamlaka yake as an executive president kubadili katiba na sheria ya uchaguzi kwa kutumia hati ya dharura, kwa jinsi ile ile ubatili huo ulivyochomekewa ndani ya katiba yetu, na afanye mabadiliko ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC kuifanya kuwa ni tume huru na Shirikishi na kuiwezesha NEC wasimamie chaguzi zote toka uchaguzi wa serikali za mitaa mpaka Uchaguzi Mkuu kwa kuajiri wasimamizi wa uchaguzi na sio huu mtindo wa sasa wa kuwatumia makada wa chama kimoja waliolamba uteuzi.
Mungu Ibariki Tanzania
Paskall
Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa huja na makala zangu elimishi za Kwa Maslahi ya Taifa, ambazo zinachapishwa kwenye gazeti la Nipashe kila siku za Jumapili.
Leo naendelea na sehemu nyingine ya Ijue Katiba ya JMT kwa jicho la mtunga katiba. Sehemu ya kwanza nilifundisha katiba ni nini na katiba ni ya nani Ijue Katiba ya JMT Kwa Jicho la Mtunga Katiba: Watanzania Tusishabikie Uhaini!. Hukuna Uhaini wa Kauli na Maneno, Uhaini ni Mipango na Matendo!.
Sehemu ya pili nikazungumzia Mtunga katiba alimaanisha nini aliposema Katiba ni Sheria Mama Ijue Katiba kwa Jicho la Mtunga Katiba: Mtunga Katiba alimaanisha nini aliposema "Katiba ni Sheria Mama"? Ni kweli Katiba ni Sheria Mama? leo nazungumzia jinsi Bunge letu Tukufu, linavyotunga sheria batili zinakwenda kinyume cha katiba na nyingine sio tuu Bunge letu limetunga sheria batili, bali ubatili huo ukachomekewa (kiubatili) mpaka ndani ya katiba yetu ya JMT ya mwaka 1977 ndio maana hitaji la katiba mpya ni hitaji very bonafide genuine kwa Watanzania kuweza kusonga mbele kimaendeleo kwa kuwapata viongozi able people wenye uwezo, ability, capacity and capability ya kututoa hapa tulipo na kutufikisha kule tulipaswa kuwepo kama Singapore, Taiwan, Malaysia, Indonesia, ambazo tulipata nazo uhuru wakati mmoja, sisi tukiwa with everything wao wakiwa with nothing!, lakini angalia leo wenzetu walipo compared na sisi tulipo!, the magic is, the right people and the right strategies, hatua ya kwanza is to get the right people!.
Bandiko hili ni la swali
Watanzania tutaendelea kusubiria mpaka lini wakati Bunge letu Tukufu likitunga Sheria batili na sometimes kuuchomekea ubatili huo hadi ndani ya Katiba yetu na kuifanya katiba yetu kuwa na vipengele batili?. Je Watanzania tufanye nini?, au tunaweza kulifanya nini Bunge la aina hii?.
Sii wengi wanafahamu Bunge letu Tukufu linaporidhia mkataba wowote wa kimataifa, mfano ile IGA ya ajabu ajabu ya DPW, maana yake hicho kilichoridhiwa kwenye huo mkataba ulioridhiwa na Bunge, kinakuwa ni sehemu ya sheria zetu za ndani, under local laws!. Ina maana Bunge ni linatunga sheria zetu za ndani kupitia miswada ya sheria inayoletwa bungeni na kupitishwa kuwa sheria, na Bunge linaporidhia mikataba ya kimataifa, maana yake ni Tanzania tume imports sheria hizo za nje na kuzi domesticate kuwa ni sheria za ndani, hivyo hivi tunapozungumza ile IGA ya DPW na Bandari zetu ni sheria yetu halali!.
Kwa mujibu wa sheria yetu ya Rasilimali za Taifa, ile IGA ya DPW na Bandari zetu ni batili!, lakini kwa mujibu wa katiba yetu, mamlaka pekee ya kutangaza ubatili wa katiba au sheria yoyote ni Mahakama Kuu ya JMT. Mahakama Kuu imeibariki IGA ile licha ya mapungufu yote ya kisheria ya ile IGA.
