Ongezeko kubwa la wagonjwa wa akili nchini; Je, jamii ina elimu ya kutosha juu ya namna ya kukabiliana na janga hili?

Undava King

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
3,205
5,333
Kwa kipindi kirefu tumekuwa tukiyapa kipaumbele magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza, ambapo kwa kiasi kikubwa yameelezewa kwa mapana yake kuhusiana na chanzo, dalili, na tiba zake.

Huku semina na mafunzo mbalimbali ya uelimishaji yakifanywa kwa umma kupitia Serikali na wadau wake, lakini aghalabu mara chache sana kuona suala la magonjwa ya Akili au Saikolojia yakipewa kipaumbele.

Leo hii kuna ongezeko kubwa sana la wagonjwa wa akili kiasi kwamba hospitali zetu zimefurika wagonjwa wa namna hii na kama hujawahi tembelea mahospitalini au kufikwa na tatizo kama hili uwezi ng'amua ukubwa wa tatizo.

Kama tunavyojua magonjwa ya akili ni mengi na yana madhara makubwa juu ya afya ya mgonjwa na jamii inayomzunguka.

Kama hatua za kumtambua mgonjwa na kumfikisha mapema hospitalini kupata matibabu stahiki hazitochukuliwa mapema zinaweza kupelekea madhara makubwa ikiwemo kifo, uwendawazimu,kufarakanisha jamii, kupoteza vipato vya familia, kutotimia kwa malengo n.k

Leo nimeona nizungumzie Uwendawazimu (Psychopath) ambao ni moja ya ugonjwa ambao wengi wetu pengine tumezaliwa na au tuko nao na tunaishi nao pasipo kufahamu kuwa tu wagonjwa mpaka pale utakaposababisha madhara makubwa kwetu au kwa jamii inayotuzunguka.

Je, utatambuaje kuwa wewe ni Mwendawazimu au Psychopath?

1. Mpotoshaji (manipulative)- kujikuta mara kwa mara unapotosha ukweli na unapenda kuongea uongo kwa nia ya kuumiza wengine na huoni kama ni hatia kuingiza wengine kwenye matatizo.

2. Kukosa uaminifu (dishonest) unajikuta uwezi kuaminiwa katika suala lolote linalohitaji uaminifu kwani ukipewa nafasi kama hiyo lazima uharibu kwa kukwapua au kushindwa kulipa hisani.

3. Unajijali mwenyewe (narcissistic) we ni mbinafsi kiasi kwamba kila jambo unahisi unastahili wewe tu na siyo wengine, huko sociopath kiasi kwamba huwezi kujua wengine wanajisikia vipi au kujali hisia zao kwa yale unayowatendea iwe wameumia au wanafuraha kwako si kitu

4. Huna majuto (unremorseful) Binadamu mwenye akili timamu anatambua kuwa katenda makosa au kuna jambo alikwenda sawa na matarajio yake hivyo upitia kipindi cha majuto lakini kwako hili halipo.

5. Huna hisia za upendo au huruma (non empathetic)-Mara nyingi unajikuta huko bize na mambo yako tu iwe ni kazini,mtaani au nyumbani huwezi kujihusisha nakutaka kujua hisia za wengine, matarajio yao, mahusiano, kuwapatia msaada, sadaka, kutembelea wenye uhitaji, kuwapa pole wagonjwa au kuhisi kuguswa na habari mbaya ya msiba au ajali n.k

6. Mnyonyaji (exploitative) kuwa na tabia ya kupenda maisha yasiyo halali na halisi na kufanya mabaya kuwa ndiyo ngazi ya mafanikio au furaha yako yaweza kuwa pia sehemu ya dalili za Uwendawazimu mfano ni kujihusisha na ujambazi/uhalifu (criminality), Uasherati/uzinzi (promiscuity) na Uvivu (lack of responsibility)

Dalili zingine ni pamoja na:-
a) Kupenda au kuwa na hisia za kutaka kuua hasa binadamu, na ukifanya kitendo hicho unajihisi ridhiko moyoni mwako na ukikaa pasipo kumwaga damu ujisikii vizuri.

b) Kupenda kubaka hasa watoto wadogo na watu wazima wanaokuzidi umri pengine hadi wanafamilia yako unawafanyia ukatili huo wa kingono na vipigo juu kwa mke na watoto.

c) Kuona Maruweruwe (hallucinations) Mara kwa mara umekuwa ni mtu wa kuona na kusikia sauti au milio ya vitu visivyoonekana kwa macho, unaweweseka ukiwa macho ama usingizini, unaongea kimya kimya au kwa sauti na kujijibu peke yako pengine ukiwa hata matembezini mwenyewe.

