Yaliyojiri bungeni Dodoma: Alhamisi tarehe 11 Septemba, 2014 - Kikao cha 38

Hivi nyie huko dodoma mnajuwa kuwa mnatukera sana?
Haki ya nani ngoja tuje huko na bakora tu ndo mtaelewa kuwa tumewachoka.
Mnakula pesa yetu for nothing.......... grrrrrrp!!!!!!!!!!

Nani atusaidie watanzania
Pesa yetu inaliwa tu bure
Wanasiasa wameamua kutudhulumu pamoja na umaskini wetu
Ila sisi watanzania wajinga mno
Tutaishia kuongea tu
 
Mimi nawajuza kinachoendelea jamani, suala la ni halali Bunge liendelee au la nadhani tungewauliza UKAWA waliokutana na Rais na kukubaliana liendele, huwenda wameona kuna sababu za msingi kwa Bunge kuendelea

Sisi tunakuuliza wewe ripota wao...bunge hilo linasaidia nini kwa sasa?...ilihali mchakato utaanza upya kwenye serikali ijayo......Huoni kama mnang'ang'ania kufilisi hela zetu...kodi zinauma we acha tu
 
Kwa Mujibu wa Mjumbe Wa Bunge Maalum la Katiba, amedai kua Wakiristo Nchini ni Milioni 28. Mjumbe huyo ambae kiimani ni Baba Askofu (kwa wakirsto) alisema hayo bila woga!

Mjumbe huyu ametumia vizuri uhuru wake wa kuongea lolote ndani ya Bunge. Lakini mimi naona kama amewapunja kidogo. Vizuri angesema Wakristo wapo milioni 38. Who cares?. Tunachotaka sisi ni INDEPENDENT CENSUS.

Kwani sheikh akiibuka hapo na Akasema kua Waislamu wapo Milioni 39, nani atakua ameliambia taifa ukweli?.
 
Itakumbukwa kwamba moja ya mada zilizotawala kwenye mijadala ya Bunge Maalum la Katiba ni hoja ya mwanasiasa wa siku nyingi, mzee Kingunge Ngombale Mwiru ya kutaka Katiba iwe na Sura inayojitegemea ya Uchumi ili Taifa liwe na Dira yaUchumi kwa Maendeleo yaTaifa. WAJUMBE wengi wamependekeza hoja hiyo kuungwa mkono. FUATILIA mzee Kingunge akifafanua juu ya hoja yake.
 
Hoja ya ya Uchumi ya mzee Kingunge inaanza kuingia kichwani mwangu, anasema, Ndege, Treni, Reli, nguo n.k tunavyovitumia vinatengenezwa nje ya nchi na sisi wataalam wetu wameridhika kuwa watu wa kukarabati. Anatka taifa lijenge uchumi wa kisasa wa taifa linalojitegemea. Tufanye mapinduzi ya elimu, kilimo, ufugaji, viwanda , sayansi na technolojia.
 
hivi nyie huko dodoma mnajuwa kuwa mnatukera sana?
Haki ya nani ngoja tuje huko na bakora tu ndo mtaelewa kuwa tumewachoka.
Mnakula pesa yetu for nothing.......... Grrrrrrp!!!!!!!!!!
nimekupendajeeeee..........
 
Hawa itabidi wakitoka huko bungeni watafute kisiwa chao wakaishi huko,
la sivyo warudi na hela zetu mkononi.

Nani atusaidie watanzania
Pesa yetu inaliwa tu bure
Wanasiasa wameamua kutudhulumu pamoja na umaskini wetu
Ila sisi watanzania wajinga mno
Tutaishia kuongea tu
 
Hawa itabidi wakitoka huko bungeni watafute kisiwa chao wakaishi huko,
la sivyo warudi na hela zetu mkononi.

Mi naona CCM ,UKAWA wote walewale tu
Wanajali matumbo yao na ubinafsi
Wametumia Bil 21 na sasa mchakato wameuharibu makusudi
wanataka ili baadae wale pesa zetu tena
Wale wa dodoma nao wamekuwa wabishi kisa laki tatu kwa siku.
Wanatakiwa watumie tu common sense
Wanafanya hivyo vikao kwa manufaa yapi sasa.
Watu tunakatwa mamilioni ya PAYE alafu wao wanazitumia bureee tu
 
