Yaliyojiri bungeni Dodoma: Alhamisi tarehe 11 Septemba, 2014 - Kikao cha 38

Hamna kitu yule mama, Maalim hakuongelea viti maalum aliongelea majembe yaliyochaguliwa na wananchi.
 
Anajua kilichompeleka na lazima atumike kwa uaminifu. Aliteuliwa maalumu kwa kazi hiyo kama huelewi. Kuunga mkono hoja ili kuongeza hesabu ya mashabiki. Hivi ni kweli hujui?

Ivi kuna mtu kweli anaweza kufungua TV kumsikiliza huyu mama? angekuwa na thamani angesimama kuitetea Zanzibar yake iliyomezwa ni Tanganyika miaka nenda miaka rudi, badala kujenga hoja anasema yeye anaunga mkono tu maoni ya wengi
 
Ilitokana na sababu za mfumo wa vyama vingi ambavyo vilileta mkanganyiko ufuatao:
1. Inaweza kutokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka chama kimoja na Rais wa Zanzibar chama kingine
2.Ikitokea Rais wa Jamhuri ameugua , kufariki au kufukuzwa kazi, Rais wa Zanzibar ataongozaje nchi nzima wakati amechaguliwa na watu wa Zanzibar tu?

MH. Hatib amenukuu viongozi mbalimbali wa CUF akiwemo SEIF SHARIF HAMAD waliposema kuwa kuondolewa kwa Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa Jamnhuri ni pigo kwa Zanzibar na kusema sasa nafasi hiyo imerudishwa na rasimu inayojadiliwa na Wapinzani watafute kisingizio kingine.
Kwa maana hii ina maana hapatakuwa tena na uchaguzi wa Kiongozi wa Zanzibar bali mgombea Urais atakuwa na mwenza wake ambaye kama watashinda basi mwenza atakuwa moja kwa moja kiogozi wa serikali ya upande wa pili.

Kwa mfano, Lowassa akishinda uchaguzi mkuu na mwenza wake ni Ali Mwinyi basi moja kwa moja Mwinyi anakuwa rais ama kiongozi wa serikali ya Zanzibar hapatakuwa na uchaguzi wa rais wa Zanzibar, tumerudi kama ilivyokuwa zamani. Hivyo basi hata kama Zanzibar itampa kura nyingi Maalim Seif na CUF kumchagua mgombea ambaye yuko chama kilichoshindwa uchaguzi mkuu watalazimika kuongozwa na makamu (Mwinyi) aloshindwa kwa kura za uchaguzi Zanzibar!
- Does it make sense?
 
Mjumbe wa bunge la katiba,John Chilighati amesema kufufua Tanganyika ni sawa na kufufua maiti iliyokufa miaka 50 iliyopita.Chilighati alienda mbali zaidi kwa kusema kazi ya kufufua maiti aliiweza Yesu tu.

MY TAKE:
Hivi nikisema huyu mtu karopoka nitakuwa nakosea?Hivi huu si ushahidi wa kuwa na viongozi wabovu na wasiothamini hata historia ya nchi yetu.

Nahakika kwa kauli hii ya Chilighati hata wazanzibari wanatudharau tena sana.

Mods naomba msiunganishe huu uzi ili watanzania wampime mtu huyu.

Hujakosea lolote mkuu. Hawa ni walevi tu wa madaraka ya ccm.Wasubiri vijana watakapochukua hatamu za uongozi wa nchi yao uone watakavyoitengeneza hii nchi. Hawa ndio wazee wanaoamini hadi sasa kuwa wanaweza kufikiri kwa niaba ya vijana tena wakidigitali. Ona tu hata michango yao bungeni. Ninachokubali ni alichoeleza mh.Cheo kuwa walichokubaliana kwenye kikao cha maridhiano na raisi hawakukubaliana kusimamisha bunge maalumu la katiba linaloendelea hivi sasa kwani lipo kisheria hadi tarehe 4.oct.Hili bunge linaweza kusimamishwa na mahakamqa ikiwa Saidi Kubenea atashinda kesi tar.15 mwezi huu na sio kwa njia nyingine toyote. Wananchi tunaelewa kinachoendelea kwenye bunge hili hakina maana kwa wananchi zaidi ya hao wajumbe kuendelea kuchota mamilioni yao yatakayowasaidi kwenye kampeni ya chaguzi zijazo.Hiyo kwao ni asante ccm. Wananchi tunaingia kwenye chaguzi na katiba ya zamani iliyofanyiwa marekebisho. Hii ya kwao itasubiri hisani ya raisi ajae.
 
