Wizi wa Kampuni za Simu na vinywaji Tanzania

Duh! Duniani kote gharama za simu zinashuka sisi ndio tunazidi kuzipaisha tena!!? Wengine tutaachana na masimu ya mikononi, tunabaki na email tu basi, by the way tutaepusha mengi ah!
mkuu kitila,

Nimeziona bei mpya za simu,na kinachonikitisha hawa wapuuzi watanza kutangaza bei hizo bila kodi na VAT ili kuwahadaa watu..kuna kampuni moja wataanza kwa kusme SMS ni sh 43. bila VAT,ila hawaitaji kodi ambayoimo ndani yake ambayo ni sh. 17.wameshaanza kutengeneza na matangazo na wametumwa na serikali

kuna kitu hapa.....Nahitaji Msaada,zitto soma PM yako
 
Sijajua bado mwelekeo wa Tanzania, kama tunaenda mbele ama tunarudi nyuma ama we are just moving sideways?

Naona hii nchi inaenda kwa manufaa ya wachache sana na wanapanga kodi kujinufaisha wenyewe... Sasa kama wanafikia mpaka kwenye simu, kitu ambacho kwa dunia ya leo kinaelekea kuwa ni muhimu kwamaisha ya kila siku ya mwanadamu. Kupandisha kodi katika simu nataka kujua ni nani atanufaika? Mtumiaji wa Mwisho ama?

Maumivu yote najua ni sisi ambao tunakomaa nayo... Tunahitaji mabadiliko ya kweli!
 
Wanataka kuturudisha kwenye enzi za kuona simu kuwa ni anasa?
Hivi ni kwanini wanatufanyia hivi???

Serikali imekosa watu makini,nahisi kuna haja ya akuwaondoa wale wote ambo wamelewa na Mvinyo wa madaraka na kukosa Tija katika utendaji wao.
 
Hili lisiwape shida... ushindani utafanya kazi yake! nadhani kuna kodi imeongezwa kwenye voice kwa ajili ya mfuko fulani... kama sio wa universal access ... sijui nini tena!
 
Gembe,nakubaliana na wewe kimsingi lakini naamini makampuni haya ya simu hayako tayari kufanya hivyo kwasasa hasa ukizingatia kwamba ushindani umekuwa mkubwa sana na gap ya tariff kwa hizi kampuni ni kubwa sana.Kwamfano Zantel na TIGo wanaweza kupandisha bei zao angalau slightly lakini VODACOM na Celtel bei zao tayari ziko juu sana na effect ya kupandisha bei kidogo itapelekea kupoteza wateja wengi sana.Lakini cha msingi zaidi ni kwamba makampuni haya mengi tayari yameshafanya Investment ya kutosha katika network wanachofanya sasa ni ku-recoup mtaji waliowekeza kwahivyo hawana gharama kubwa sana za investment na hivyo ni rahisi kuji-adjust kwenye matumizi yaani Operating expenses(OPEX) kama vile kwenye matangazo na vitu kama hivyo ili kuepusha dhahama ya kupandisha bei.

Naamini kwamba gharama za simu hazitapanda bei kwa sasa hebu tusubiri tuone.
 
Bajeti zetu mara zote huwa ni mzigo kwa mwananchi! Waandaaji wamekuwa wakiongeza kodi kule ambapo wananchi wengi u-"spend" zaidi. Na mara zote ufanya hivyo wakiamini walipaji wa kodi hiyo ni wengi zaidi, lakini wanashindwa kujua wanakwamisha wananchi kwa kiasi gani.

Kwa mfano, miaka yote wamekuwa wakiongeza kwenye vinywaji, lakini mwaka huu wameona hiyo haitoshi wameongeza kwenye sukari pia!

Tunahitaji waandaaji wa bajeti wenye kujua vipaumbele vya wananchi katika maendeleo yao ya kila siku, na vipaumbele hivyo visipandishwe kodi kiholela!
 
Duh! Duniani kote gharama za simu zinashuka sisi ndio tunazidi kuzipaisha tena!!? Wengine tutaachana na masimu ya mikononi, tunabaki na email tu basi, by the way tutaepusha mengi ah!

Mkuu Kitilya ulichosema ni kweli tupu sasa hiivi makampuni yanagombea wateja na mengi ili kuvutia wateja hao yanayotoa bei ndogo sana ili 'kuwaiba' wateja toka kwa washindani wao. Ndiyo maana nasema makampuni binafsi haina maana huduma ndiyo zitakuwa bora au zenye ufanisi na bei nafuu.
 
Gembe,nakubaliana na wewe kimsingi lakini naamini makampuni haya ya simu hayako tayari kufanya hivyo kwasasa hasa ukizingatia kwamba ushindani umekuwa mkubwa sana na gap ya tariff kwa hizi kampuni ni kubwa sana.Kwamfano Zantel na TIGo wanaweza kupandisha bei zao angalau slightly lakini VODACOM na Celtel bei zao tayari ziko juu sana na effect ya kupandisha bei kidogo itapelekea kupoteza wateja wengi sana.Lakini cha msingi zaidi ni kwamba makampuni haya mengi tayari yameshafanya Investment ya kutosha katika network wanachofanya sasa ni ku-recoup mtaji waliowekeza kwahivyo hawana gharama kubwa sana za investment na hivyo ni rahisi kuji-adjust kwenye matumizi yaani Operating expenses(OPEX) kama vile kwenye matangazo na vitu kama hivyo ili kuepusha dhahama ya kupandisha bei.

Naamini kwamba gharama za simu hazitapanda bei kwa sasa hebu tusubiri tuone.

Haina haja ya kusubiri,siku si nyingi utaanza kuona mabdailiko,tena yawezekana yameshaanza kufanyika bila wewe kujua..
 
Kwanini serikali hutoza kodi? zipo sababu nyingi sana kubwa ni mbili tu au tatu hivi; to raise funds (revenue), to regulate a commodity (kwa mfano kukifanya ghali kama mvinyo and hence discourage its use), na kulinda bidhaa nyingine (mara nyingi wanafanya hivi kwa bidhaa za nje ili kulinda za ndani).

Sasa, swali langu kubwa ni je kodi ya simu kuongezwa inafanya nini kati ya hayo matatu? Of course kama kuna mtu anaweza akanifahamisha kuwa hiyo kodi ni lazima iwe kwenye simu na si kitu kingine au kuondolewa kabisa (ulazima wa kodi hii).

Gembe, what is reasoning ya serikali kuongeza hii kodi kwenye simu?
 
Gembe, what is reasoning ya serikali kuongeza hii kodi kwenye simu?
Kama waziri alivyosema,
Sababu kubwa ya rekebisho hili ni kwenda sanjari na mfumuko wa bei (adjustment forinflation).

sijui Uchumi unasemaje katika hili ila ndiyo mojawapo ya sababu kuu,
 
Kama waziri alivyosema,
Sababu kubwa ya rekebisho hili ni kwenda sanjari na mfumuko wa bei (adjustment forinflation).

sijui Uchumi unasemaje katika hili ila ndiyo mojawapo ya sababu kuu,

wamebadillisha kodi zote kureflect inflation?
 
Na sababu nyingine ni kujaribu kubadilisha tabia za watu. kwa mfano, duniani kote kodi za pombe na sigara zipo juu sana kwa lengo la kujaribu kupunguza wanywaji na wavutaji na hivyo kuokoa afya za raia.

hapa nafikiri ndipo tunapohitaji msaada wa mbunge wa watu Zitto Kabwe, especially kwamba hili ni eneo lake la kitaaluma na kitaalamu. Zitto, sisi wapiga kura ndugu yangu hebu tuulizie haya majambo huko Dodoma!
 
Kama waziri alivyosema,
Sababu kubwa ya rekebisho hili ni kwenda sanjari na mfumuko wa bei (adjustment forinflation).

sijui Uchumi unasemaje katika hili ila ndiyo mojawapo ya sababu kuu,

Hii ni sababu tu iliyowekwa ili kuongeza mapato ya serikali kupitia kodi.
  1. Kwa nini badala ya kuongeza kodi wasingepunguza ukubwa wa serikali? Mawaziri zaidi ya 60 ni wa nini kwa nchi masikini kama TZ?
  2. Je wapinzani haya hawakuyaona? Kama wameyaona wamechukua hatua gani kuhakikisha angalau mwananchi anaelewa serikali yao inavyowaminya?
  3. Nini sasa kifanywe na mwananchi maana CCM inaelekea kukubaliana na wapinzani katika hili??
 
Hapa kweli tumepatikana sijui tutaponea wapi, unajua serikali hii imeamua kutukamua hadi tubaki mifupa, haituingiii akilini kweli sisi hawa hawa watanzania maskini tuongezewe kodi ktk mawasiliano, kula yetu taabu sijui tukimbilie wapi?
 
Hili lisiwape shida... ushindani utafanya kazi yake! nadhani kuna kodi imeongezwa kwenye voice kwa ajili ya mfuko fulani... kama sio wa universal access ... sijui nini tena!

Kwa nini tusipate shida? Huo ushidnani mbona haujatusaidia hadi hivi sasa? Hata kama wameanzisha hiyo kodi wka ajili ya mfuko fulani, kwa nini iwe siri? kwa nini wananchi ndo wafanye mbuzi wa shughuli wa kuchangia mfuko huo?
 
wamebadillisha kodi zote kureflect inflation?
Hii ni sababu ya kipuuzi sana na inadhihilisha jindi wanvyotuona sie wapumbavu,hivi hii ni sababu ya kitaalam kweli?

Nenda kapitie Bajeti vizuri unaweza kulia,Niemkuwa nikiisoma hiyo bajeti kila siku baada ya waziri flani kusoma bajeti yakle na kuangalia nini wamefanya nabakia kuumia kichwa...
 
....waache wapandishehizo bei maradufu halafu tuone loser ni nani? nakuhakikishia makampuni yatalose wateja na serikali makusanyo yataenda chini...hii vita itaishia kupiganwa kati ya hayo makampuni na serikali maana companies stand to lose big kwa hili!
 
Hii ni sababu tu iliyowekwa ili kuongeza mapato ya serikali kupitia kodi.
  1. Kwa nini badala ya kuongeza kodi wasingepunguza ukubwa wa serikali? Mawaziri zaidi ya 60 ni wa nini kwa nchi masikini kama TZ?
  2. Je wapinzani haya hawakuyaona? Kama wameyaona wamechukua hatua gani kuhakikisha angalau mwananchi anaelewa serikali yao inavyowaminya?
  3. Nini sasa kifanywe na mwananchi maana CCM inaelekea kukubaliana na wapinzani katika hili??

Mie Nadhani hili suala la kuwa na wizara nyingi ndiyo tatizo..ila tatizo kubwa ni hawa watumishi wa serikali.Ni watu wa ovyo sana..serikali imekuwa ikitoa Ajira kwa kufahamiana na imesababisha kuwa na watu wenye uwezo mdogo..

What do we do?I have an idea...
 
Back
Top Bottom