Itakumbukwa kwamba 09/09/2014 wakati akichangia majadala wa taarifa za Kamati , aliwataka Waislamu wote kukutana na kuweka msimamo wa kutoiunga mkono Katiba inayopendekezwa kama Mahakama ya Kadhi haitaingizwa kwenye Katiba. mh. MTUTURA ameomba radhi watanzania kupitia Bunge hilo hilo Maalum la Katiba. MAKAMU mwenyekiti amempongeza kwa kujikosoa mwenyewe na kuwaasa Wajumbe wengine kuiga mfano wa Bwana MTUTURA
 
Mh mtutura amefuta kauli zake zote kali alizotoa katika kudai mahakama ya kadhi,amesema kwamba kwenye bango kitita ameona kwamba taratibu zao na za watu wa mila zitazingatiwa,cc kahtaan MZIMU Ritz,
 
Last edited by a moderator:
Ni jambo la busara sana amelifanya..walimjaza jazba ila amekaa na kuutafakari ukweri
 
I think wa tz sasa mna majibu sahihi kuhusu chama tawa name viongozi wake kupitia BMK
 
Mwenyekiti wa TCD, John Cheo amesema walichokubaliana na Rais wakiwemo UKAWA ni kwamba Bunge linaloendelea lipate Katiba inayopendekezwa na Wananchi. CHEYO amesema Video za ambacho kila mtu aliongea wakati wa kikao na Rais zipo. CHEYO amekwenda mbali zaidi na kusema BUNGE Maalum la Katiba haliongozwi na Mtu wa bararani. Mzee Cheo amewataka Wabunge wa Jumbe Maalum la Katiba wajiamini kwa kile wanachokifanya.
 
Akitoa mchango wake kwenye Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa TCD na UDP John Momose Cheyo anasema kuwa mchakato wa bunge unaendelea vema. Alisema kuwa wakati walipozungumza na Rais Kikwete, wajumbe wa TCD walikubaliana kuwa Bunge liendelee mpaka likamilishe kazi ya kutunga katiba inayopendekezwa. Kwamba wamekubaliana kuwa Bunge Maalum likamilishe kazi yake na ana imani kuwa kazi hiyo itakamilika. Anasema kuwa bunge hili haliendeshwi kwa kelele za barabarani bali linaendeshwa kwa sheria. Alitaja sheria hiyo kuwa ni GN 254 ambayo inataja uhai wa bunge hili kuwa unaishia tarehe 5 Oktoba 2014. Amempongeza Rais Kikwete kwa kuwa mfano wa kuigwa katika kuleta suluhu ya jambo hili.

Amesema kuwa kila mtu amerekodiwa jinsi alivyoongea wakati wa majadiliano hivyo ameomba zitengenezwe CD na kuzisambaza ili Watanzania wajue nini viongozi wao waliongea. Anawashangaa sana ukawa kwa kupiga kelele barabarani ilhali wakiwa na Rais hawakuongea wanayoongea mtaani. Anasema kuwa yale waliyoongea mbele ya waandishi wa habari ndiyo waliyokubaliana wakati wa mazungumzo. Anasema kuwa bunge hili lina watu makini na amewataka wabunge wajiamini ili wakamilishe kazi zao kwa wakati.

Anasema kuwa kuna mambo mengi mazuri yamezungumzwa kwenye bunge maalum hasa juu ya mambo yanayowahusu watanzania. Ametaja mambo hayo kuwa ni yale yanayowahusu wakulima, wafugaji, wavuvi nk. Pia amesema kuwa suala la muungano limepatiwa ufumbuzi. Kwamba Rais wa Zanzibar atakuwa makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu atakuwa Makamu wa Pili wa Serikali ya Muungano.
 
Niko namsikia mzee cheyo live. Anaonekana anawaponda wenzie waliokaa pamoja na rais kwenye mashauriano kuhusu katiba mpya. Anasema mh. Rais amekubali ila waliyokubaliana hakuyasaini. Kati ya watu ambao ukawa wanapashwa wawang'oe ni hii misukule ya ccm. Amemaliza muda wake lakini mwenyekiti kamuongezea muda. Misukule mingine ya ccm imepiga makofi sana kumshangilia
 
Huyo nae si popo? mzee na mvi zake anakesha club mpaka asubuhi... Lazima atetee ulaji ili apate hela za kukeshea bar!
 
Katuni%2BSix.jpg
 
Hapo wasomi wamejitoa ufahamu ili tu waendelee kusaini posho hivi hawajasikia siku RAis alipokutana na Tcd walisema,hiyo kitu isitishwe hadi tutakapompata Rais mpya 2015
 
Back
Top Bottom