Kuna upungufu mmoja mkubwa ambao hakutajwa sana, huu ni upungufu wa illegality. IGA ile ya DPW na Bandari zetu, ina illegalities mbili.
Ya kwanza ni illegality ya the capacity of Dubai to contract an international Treaty, kwasababu Dubai sio nchi, haina sovereignty hivyo haina the capacity to enter into an international Treaty with a nation kama Tanzania, mwenye uwezo huo ni UAE tuu na hakukuwa na POA (power of attorney) kutoka UAE kuiwezesha Dubai kuingia an international Treaty!.
Illegality ya pili, mkataba ule una kipengele kilicho kinyume cha sheria zetu, hivyo it's an illegal contract, lakini Bunge letu Tukufu limeipitisha hivyo hivyo.
Hii sii mara ya kwanza kwa Bunge letu kutufanyia mambo ya ajabu kama haya!.
Leo naomba niwaletee mifano Bunge letu Tukufu kutunga sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba ya JMT. Kwa kuonyesha Katiba inasema nini, hiyo sheria batili ikasema nini, na mwisho kuonyesha sheria batili hiyo, imekinzana wapi na katiba ya JMT.
Kama wewe sio mpenzi wa kusoma mambo marefu na huna interest na kujua vifungu vya katiba na sheria, unaweza ku skip sehemu hii, ukaibukia kule kwa Mchungaji Mtikila
Mchungaji Mtikila, licha ya kuwa ni mwanasiasa, Mwenyekiti wa chama cha siasa cha DP, (Democratic Party), lakini alikuwa ni mtu wa Mungu kiukweli kabisa, kwa sababu hakukubali kabisa katiba yetu inajisiwe!, hivyo akafungua kesi nyingine No. 10 ya mwaka 2009 kupinga marekebisho hayo ya 8 ya katiba na kuyaita ni ubatili!.
- Tuanze na Ibara ya 5 ya katiba ya JMT inasema
Haki hii ndio haki kuu ya kwanza ya kidemokrasia, haki ya kupiga kura, japo haki hii bado ipo kwenye katiba yetu, haki hii imeingiliwa na kukiukwa na ukosekanaji wa haki ya kuchaguliwa, hivyo Watanzania kuruhusiwa kuwachagua sio viongozi wao wanaowapenda kwa uhuru, bali Watanzania wanalazimika kuwachagua viongozi waliopitishwa na wahuni fulani (kudhaminiwa na chama cha siasa), hivyo ni kukiuka nia njema ya mtunga katiba ya kila Mtanzania anakuwa na haki ya kupiga kura kuchagua kiongozi anamtaka kwa Tanzania ni kumchagua kiongozi chama kilicho wachagulia!.
2. Ibara ya 5 (2) inalipa Bunge mamlaka ya kutunga sheria kuzuia mtu kupiga kura
Haki hii ya uhuru wa kupiga kura kuchagua ni moja ya haki zinazoitwa fundamental rights, yaani haki za msingi za binadamu.
3. Ibara ya 3 imelipa Bunge la JMT, mamlaka ya kutunga sheria ya uchaguzi
Mamlaka haya ya Bunge kutunga sheria ya uchaguzi pia limewekewa masharti, hivyo Bunge halina mamlaka ya kutunga sheria inayokwenda kinyume cha katiba.
Kisha tuje ibara ya 21 ya katiba ya JMT
Tuje ibara ya 39 ya katiba ya JMT.
Tumalizie Ibara ya 67 ya Katiba ya JMT
Baada ya kukuwekea vifungu, sasa twende taratibu nikuchambulie
Ibara ya 5 ni haki ya kupiga kura kwa kila Mtanzania aliyetimiza umri wa miaka 18. Ili haki hii iwe na maana, Mtanzania huyu anapaswa kuwa huru kumchagua kiongozi yoyote anayemtaka. Lakini kwa Tanzania haki hii inabaguliwa, Watanzania wanalazimishwa kuwachagua wanachama tuu wa vyama vya siasa ambayo ni kinyume cha Ibara ya 11!.
Ibara hii ya 21 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inatoa haki ya kila Mtanzania mwenye sifa, kuwa huru kushiriki katika siasa na uongozi kuanzia serikali za mtaa hadi serikali kuu, bila ubaguzi wowote.
Uhuru wa kushiriki shughuli za umma
21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.
Lakini kukafanyika uhuni fulani kwa maslahi ya watu fulani na chama fulani kwa vile serikali ni yao, wakaipindua katiba kwa kuinyofoa haki hiyo ya kila mtu kushiriki siasa, iliyotolewa na katiba, na kupachika shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa hivyo kujenga ubaguzi katika kushiriki shughuli za uongozi wa umma kwa watu kulazimishwa kwanza kujiunga na vyama vya siasa, ndipo upate haki ya kugombee nafasi yoyote ya uongozi wa umma, huku sio kuwatendea haki Watanzania wengine wote, wasiotaka kujiunga na vyama vyovyote vya siasa, kutokana na kuviona karibu vyama vyote ni vyama vya hovyo hovyo, isipokuwa chama kimoja, lakini kuna watu wazuri na wana uwezo mkubwa wa uongozi, hawawezi kugombea uongozi kwasababu ya ujinga huo!. Shurti hili la kudhaminiwa na chama cha siasa ni kinyume cha Ibara ya 11 ya katiba ya JMT ya mwaka 1977!.
Hii ni haki muhimu iliyotolewa na katiba, kitendo cha kuingiza shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa ni kinyume cha katiba. Hivyo sheria hii ibadilishwe ili kukidhi kile ambacho mtunga katiba ilidhamiria ilipoiweka haki hii, ndani ya katiba yetu!, hivyo baada ya mabadiliko hayo ya mlango wa nyuma, kipengele hicho sasa kinasomeka hivi
Uhuru wa kushiriki shughuli za umma Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 Sheria ya 1994 Na.34 ya ib.4
21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.
Ule uhuru uliotolewa na Katiba wa kila mtu kuwa huru kushiriki shughuli za uongozi, kupitia ibara ya 21, umekuja kunyofolewa na ibara ya 39 na 67 (b)(c) kwa kuweka sherti, ili mtu kuweza kugombea nafasi yoyote ya uongozi wa umma, ni lazima awe ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa hivyo lazima adhaminiwe na chama cha siasa!, Haki zinatolewa na ibara moja halafu zinaporwa na ibara nyingine ya katiba hiyo hiyo!.
Mchungaji Mtikila (Mungu amuweke mahala pema peponi), mwaka 1993, alifungua kesi No. 5 ya 1993, alifanya juhudi kubwa kukipinga kifungu hiki na Mahakama Kuu kupitia kwa Jaji Lugakingira, (Mungu amuweke mahala pema peponi), ikatamka wazi na bayana kipengele hicho ni batili na kinakiuka katiba ya JMT ya mwaka 1977, hivyo kifutwe, na kutoa haki kwa kila Mtanzania ana haki ya kushiriki kugombea Uongozi wowote wa nchi.
Baada tuu ya Mtikila kushinda kesi serikali ikafanya mambo mawili makubwa ya ajabu!, kwanza ilikata rufaa!. Hivi kwa uamuzi kama huu, serikali ilikata rufaa kwa maslahi ya nani?. Wiki iliyopita nilisema ile Ibara ya 64(5) iayotamka Katiba ni sheria Mama, sheria nyingine yoyote inayokwenda kinyume cha katiba ni batili, aliyebatilisha sheria batili ni katiba yenyewe na sio Mahakama!. Kazi ya Mahakama ni kutamka tuu huo ubatili na tangu baada ya tamko hilo, sheria hiyo inakuwa tayari ni imebatika!, unawezaje kukata rufaa kwa kitu kilicho batilishwa na katiba?. Kiukweli kabisa hili ni jambo la ajabu sana!.
Jambo la pili la ajabu sana na kubwa ya mwaka ni serikali yetu ilipeleka bungeni kwa hati ya dharura, sheria No. 34 ya mwaka 1994, kufanya marekebisho ya 8 ya Katiba ya JMT na kukichomeka kipengele hicho ndani ya katiba, hivyo kuibatilisha ile hukumu ya Jaji Lugakingira!. Hapa ndipo ujinga unapoanzia katika siasa zetu kwa serikali kufanya kazi kwa maslahi ya kisiasa ya watu fulani na chama fulani, hivyo kupoteza haki ya wengi kwa ajili ya kuwanufaisha wachache!..
Hiki kilichofanyika, mimi nakiita ni kitendo cha kihuni!, Watanzania tulifanyiwa uhuni na serikali yetu, kwa kuinajisi katiba yetu!, kitu kimeelezwa ni kinyume cha katiba, kinatoa haki zilizotolewa na katiba, halafu serikali hiyo inakuja kuihalalisha haramu hiyo kwa kuiingiza rasmi kwenye katiba!, huku sii kuinajisi katiba yetu?. Uhuni huu ulifanywa na awamu zilizopita, lakini kitu cha ajabu ni serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia, inataka kuurudia uhuni huu!, nimeshauri kwa vile ni sio kosa la awamu ya Rais Samia, hivyo kosa lililofanyika sio kosa kwasababu watendaji waliofanya hayo hawakujua kuwa ni makosa, kutenda kosa bila kujua ni kosa, sii kosa, kosa ni kurudia kosa Kufanya Kosa, Si Kosa, Kosa Kurudia Kosa!. Sheria ya Uchaguzi ni Kosa!, Kwanini Tunarudia Kosa?!. Haki Sii Hisani ni Stahiki!. Bunge Tutendeeni Haki!
Kwa vile mimi ni Mtanzania na nawafahamu vizuri Watanzania walio wengi hawako deep kusoma makitu marefu, hivyo kwa wale wa short and clear mnaweza kuishia hapa and jump kwenye A way forward na conclusions, wale wa deep tuendeleeni
Katika kesi hiyo, Mchungaji Mtikila aliomba mambo mawili makuu
Nini Kifanyike, A Way Forward.mambo hayo ni
(a) Mahakama itamke ibara 39 na 67 za katiba zilizorekebishwa na marekebisho ya 8 kwa sharia No. 34 ya mwaka 1994, ni batili na kinyume cha katiba.
(b) Kutamka wazi kuwa Kila Mtanzania ana haki ya kugombea kwa mujibu wa ibara ya 21 ya Katiba, bila kulazimishwa kudhaminiwa na chama cha siasa, hivyo mtu anaweza kugombea kama mgombea binafsi.
Mahakama Kuu chini ya majaji watatu, (majaji watatu kisheria inaitwa Half Bench), Manento, Masati na Mihayo, wakayakubali mambo yote ya Mchungaji Mtikila na kumpa ushindi tena kwa kutamka marekebisho hayo ya katiba ni batili!. Lakini serikali yetu ilivyo ya ajabu, ikakata tena rufaa, na safari hii Mahakama Kuu ikakaa Full Bench ya majaji 7, chini ya Jaji Mkuu Mwenyewe, Agustino Ramadhani, akisaidiwa na Jaji Eusebio Munuo, Jaji January Msoffe, Jaji Natalia Kimaro, Jaji Kassim Mbarouk, Jaji Benard Luanda, na Jaji Sauda Mjasir, ambapo tarehe 17 mwezi June, mwaka 2010 ikatoa hukumu ya ajabu kabisa kuwa kutokea Tanzania!.
Tena Mahakama ya rufaa haikuwa peke yake, bali iliwaita mabinga wabobezi na wabobevu wa sheria na katiba kuisaidia, hawa wanaitwa marafiki wa mahakama, kwa kiingereza ni friends of the Court, kisheria wanaitwa Amicus Curiae, hivyo ma Amicus Curiae hawa, Mr. Othman Masoud, Prof. Palamagamba Kabudi, na Prof.Jwan Mwaikusa(Mungu Aiweke Roho yake Mahala Pema Peponi).
Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Rufaa uliamua kitu cha ajabu sana na hapa naomba kunukuu
“So as to let the will of the people prevail as to whether or not such [independent] candidates are suitable. We are definite that the Courts are not the custodian of the will of the people. That is the property of elected Members of Parliament”.
Hii kiukweli ni kauli ya ajabu sana kutolewa na mahakama yetu kwenye jambo zito na muhimu kama hili!. Kitendo cha Mahakama kujivua jukumu la kuwa the custodian of the will of the people!, ni kitendo cha ajabu sana na kushangaza sana!. Hakuna will of the people kubwa kuliko katiba!, kama katiba imetoa haki fulani, halafu Bunge likatunga sheria ya ajabu kabisa kuifuta haki hiyo, halafu mahakama ikatamka haiwezi kuliingilia Bunge!, where is the doctrine of separation of powers, checks and balance?!.
Kwa ajili ya kulinda heshima ya Mahakama Kuu, naomba niweke ilichokisema bila kukitafsiri.
“In our case, we say that the issue of independent candidates has to be settled by Parliament which has the jurisdiction to amend the Constitution and not the Courts which, as we have found, do not have that jurisdiction. The decision on whether or not to introduce independent candidates depends on the social needs of each State based on its historical reality. Thus the issue of independent candidates is political and not legal However, we give a word of advice to both the Attorney General and our Parliament: The United Nations Human Rights Committee, in paragraph 21 of its General Comment No. 25, of July 12, 1996, said as follows on Article 25 of the International Covenant on Civil and Political Rights, very similarly worded as Art 23 of the American Convention and our Art 21: The right of persons to stand for election should not be limited unreasonably by requiring candidates to be members of
parties or of specific parties. Tanzania is known for our good record on human rights and particularly our militancy for the right to self determination and hence our involvement in the liberation struggle. We should seriously ponder that comment from a Committee of the United Nations, that is, the whole world.
DATED at DAR ES SALAAM this 17th day of June, 2010”
Mahakama ya Rufaa ikaamua kuwa Mahakama haina mamlaka ya kuliingilia Bunge, katika vipengele vya katiba, kumaanisha kwa vile marekebisho hayo ya 8 yamefanywa na Bunge, hivyo ni Bunge ndio lirekebishe kipengele hicho!, kiukweli kabisa, kwa maoni yangu, uamuzi huu sio utii wa mhimili wa Mahakama kwa mhimili Bunge, bali huu ni ukondoo wa hali ya juu kwa Mhimili wa Mahakama kwa serikali kwa manufaa ya watu wachache!.
Uchaguzi wa Mwaka 2015 ukalithibitisha hili, kumbe baadhi ya majaji wetu ni makada!, Jaji Mkuu Mstaafu aliyeongoza jopo hilo, alichukua fomu kugombea urais!, for what my God?!. Baadhi ya wale ma amicus curiae naamini tunawajua na tunawaona na ukada wao!. Unategemea nini kama sheria za nchi hii zitafinyangwa finyangwa kwa manufaa ya wachache?!. President Samia must stop this nonsense!.
Japo Lengo la Kudhaminiwa na Chama ni zuri, ila Huu Sii Ujinga Tuu?!.
Katiba ilisema kila Mtanzania ana haki ya kushiriki uongozi, hili sherti la kudhaminiwa na chama lilitoka wapi? na kwa kwa nini watu walazimishwe kuwa wanachama wa vyama ili wadhaminiwe, ndipo waweze kugombea?. Mfano mimi, sina chama kwa sababu naziona siasa za vyama ni za hovyo hovyo, ikitokea nina uwezo wa kuwatumikia wananchi wa eneo langu na kuwaletea maendeleo bila kupitia chama chochote, kwa nini nizuiliwe?!. Kiukweli kabisa, kwa maoni yangu, huu ni ujinga uliopitiliza!, tutaliacha Bunge letu Tukufu kutufanyia ujinga huu mpaka lini?, is this not nonsense?.
Watanzania tusikubali ujinga huu uendelee hadi 2025!, tupiganie milango ya wagombea binafsi ifunguliwe kabla ya, 2025, ili watu wenye nia ya kugombea, na wana uwezo wa kuwaletea wananchi maendeleo, bila kupitia hizi nonsense za vyama waingie, washindane kwa hoja na sio kushindana kuhonga, kama hali inavyoendelea sasa!. Hili shurti la vyama lingekuwa limendolewa, mngeweza kushangaa watu wazalendo wa kweli wa nchi hii, kama kina Reginald Mengi, Ali Mfuruki, Yogesh Manek, SS Bakhresa, Pascal Mayalla, and the like, wenye uchungu wa dhati na umasikini wa taifa hili, wangejitokeza kugombea kuwatumikia wananchi!.
Kiongozi Akiishachaguliwa, Anakuwa ni Kiongozi wa Watu, na Sio Kiongozi wa Chama, Kwa Sababu Anachaguliwa na Watu na Sio Chama!.