Ivi kuna mtu kweli anaweza kufungua TV kumsikiliza huyu mama? angekuwa na thamani angesimama kuitetea Zanzibar yake iliyomezwa ni Tanganyika miaka nenda miaka rudi, badala kujenga hoja anasema yeye anaunga mkono tu maoni ya wengi

Nimemsikiliza huyu mama hakika kweli Fedha wanayopewa ni bure tu inapotea, katoa pongezi Mwanzo mwisho kuanzia kwa JK,SITTA, SULUHU, KINGUNGE CHEYO, SHEIN, WAJUMBE WANAUME WOTE WALIOSEMA 50 KWA 50, BILA KUWASAHAU BABA WATOTO ZAKE WALIOMSAIDIA KUMUUGUZA
PILI; AKAPINGANA NA MAALIM SEIF AKATAJA ORODHA YA WAJUMBE WALIOMO BMK KUTOKA PEMBA.

MWISHO AKAMALIZIA , HUU NDO MCHANGO WANGU WA KATIBA INAYOPENDEKEZWA. aksante makamu m/kiti
 
daa mtihani hata shekh kundecha tunakuaminia bado unakaza dodoma km mahakama ya kadhi imekataliwa unasubiri nini au tonge
?
 
Mi naona CCM ,UKAWA wote walewale tu
Wanajali matumbo yao na ubinafsi

Wametumia Bil 21 na sasa mchakato wameuharibu makusudi
wanataka ili baadae wale pesa zetu tena
Wale wa dodoma nao wamekuwa wabishi kisa laki tatu kwa siku.
Wanatakiwa watumie tu common sense
Wanafanya hivyo vikao kwa manufaa yapi sasa.
Watu tunakatwa mamilioni ya PAYE alafu wao wanazitumia bureee tu
Kama ambavyo wewe huna tofauti na mafisadi.
 
Hongera sana Mzee Cheyo kwa kuanika ukweli kilichozungumzwa baina yenu na Raisi maana hao UKAWA wameshazoea utaplo
 
Jana Kepteni John Chiligati amedai Tanganyika ni maiti, Tanganyika ilishakufa hivyo Tanganyika haipo. Sasa najiuliza Nchi yetu ni maiti??

Kwa hiyo sisi ni mizimu? Yani Zanzibar imejiunga na maiti? So Jamhuri ya Muungano ndio mochwari? Afu Kumbe tunaposherehekea uhuru wa
Tanganyika tunasherehekea marehemu?

Akaongezea eti tukitaka Tanganyika ifufuke tumsubiri Yesu arudi maana yeye ndiye mwenye miujiza ya kufufua wafu? Viongozi wa aina hii wanatupeleka wapi?.
 
Hawa wapo kwa ajili ya POSHO tu wala usiwasikilize,wakitoka huko wataongea tofauti na walichokisema
 
Huyu kapteni naye anaropoka tu hivi tukimuuliza Tanganyika ilikufaje anazosababu za kutushawishi tukamuelewa?
Naamini Tanganyika haijafa ila ipo imelala! siku ikiamka ndo mtaona wale wote wasiopenda irudi ndo haoa hao wanaotaka uraia pacha na ndo hao hao wanaowapa uraia wahindi na wasomali huku wakiwafukuza Wanyarwanda, warundi na wakongo.


Jana Kepteni John Chiligati amedai Tanganyika ni maiti, Tanganyika ilishakufa hivyo Tanganyika haipo. Sasa najiuliza Nchi yetu ni maiti??

Kwa hiyo sisi ni mizimu? Yani Zanzibar imejiunga na maiti? So Jamhuri ya Muungano ndio mochwari? Afu Kumbe tunaposherehekea uhuru wa
Tanganyika tunasherehekea marehemu?

Akaongezea eti tukitaka Tanganyika ifufuke tumsubiri Yesu arudi maana yeye ndiye mwenye miujiza ya kufufua wafu? Viongozi wa aina hii wanatupeleka wapi?.
 
Mh mtutura amefuta kauli zake zote kali alizotoa katika kudai mahakama ya kadhi,amesema kwamba kwenye bango kitita ameona kwamba taratibu zao na za watu wa mila zitazingatiwa,cc kahtaan MZIMU Ritz,

Sijui amefanyajwe hadi akaomba radhi wakati Maskofu na Wakristo wengine wanajadili kwa jazba ileile kuzuia Mahakama ya Kadhi wakati hata haiwahusu. Pamaja na Hoja nzuri ambazo zinatolewa tena na kimama na shangaa huyu Mheshimiwa amezidiwa mbinu wapi?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom