Ya ITV & RFA NA TANGAZO LA KULAZIMISHA NGONO...

Nilikuwa nakuja kupost kuhusu hili tangazo,kumbe linawakera wengi. Nimesikitishwa sana na kituo kama ITV kuruhusu tangazo kama hili kurushwa hewani. Halina maadili hata kidogo, ni aibu umekaa na mama yako kisha linawekwa tangazo hilo, mbaya zaidi ni kuwa huwa ni katika taarifa ya habari ya saa mbili ambapo huwezi kuacha kuangalia. ITV naamini ina wahariri makini, nawaomba waliondoe haraka kwani wanajishushia hadhi.
 
Ni tatizo la serikali legelege. Enzi zile marehemu Remmy Ongala (RIP) alitunga wimbo wa mambo kwa soksi ukapigwa ban...leo kelele za mapenzi halafu kimya...tusishangae ikafuatia kuweka na picha. Ingekuwa kwa Mao tayari kituo kingekuwa kimefungiwa na uongozi mzima uko rumande. Kuzaliwa tz nako sio dili kabisa..inaudhi..inakera. yaani we acha tu!
 
Tunawapa wazazi wakati mgumu sana kutazama/kusikiliza hili tangazo wakiwa na watoto wao..
Binafsi hili tangazo linalorushwa ITV na redio hasa RFA halina maadili, kuna ulazima gani wa kurusha sauti ya mwanamke akilalamika kwa sauti huku mwanamume akisikika kwa sauti ya kulazimisha kufanya mapenzi.

Kamalengo la tangazo hili ni kutoa uelewa juu ya unyanyasaji wa kijinsia, watoaji wa tangazo hili wamekosa namna nyingine ya kutoa ujumbe huu? Hivi hakuna tume ya maadili na malezi ambayo inaweza kudhibiti matangazo kama haya?

TAFAKARI!
Hli Tangazo nimeliona jana ni la kingese sana aisee ni aibu kuangalia na mzazi wako yaani ni la kipuuzi kupita kiasi yaani maadili hayajazingatiwa kwa kweli.
 
TCRA wao wanaabgalia DSTV maana wengi wao wamefungiwa za bure kutetea maslai ya DSTV hapa nchini
 
Nilijua ni peke yangu nnayetapishwa na tangazo hili, kumbe wengi! Huwa tangazo hilo likianza naona bora niwatume watoto ghafla kwenda dukani kuninunulia konyagi hata kama ipo kwenye stock ndani!
Ni tangazo la aibu na kuzidhalilisha familia na halifundishi kitu!
 
Sasa wazazi si muwafafanulie watoto kinachofanyika kwenye hilo tangazo?
Maana msipowajibu, watawauliza wrong pipo, na watajibiwa hadi kwa practico!

Msendekwa,
Ukiwa unakaa na watoto na ni responsible parent/guardian huwezi kulipenda hilo tangazo.
 
Nilijua ni peke yangu nnayetapishwa na tangazo hili, kumbe wengi! Huwa tangazo hilo likianza naona bora niwatume watoto ghafla kwenda dukani kuninunulia konyagi hata kama ipo kwenye stock ndani!
Ni tangazo la aibu na kuzidhalilisha familia na halifundishi kitu!

hii hatari, hata wazee wamekasirishwa..
 
Duh ilo tangazo kwa kweli ni aibu 2 afu mara nyingi wanalirusha muda mbaya karibu na taarifa ya habari apo familia nzima mpo sebuleni
 
Lakini jaman twende mbele turudi nyuma,hili tangazo linauwalisia wa mambo wanayo tendeana wana ndoa,so kwa vile wa tz hatupend kuambiwa kweli basi hii ni nongwa....

Hili tangazo limekaa vibaya. Siku likitangazwa utakapokuwa na Mkwe wako ndio utajua kama sio zuri, au unajifanyisha? Mbona hatulalamikii lile ambalo jamaa (nadhani ni mtu wa Mara) anavyomkung'uta mke wake? ( Nimesema, usi, rudie, tena, kosa, hili ulilolifanya sasa hivi, mhh, mhh, nyamaza, kelele) kwa kweli mie linanifurahisha...!
 
si kila kitu kinaoendeza. Ukweli ni kuwa ujumbe umegonga ikulu kwani wengi huliona hasa wakati wa taarifa za habari. Katika hili naona watu wa jenda wana mkono pia. Lengo likitimia tangazo litatolewa
 
Kama Aunt yako angekupa masomo juu ya mapenz ktk muda muwafaka,usingeshanga ila kwa vile100% ya watanzania wazaz hawana muda kuwaambia watoto wao juu ya mabadiliko ya tabia ktk miili yao watu tunaoneana aibu.

kila kitu kina muda wake na mahali pake,,,na huwa naongea nae masuala ya mahusiano na ndoa,lakini content za tangazo mdau,hazijasimama
 
Lakini jaman twende mbele turudi nyuma,hili tangazo linauwalisia wa mambo wanayo tendeana wana ndoa,so kwa vile wa tz hatupend kuambiwa kweli basi hii ni nongwa....

kwanza inaonekana bado hujajijua wewe na usemalo hulijui,hebu angalia hapo kwenye red kama upo sahihi wewe. Tuachane na hilo kwanza twende upande mwingine wa shilingi,hilo tangazo halina content validity kwa jamii ya wa jamii ya watu mchanganyiko with regard to age. sidhani kama utakuwa comfortable listening to that advert with your elders or young children unless uwe na certain abnormalities in your mind.
navyokuona wewe unaweza sema hata ndoa za jinsia moja ni sawa kwa sababu ni haki za binadamu kwa sababu hata hilo TANGAZO liko against maadili ya kitanzania kama hizo ndoa tu zilivyo na mwishowe utasema NGONO ijadiliwe in public
 
Lakini jaman twende mbele turudi nyuma,hili tangazo linauwalisia wa mambo wanayo tendeana wana ndoa,so kwa vile wa tz hatupend kuambiwa kweli basi hii ni nongwa....

Na mambo wanayotendeana wana ndoa huwa yanafanyika sirini, na si hadharani, tena pengine watoto wakiwa wamelala. Sasa iweje leo yawekwe hadharani? Wewe unaweza kumvuta Mumeo/mkeo kuelekea chumbani mbele ya wanao? Acha ulimbukeni wewee, hata kama ni .com, bado maadili yetu yanatuhusu sana
 
.
Ni freemasons hao. Wanakiandaa kizazi cha kitanzania kisaikolojia kabla ya kuanza kujadili suala la uhahali wa ndoa za jinsia moja.
.

Mambo mengine tunajitakia wenyewe alafu tunamsingizia shetani ama freemason kwani kama kuna njia mbadala ya kukabiliana nayo ama kuna taasisi husika kwanini haijui wajibu wake!?
 
Hivi kweli jamani unaweza ukarusha tangazo kama hili? hakika jana mbele ya wanangu nimeaibika vibaya hawa jamaa ni pumbavu sana hawana maana....
 
Back
Top Bottom