Yaliyojiri bungeni Dodoma: Alhamisi tarehe 11 Septemba, 2014 - Kikao cha 38

BungelaKatiba2014tz

JF-Expert Member
Feb 18, 2014
1,231
648
Majadiliano ya Taarifa za Kamati za Bunge Maalum la Katiba yanaendelea leo tarehe 11/09/2014.

=====

Akitoa mchango wake kwenye Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa TCD na UDP John Momose Cheyo anasema kuwa mchakato wa bunge unaendelea vema. Alisema kuwa wakati walipozungumza na Rais Kikwete, wajumbe wa TCD walikubaliana kuwa Bunge liendelee mpaka likamilishe kazi ya kutunga katiba inayopendekezwa. Kwamba wamekubaliana kuwa Bunge Maalum likamilishe kazi yake na ana imani kuwa kazi hiyo itakamilika. Anasema kuwa bunge hili haliendeshwi kwa kelele za barabarani bali linaendeshwa kwa sheria. Alitaja sheria hiyo kuwa ni GN 254 ambayo inataja uhai wa bunge hili kuwa unaishia tarehe 5 Oktoba 2014. Amempongeza Rais Kikwete kwa kuwa mfano wa kuigwa katika kuleta suluhu ya jambo hili.

Amesema kuwa kila mtu amerekodiwa jinsi alivyoongea wakati wa majadiliano hivyo ameomba zitengenezwe CD na kuzisambaza ili Watanzania wajue nini viongozi wao waliongea. Anawashangaa sana ukawa kwa kupiga kelele barabarani ilhali wakiwa na Rais hawakuongea wanayoongea mtaani. Anasema kuwa yale waliyoongea mbele ya waandishi wa habari ndiyo waliyokubaliana wakati wa mazungumzo. Anasema kuwa bunge hili lina watu makini na amewataka wabunge wajiamini ili wakamilishe kazi zao kwa wakati.

Anasema kuwa kuna mambo mengi mazuri yamezungumzwa kwenye bunge maalum hasa juu ya mambo yanayowahusu watanzania. Ametaja mambo hayo kuwa ni yale yanayowahusu wakulima, wafugaji, wavuvi nk. Pia amesema kuwa suala la muungano limepatiwa ufumbuzi. Kwamba Rais wa Zanzibar atakuwa makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu atakuwa Makamu wa Pili wa Serikali ya Muungano.
 
  • Thanks
Reactions: gsu
Duh, hawa misukule hawajui kusoma alama za nyakati au wanatufanyia makusudi?, Rasilimali zetu chache zinaendelea kufujwa kwa ishu ambayo iko wazi kuwa haitakuwa na tija.
 
Mchangiaji kwanza ameanza na ibara iliyotawala mjadala siku ya jana ya Uraia Pacha. Pia amesema Mbunge lazima awe na angalau elimu ha kidato cha nne
 
Edit heading yako kaka, leo ni tarehe 11 Sept.....
 
Madamu UKAWA wamekubaliana na Mkuu wa nchi na kuona Bunge liendelee , sidhani kama sisi tunaweza kusema lisiendelee. UKAWA na Rais ni wawakilishi wetu katika hilo, hatuna budi kukubaliana nao
 
Pamoja na Uzuri wa Uraia Pacha, lakini Chonde Chonde, Katika Uraia huo Pacha, kuwe na kipengele kitakacho sema kua, ili Raia Pacha awe kiongozi, lazima awe raia wa kuzaliwa Tanganyika au Zanzibar kwa Uasili wa Wazazi wake Wote au angalau Mmoja.

Wasiwasi wangu isije tukajikuta, Bunge lote limejaa Wachina na Rais wa Tanzania ni Mchina Mheshimiwa Hu jin che
 
Ahsante kwa tarifa mkuu endelea kutujuza kila kinachojiri pamoja sana.
 
Madamu UKAWA wamekubaliana na Mkuu wa nchi na kuona Bunge liendelee , sidhani kama sisi tunaweza kusema lisiendelee. UKAWA na Rais ni wawakilishi wetu katika hilo, hatuna budi kukubaliana nao

Naungana na wewe kwa dhati kabisa tunasonga mbele mungu awe na sisi.
 
Mahakama ya Kadhi bado ni agenda kuu kwenye majadiliano haya, busara , kuvumiliana lazima vitawale katika hili.
 
Najiuliza hii katiba isipopatikana hawa wajumbe waliomo humo ndani watatuambia nini.......maskini Tanzania na Watanzania wake.
 
Ni dhahiri uwakilishi wa wanawake, watu wenye ulemavu katika Bunge la jamhuri ya Muungano na vyombo vingine vya maamuzi vimepewa uzito sana katika mijadala na niseme tu kwamba ibara hizi zitaungwa mkono takribani na wabunge wote.
 
Hivi nyie huko dodoma mnajuwa kuwa mnatukera sana?
Haki ya nani ngoja tuje huko na bakora tu ndo mtaelewa kuwa tumewachoka.
Mnakula pesa yetu for nothing.......... grrrrrrp!!!!!!!!!!
 
Hivi nyie huko dodoma mnajuwa kuwa mnatukera sana?
Haki ya nani ngoja tuje huko na bakora tu ndo mtaelewa kuwa tumewachoka.
Mnakula pesa yetu for nothing.......... grrrrrrp!!!!!!!!!!
Mimi nawajuza kinachoendelea jamani, suala la ni halali Bunge liendelee au la nadhani tungewauliza UKAWA waliokutana na Rais na kukubaliana liendele, huwenda wameona kuna sababu za msingi kwa Bunge kuendelea
 
Back
Top Bottom