Kiukweli kwenye hili jambo, kuna ujinga mwingi!, ujinga mwingine mkubwa kabisa ni huu, hata kama mgombea amedhaminiwa na chama cha siasa kugombea, akiishapitishwa na Tume ya Uchaguzi kuwa Mgombea, japo anatambulika kama ni mgombea wa chama fulani, lakini akiishachaguliwa, mwenyekiti wa mtaa, diwani, mbunge au rais, anakuwa sio kiongozi tena wa chama kilichomdhamini, bali sasa anakuwa ni kiongozi wa umma, kiongozi wa wananchi. Mfano baada ya rais Magufuli kuchaguliwa kuwa rais kwa tiketi ya CCM, lakini hakuchaguliwa na wana CCM pekee, amechaguliwa na Watanzania wote, yeye anakuwa sio kiongozi wa CCM bali kiongozi wa Watanzania wote, vivyo hivyo kwa wabunge, madiwani na viongozi wa serikali ya mtaa, kitendo cha mtu ambaye ni kiungozi wa umma, kujitoa chama na kupoteza ubunge, udiwani au uongozi wa umma, ni ujinga ambao haupaswi kuvumiliwa. Nini muhimu kati ya umma na chama?. Kuukosesha umma kiongozi wao waliemchagua kwa sababu za chama, sio tuu sio haki kwa wananchi waliomchagua, bali pia ni dhambi, kuwalipisha masikini hawa gharama za uchaguzi wa marudio kwa sababu za kijinga!.
Kama nilivyowahi kushauri humu, ukosoaji wenye kujenga, huandamana na ushauri wa nini kifanyike kurekebisha kasoro hizi ili kuundoa ujinga huu unaoendelea nchini mwetu kwa sasa kwa viongozi wa umma kuhama vyama na kupoteza uongozi wa umma.
- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amirati Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan asiruhusu ule ujinga wa kuhama vyama unaosababisha hasara kwa taifa, kwa kuwashukuru kumuunga mkono na kuunga mkono juhudi zake, lakini wabaki huko huko kwenye vyama vyao, hadi 2025, wakiishamaliza muhula wao, ndipo wajitoe na kuhama vyama!.
- Ikulu ni mahali patakatifu, Rais wa Nchi, akiwa Ikulu yetu, atenganisha kofia zake mbili za rais wa nchi na Mwenyekiti wa chama cha CCM, rais wetu akiwa Ikulu yetu afanye kazi takatifu, asiendeshee vikao vya CCM, pale patakatifu petu, vikao vya CCM akavifanyie ofisi ya CCM Lumumba au kumbi za CCM Dodoma. Japo hakuna kosa lolote kuendeshea vikao vya CCM Ikulu yetu, lakini halileti picha nzuri kwa rais wetu, ambaye ni mpenda haki, kwa sababu yeye sio rais wa CCM ni rais wa Watanzania wote!.
- Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kufuta chaguzi zote ndogo, na tuanzishe utaratibu wa proportional representation kwa mwenye kura nyingi ndiye mshindi, lakini likitokea lolote, akasita kuwa rais, kwa rais tunaye VP, kwa mbunge au diwani, yule aliyemfuatia kwa kura katika uchaguzi uliopita ndio anatangazwa mbunge, kama alipata zaidi ya 10% ya kura zote, kama hayupo aliyefikia asilimia hizo, ndipo uchaguzi mdogo unafanyika.
- Kile kipengele cha kudhaminiwa na chama kiishie kwenye uteuzi tuu, kiongozi akiishachaguliwa, anakuwa kiongozi wa watu, anaweza kuhama chama bila kupoteza uongozi wake kama ilivyo nchini Kenya na nchi nyingine zenye kuheshimu demokrasia ya kweli na sio hii demokrasia fake ya vyama!.
- Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kuondoa kipengele cha kudhaminiwa na vyama ili kila Mtanzania mwenye sifa za kugombea uongozi wa nafasi yoyote, aruhusiwe, ila kwenye urais, tuweke vigezo vya ziada, ili asijetokea tajiri mmoja mwenye ukwasi wa kuwanunua watanzania wote, tukajikuta tuna rais wa kununuliwa. Ila kwenye ubunge, udiwani na serikali za mtaa, kila mtu awe free kugombea, hivyo tuwe na wagombea huru, na hili likifanyika hata sisi tusio na vyama tutashiriki, mfano mimi, naweza kabisa kugombea jimbo fulani na kulitwaa kama kuokota embe dodo lililojiangukia, ambapo mbunge wa hapo, nitamsukuma kama nimesukuma mlevi!.
- Tuibadili Tume yetu ya Uchaguzi iwe Tume Huru zaidi na Shirikishi, tujenge uwanja sawa wa ushindani wa haki kwa vyama vyote, uchaguzi uendeshwe kwa transparency ya hali ya juu kwa kuruhusu mawakala hadi kwenye tallying, na vyama au taasisi zozote ziwe free kuwa na tallying centers zake, kitu ambacho hakitaruhusiwa na talling centers hizo ni kutangaza matokeo, kama matokeo yote ya uchaguzi hadi wa rais yanahesabiwa kituoni na kubandikwa ukutani, kama hakuna jambo lolote la kificho, yaani nothing to hide, kwanini uzuie independent tallying?!. Uchaguzi wa 2020, kila mwenye uwezo wa kufanya tallying aruhusiwe afanye ila sitangaze matokeo, hii itazuia bao la mkono!.
Mambo ya ajabu kulihusu Bunge letu ni mengi nineisha wahi kuyaulizia humu na miongoni mwake ni haya,
- Wabunge Wetu wa Ajabu!, Wanaachaje Bunge Lijipendekeze Kwa Serikali!, Wanajua Wajibu Wao?. Check 'n' Balance Itoke Wapi?
- Sehemu ya Pili: Je, Bunge letu tukufu linajipendekeza kwa Serikali?
- Bunge jipya lina hali mbaya! Serikali itafanaje kuliokoa Bunge ili kuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni?
- Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?
- Wajua japo Rais ni sehemu ya Bunge, bado hana mamlaka ya kuliingilia Bunge? Ili kufuta IGA ya DPW, Rais anapaswa kulivunja Bunge?
- Bunge letu ni Bunge la ovyo? Bunge linafanya Uhuni? Wabunge Wetu ni Wahuni? Tumshauri Spika naye aanze kuita Watu kwenye Kamati, au waachwe tu?
- Baadhi ya Wabunge ni Stupid!, Tanzania haina Demokrasia!, Bunge ni Rubber Stamp!- TBC, Watch Now!
- Mbunge kama huyu, ukiwaita baadhi ya wabunge wetu ni vilaza, utakuwa umewakosea?
- Je, Bunge letu ni Bunge Butu?. Angalia Bunge la Uingereza lenye meno linavyong'ata Serikali. Je, Kuna ubaya tukiiga?
Watanzania tutaendelea kusubiria mpaka lini wakati Bunge letu Tukufu likitunga Sheria batili na sometimes kuuchomekea ubatili huo hadi ndani ya Katiba yetu na kuifanya katiba yetu kuwa na vipengele batili?. Je Watanzania tufanye nini?, au tunaweza kulifanya nini Bunge la aina hii?.
Mhimili wa serikali unapotukosea tunaweza kuushitaki mahamani, lakini mhimili wa Bunge na mhimili wa Mahakama, niliwahi kuuliza humu, kiukweli in reality kwa mujibu wa katiba yetu, there is nothing anybody can do zaidi ya kumlilia Mama!.Tanzania tumebarikiwa kumpata rais mpenda haki na mtenda haki, ni tumuombe tuu kutumia mamlaka yake as an executive president kubadili katiba na sheria ya uchaguzi kwa kutumia hati ya dharura, kwa jinsi ile ile ubatili huo ulivyochomekewa ndani ya katiba yetu, na afanye mabadiliko ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC kuifanya kuwa ni tume huru na Shirikishi na kuiwezesha NEC wasimamie chaguzi zote toka uchaguzi wa serikali za mitaa mpaka Uchaguzi Mkuu kwa kuajiri wasimamizi wa uchaguzi na sio huu mtindo wa sasa wa kuwatumia makada wa chama kimoja waliolamba uteuzi.
Mungu Ibariki Tanzania
Paskall