Nzowa Godat
JF-Expert Member
- Jun 15, 2011
- 2,783
- 819
Hata mimi naafiki kabisa kwamba tangazo hili ni la KISHENZI, out of ethics, la ki-freemason, immoral labda wangetangaziwa walengwa tu lingekuwa ok
tangazo la kishenz kupata kutokea,alafu linawekwa wakati wa taarifa ya habari,kwakweli litawatia aibu wengi!
Hakuna cha aibu wala nini, utitiri wa matatizo ktk ndoa unasababishwa na kubakana ktk ndoa, wanaume wakitanzania hawajuwi kubembeleza hadi mwenz wake ajisikie ila wanalazimisha sm tm hata kwa maandiko, tusinyimane... Ujinga huu tunajenga taifa lisilo na ndoa madhubuti ila malalamiko ambayo mwisho wake kuvunjika ndoa.
hivi vitu vya misaada vina matatizo sana,maana lile tangazo ni msaada wa wamarekani,mimi ndo maana nauchukia umaskini
tunawapa wazazi wakati mgumu sana kutazama/kusikiliza hili tangazo wakiwa na watoto wao..
Binafsi hili tangazo linalorushwa itv na redio hasa rfa halina maadili, kuna ulazima gani wa kurusha sauti ya mwanamke akilalamika kwa sauti huku mwanamume akisikika kwa sauti ya kulazimisha kufanya mapenzi.
Kamalengo la tangazo hili ni kutoa uelewa juu ya unyanyasaji wa kijinsia, watoaji wa tangazo hili wamekosa namna nyingine ya kutoa ujumbe huu? Hivi hakuna tume ya maadili na malezi ambayo inaweza kudhibiti matangazo kama haya?
Tafakari!
nilijua ni peke yangu nnayetapishwa na tangazo hili, kumbe wengi! Huwa tangazo hilo likianza naona bora niwatume watoto ghafla kwenda dukani kuninunulia konyagi hata kama ipo kwenye stock ndani!
Ni tangazo la aibu na kuzidhalilisha familia na halifundishi kitu!
inatisha sana,kwa namna hii,tunadhalilishwa sana wazazi na tangazo,laiti ningekuwa mkoma tcra ningejiudhuru haraka sana ama kuliban hilo tangazo haraka sana
Tunawapa wazazi wakati mgumu sana kutazama/kusikiliza hili tangazo wakiwa na watoto wao..
Binafsi hili tangazo linalorushwa ITV na redio hasa RFA halina maadili, kuna ulazima gani wa kurusha sauti ya mwanamke akilalamika kwa sauti huku mwanamume akisikika kwa sauti ya kulazimisha kufanya mapenzi.
Kamalengo la tangazo hili ni kutoa uelewa juu ya unyanyasaji wa kijinsia, watoaji wa tangazo hili wamekosa namna nyingine ya kutoa ujumbe huu? Hivi hakuna tume ya maadili na malezi ambayo inaweza kudhibiti matangazo kama haya?
TAFAKARI!
athari za utandawazi hizo shughuli ipo
Ni tatizo la serikali legelege. Enzi zile marehemu Remmy Ongala (RIP) alitunga wimbo wa mambo kwa soksi ukapigwa ban...leo kelele za mapenzi halafu kimya...tusishangae ikafuatia kuweka na picha. Ingekuwa kwa Mao tayari kituo kingekuwa kimefungiwa na uongozi mzima uko rumande. Kuzaliwa tz nako sio dili kabisa..inaudhi..inakera. yaani we acha tu!
Wandugu,
Nimefatilia kwa makini mjadala huu lakini kikubwa kinacho onekana ni malalamiko tu pasipo kuweka wazi hoja ya msingi. Tunaposema tangazo halina maadili, tuna maanisha nini? Hivi, maadili yetu "watanzania" ni yapi hasa? Kihistoria, 'maadili ya mtanzania' imekuwa ni zaidi ya dhana ya kudhania na kufikirika tu. Hakuna mahala pamepata kuwekwa orodha ya "Haya Ndio Maadili Yetu". Yapo? Yaliwekwa na nani? Kwa maoni yangu, niko tayari kukosolewa kwa hoja sahihi, dhana ya "Maadili Yetu" imekuwa ikitumiwa vibaya na baadhi ya wenzetu, aidha viongozi, wanajamii wa kawaida ama makundi fulani fulani ili kuweza kulinda maslahi ya chochote kile ambacho wataona kuwa hakivutii utashi wao. na kisha kutaka kuaminisha umma mzima wa "watanzania" kuwa kile wasichokifurahia, basi hakistahili kwa umma uliobaki. Hii ni dhana potofu!
Pia tukirejea kwenye ma/tangazo husika, jamani, si linasema wazi kuwa "Kulazimisha mapenzi, hata kwa mke wako ni ukatili!"? Ina maana hatukubaliani na suala hili? Ama ni kwa kuwa tumekua tukiaminishwa kuwa ukiwa na mke unaweza kufanya naye mapenzi wakati wowote, sehemu yoyote hata kama yeye hajisikii hivyo? Sio sahihi jamani, vitendo hivi vimekuwepo, vipo, baadhi yetu wanavifanya na hawana budi kuviacha. Bila shaka, yawezekana ujumbe huu ukawa umegusa maslahi ya baadhi yetu na ndio maana yanatokea mayowe yote haya. Sioni ajabu wala soni eti kwa ujumbe huu kutolewa wakati umekaa aidha na wakwe, wajomba, shangazi, na wengineo, kwani na wao wote na vizazi vyao wanapaswa kulielewa hili na hata kuweza kuwaelimisha wengine. Mbona elimu ya ngono, afya ya uzazi, maambukizi ya VVU n.k inafundisha hata shule ya msingi? Ina maana hata wewe waogopa kujadiliana na mtoto au watoto wako juu ya masuala haya? unasubiri akikua atajifunza mwenyewe "naturally" or as She/He go along in relationships"? OMG, by the time you realize, atakuwa ni "something else"!
Wasalaam!
Bazobonankira Bafakulelawamba