Ya ITV & RFA NA TANGAZO LA KULAZIMISHA NGONO...

tindikalikali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
4,855
1,117
Tunawapa wazazi wakati mgumu sana kutazama/kusikiliza hili tangazo wakiwa na watoto wao..
Binafsi hili tangazo linalorushwa ITV na redio hasa RFA halina maadili, kuna ulazima gani wa kurusha sauti ya mwanamke akilalamika kwa sauti huku mwanamume akisikika kwa sauti ya kulazimisha kufanya mapenzi.

Kamalengo la tangazo hili ni kutoa uelewa juu ya unyanyasaji wa kijinsia, watoaji wa tangazo hili wamekosa namna nyingine ya kutoa ujumbe huu? Hivi hakuna tume ya maadili na malezi ambayo inaweza kudhibiti matangazo kama haya?

TAFAKARI!
 
Hili tangazo linakera sana, mkuu. Sijajua kama TCRA huwa na wao wanatazama TV! Au wanapokuwa mahome kwao vinakuwa haviwahusu...
 
Nafurahi kuwatangazia wajumbe wa ukumbi kuwa sijawahi kulisikia/kuliona tangazo hilo maana radio ninayoisikiliza muda mwingi ni Radio Safina!
 
Nimelisikia hilo tangazo jana. Sikuamini nilichokuwa nasikia. Unatoaje tangazo kama hilo kwenye 'prime time' Huu ndio muda familia wanafuatilia habari, halafu wanaweka mambo ya ajabu kabisa. Kwa nini wasiweke saa nne au tano za usiku?
 
Naunga mkono hoja. Kijana wangu-very curious aliniuliza anamfanyaje? Nikaishiwa maneno! Tz tunapoenda na utandawazi si pazuri
 
Kwa kweli,halifai! Na linawapa wakati mgumu sana litangazwapo,mzazi akiwa karibu na watoto wake!
 
Mimi jana nilikuwa na mzazi wangu asubuhi kwenye gari,hilo tangazo lilipowekwa ilikuwa aibu tupu,mamangu alikuwa anatafuta mlango wa kutokea.Aibu tupu!!!!!!!!!!!!!
 
Sasa wazazi si muwafafanulie watoto kinachofanyika kwenye hilo tangazo?
Maana msipowajibu, watawauliza wrong pipo, na watajibiwa hadi kwa practico!
 
Tunawapa wazazi wakati mgumu sana kutazama/kusikiliza hili tangazo wakiwa na watoto wao..
Binafsi hili tangazo linalorushwa ITV na redio hasa RFA halina maadili, kuna ulazima gani wa kurusha sauti ya mwanamke akilalamika kwa sauti huku mwanamume akisikika kwa sauti ya kulazimisha kufanya mapenzi.

Kamalengo la tangazo hili ni kutoa uelewa juu ya unyanyasaji wa kijinsia, watoaji wa tangazo hili wamekosa namna nyingine ya kutoa ujumbe huu? Hivi hakuna tume ya maadili na malezi ambayo inaweza kudhibiti matangazo kama haya?

TAFAKARI!

dah jana ndo nimeliona nilikua na aunt yangu,,,sikujisikia vizuri,na yeye mwenyewe aliguna....tena wameliweka wakati wa break ya taarifa ya habar,,,,thoz medi wapo kipesa kuliko maadili so TWENDE TU
 
Halafu ile sauti ya mwanadada imekaa kama ya Wema Sepetu hivi
 
Lakini jaman twende mbele turudi nyuma,hili tangazo linauwalisia wa mambo wanayo tendeana wana ndoa,so kwa vile wa tz hatupend kuambiwa kweli basi hii ni nongwa....
 
Tangazo hili kwa kweli linakera sana na hivi waandaaji wa matangazo ya namna hii hawajui maisha ya Watanzania kuwa vyombo vya habari kama tv tunaangalia kifamilia. Tangazo hili kwa kweli linaleta aibu walifute.
 
Back
Top Bottom