d) Unadhibiti taarifa mbaya(unaphobia katika jambo fulani ulilolificha moyoni)-mara nyingi hupendi kusikia jambo ambalo linaumiza hisia zako za ndani au kitu ambacho kilipelekea ukawa mgonjwa, endapo ni kitu unachokiofia au kukichukia kikitajwa au kujitokeza mahala ulipo lazima uweweseke, utatikisa kichwa,kupikicha masikio au macho na kuonesha ishara ya kutetemeka baadhi ya viungo vya mwili kama mikono na midomo, kutamani kulipiza kisasi muda huo huo au kupoteza fahamu au kama ni mjadala utafanya juu chini jambo hilo lisiongelewe kabisa, hii uwatokea hasa wale wagonjwa waliowahi kukumbwa utotoni na vitendo vya ukatili kama ubakaji, kunusurika kuuawa,unyanyasaji wa kijinsia, ugumu wa maisha,n.k

e) Wizi, Uchawi na kupenda mno kufanya au kuhusisha kila tukio linalokutokea au kutokea wengine na ushirikina.

f) Upweke wa kujitakia- hii ni ile hali ya kujikuta unajitenga na watu na utaki mahusiano na yeyote yule bali unataka kuwa peke yako muda wote na hata huna sababu ya kufanya hivyo isipokuwa unajihisi tu kuwa hiyo ndiyo hali inayokupa utulivu na amani.

g)Kuwa na mgogoro wa nafsi wa mara kwa mara au wakudumu, ambapo muda mwingi kuna hisia inakutuma fanya nyingine inakwambia usifanye mpaka unajihisi kuchanganyikiwa na usijue nini cha kufanya.

h) Huna mpenzi na hata ukiwa nae hamaanishi chochote kwako, huna rafiki wala mahusiano na yeyote, kwako mapenzi na familia hayana thamani yeyote ni kama hisia ambazo hauko interested nazo na hata urafiki pia hauna haja nao.

i) Una urahibu usiyo wa kawaida au uliopitiliza katika jambo fulani kiasi kwamba unaugua au kurukwa na akili usipofanya jambo hilo. Mfano kutumia madawa ya kulevya, ngono, kamari, ulevi, muziki, caffeine, nikotini n.k

j) Mfadhaiko wa kudumu au kushindwa kudhibiti au kupambanua hofu iliyo ndani yako na kuishinda ndani ya kipindi kirefu. Mfano Kwa wale watu wa imani ya dini kusumbuliwa mara kwa mara na hisia za uwepo wa mapepo au majini au kupokea habari mbaya ya ugonjwa au tukio la kushtukiza.

k) Kukosa hisia za aibu na kutofuata maadili au miiko ya jamii husika, unaweza vua nguo hadharani au mitandaoni, kufanya mapenzi hadharani au mbele za watoto,kupigana au kutukana au kudhalilisha wengine n.k

l)Kufanya jambo kisha kusahau kama ni wewe ndiye uliyelitenda na kurudia kulitenda mara nyingine tena katika wakati mwingine na mara nyingi jambo unalokuwa umetenda linakuwa ni baya au lenye kusudio baya kama vile kudhuru, kuua, kubaka, kuiba n.k

m) Kushindwa kuacha tabia fulani hata kama ukionywa kwa namna gani au kuchukuliwa hatua ipi hata iwe ni jela utafungwa na ukimaliza tu kifungo ukirudi mtaani utarudia kutenda jambo lile lile.
 
Huu Uzi watu wanaogopa kukomenti wasije wakaonekana Wendawazim.

Binafsi niliwahi kwenda kijiji kimoja kipo Kanda ya ziwa mkoa wa Kagera nikakuta nusu ya KIJIJI wanakichaa nilishangaa snaa.
 
Huu Uzi watu wanaogopa kukomenti wasije wakaonekana Wendawazim.

Binafsi niliwahi kwenda kijiji kimoja kipo Kanda ya ziwa mkoa wa Kagera nikakuta nusu ya KIJIJI wanakichaa nilishangaa snaa.

Kitaje mkuu uenda wakawepo humu wakazi wa hicho kijiji wakatuambia nini chanzo au kipi kiliwasibu kwenye kijiji chao.

Lakini vilevile uwezi jua pengine madaktari na mashirika ya kibinadamu yanayodili na mambo ya afya au tafiti yanaweza kuwafikia walengwa na ukawa ni msaada.
 
Nimekumbuka ripot ya twaweza
Pasipo hata ripoti ya twaweza wewe tembelea hospitali zetu kubwa nchini huko muhimbili au bugando upande wa magonjwa ya akili kumefurika, hali inatisha unaweza fikiri upo sokoni watu ni wengi mno na kila siku wanazidi kuongezeka juhudi za makusudi zinapaswa kuchukuliwa kunusuru hili.
 
Back
Top Bottom