Ya ITV & RFA NA TANGAZO LA KULAZIMISHA NGONO...

Tunawapa wazazi wakati mgumu sana kutazama/kusikiliza hili tangazo wakiwa na watoto wao..
Binafsi hili tangazo linalorushwa ITV na redio hasa RFA halina maadili, kuna ulazima gani wa kurusha sauti ya mwanamke akilalamika kwa sauti huku mwanamume akisikika kwa sauti ya kulazimisha kufanya mapenzi.

Kamalengo la tangazo hili ni kutoa uelewa juu ya unyanyasaji wa kijinsia, watoaji wa tangazo hili wamekosa namna nyingine ya kutoa ujumbe huu? Hivi hakuna tume ya maadili na malezi ambayo inaweza kudhibiti matangazo kama haya?

TAFAKARI!

Mkuu tindikalikali, ebu nikuombe utuwekee clip au youtube link ya hilo tangazo hapa ili ambao hatujabahatika pia tupate kulisikia.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom