Wizi wa Kampuni za Simu na vinywaji Tanzania

Kwa hiyo ile kampuni ya Norway kutokuandikishwa na kulipa kodi ilikuwa ni cha mtoto, wazee wenyewe wako huku. Je, wamewahoji wakuu wa makampuni haya kuthibitisha wamelipa kodi kiasi gani tangu watinge bongo?
 
KAMPUNI ya vinywaji baridi ya Coca Cola imetajwa kuwa miongoni mwa kampuni zisizolipa kodi.

Akijibu, Chijoriga alizitaja kampuni kama vile Vodacom na Celtel kuwa zinalipa kiasi. "Wapo wengine ambao hawalipi kabisa," alisema na kuongeza kuwa atazihifadhi majina kwa sasa.

Haya makampuni mengi ya simu si ajabu katika bodi yao kuna vigunge humo. Kwanza mapato yao ni makubwa sana ndio maana hata wanatoa magari mengi bure...Hebu kuna mtu ameshawahi kujiuliza huwa wana charge shillingi ngapi kwa dakika unapotumia simu--jibu ni hakuna. Pili hakuna hata chombo cha serikali au binafsi kinacho mlinda consumers...kwa hiyo wanakusanya mapesa mengi sana kwa kifupi ni wanyoyaji haswa.

Hata hivyo, baadhi ya wabunge, akiwamo Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF) ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, walimtaka ataje kwa kile walichomweleza kuwa analindwa na Kamati hiyo ya Bunge na ndipo akaitaja Kampuni ya Coca Cola kuwa ni miongoni

Hivi kweli tunataka kuendelea? Tuna tatizo mahali!

Tujiulize kwa nini aogope kuitaja Coca Cola? na hii kampuni ina scandal nyingi sana katika nchi masikini...kama Bolivia walikomeshwa na serikali hiyo mpya.


If these giant companies are not paying, from where does the govt get its revenue which is increasng every month?

Mkuu ukitaka kuona hawa jamaa TRA wanvyokusanya pesa unaweza ukashangaa haswa mikoani utafikiri ni zile movies za ki mafia wale jamaa wanapokusanya protection money. TRA ndio imevunja kabisa biashara ndogo ndogo za wazawa mikoani....kuna wafanyabiashara wangapi wamejiua kwa sababu ya TRA?-Ni wengi tu.

Ndio maana wafanya biashara wengi wakubwa wa mikoani wamehamia Dar
 
Mkuu Halisi, hiyo theme unayozungumzia kama ilitakiwa kulipia kodi na makampuni hayo hayalipi kodi hiyo ndiyo dhamira ya kamati ya Bunge.
 
Mimi naona habari iko shallow sana, na si habari ya kiuchunguzi kama tunavyotegemea gazeti hilo kiandika, mwandishi amejishusha sana, at a risk ya kupata penalty.
Je kodi gani, manake hawa wenzetu kwenye formal sector wana lundo la kodi, kila dizaini, hadi magari ya wafanyakazi yana kodi tofauti na magari mengine.
Je mwandishi alijua ni kodi gani inazungumziwa? alijua ni tangu lini? alijua kama wamekwepa au ni mapungufu ya watendaji wa kampuni husika au TRA? alijua kama ni mapungufu ya sheria au la? je ni tangu lini hadi lini?
Naona hizi habari za kutoka kwenye kamati za bunge inabidi zihaririwe zana wa wahariri kabla hazijatoka ni very sensitive and detailed.Nikitumaini kuwa majority ya wahariri wana upeo
Je ile mikataba tulioizoea ya kuanzisha makampuni kijanja kwa dizaini za kukwepa kodi?
Anyway, habari si habari, japo lisemwalo hakika lipo.
 
Jamani kama huyu mama ambaye ni mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ndio sampuli ya wakurugenzi wa bodi zeti si tumekwisha?ikikumbukwa kuwa mkaguzi wa mahesabu ya Bot alisema kulikua na upungufu mkubwa wa uelewa na ufanisi wa kazi katika bodi uliochangia kutogundua mapema tatizo la Epa. Kazi ya bodi ni kusimamia na kurekebisha makosa ya management.TRA ni kuku wetu anaetaga mayai ya dhahabu tunahitaji bodi ya wakurugenzi makini.
 
angalia mzee kuna watu watailaumu ccm hata kwenye issue ya kodi hapa. au umewasahau!



Sasa unataka nani alaumiwe tupe mawazo yako. Wa kulaumiwa hapa ni nani?
Labda hufahamu serikali inavyofanya kazi na umeparamia tu hapa.
 
hawalipi kodi wanasponsor Ligi ya vodacom, miss tanzania na kujifanya wanagawa vyandarua vya vijimilioni kadhaa, kumbe wanatuhadaa wanatuibia huku wakitupaka mafuta kwa mgongo wa chupa eeh.Duh wanaujua kweli kuutumia msemo wa ukila na kipofu usimshike mkono.

Na coca cola nao ni cocacola company ipi? au zote? maana zipo nyingi, bonite bottlers, kwanza, au?
 
Waandishi wengine bwana, kichefuchefu tu. Huyu alishindwa kuelewa kilichozungumzwa akakurupuka na heading tu bila kujua aandike nini kuhusu hiyo heading.

Makampuni yote yaliyotajwa yanahudumiwa la Large Taxpayers Departrment ya TRA, maofisa wake wakienda pale TRA wanapokelewa kwa chai, soda na makaribisho mengine kama wateja wanaoheshimika. sasa iweje leo tuambiwe hawalipi kodi
 
Waandishi wengine bwana, kichefuchefu tu. Huyu alishindwa kuelewa kilichozungumzwa akakurupuka na heading tu bila kujua aandike nini kuhusu hiyo heading.

Makampuni yote yaliyotajwa yanahudumiwa la Large Taxpayers Departrment ya TRA, maofisa wake wakienda pale TRA wanapokelewa kwa chai, soda na makaribisho mengine kama wateja wanaoheshimika. sasa iweje leo tuambiwe hawalipi kodi

Kwa hiyo ukipewa chai na mkusanya kodi mana yake unalipa kodi?
 
Kuhani,

Chai haikuwa central issue kwnye point yangu hapo juu. The fact is hawa watu wanalipa kodi. Note that sio makampuni yote yanahudumiwa na Larget Taxpayers Department, ni lazima u-qualify kuwa large taxpayer, na moja ya criteria ni kiasi cha kodi unacholipa. kama kuna aina fulani ya kodi na mwanya unaotolewa na sheria ya kodi basi tuambiwe hivyo, na sio general statement ya "Hawalipi ikodi" ndio maana nilisema huyu mwandishi hakuelewa kitu gani kulikuwa kinaongelewa.
 
Je mwandishi huyo hayumo humu JF kutoa clarification?
Hata hivyo mimi nashangaa watu kumvaa mwandishi kwamba hajatoa true picture ya kile TRA wamesema. Sijui kwa nini watu wamewahi kumuhukumu hivi wakati yeye alikuwa anaripoti kile amesikia watu wa TRA wakisema. Wanaopinga uenda wanajua statement sahihi. Ebu watuapatie.
 

The fact is hawa watu wanalipa kodi.
Note that sio makampuni yote yanahudumiwa na Larget Taxpayers Department, ni lazima u-qualify kuwa large taxpayer, na moja ya criteria ni kiasi cha kodi unacholipa. kama kuna aina fulani ya kodi na mwanya unaotolewa na sheria ya kodi basi tuambiwe hivyo, na sio general statement ya "Hawalipi ikodi" ndio maana nilisema huyu mwandishi hakuelewa kitu gani kulikuwa kinaongelewa.

Mkuu, hiyo si kweli.

Tatizo lilikuwa kwamba aliyeleta hii habari hapa aliikata. Ukiisoma yote , kipande kilicho pigwa panga kinasema kwamba TRA wenyewe wamesema kuna makampuni yanabidi yachukuliwe hatua kwa kutokulipa kodi.

Coca-Cola yadaiwa hailipi kodi

Stella Nyemenohi
Daily News; Thursday,June 05, 2008 @09:06


KAMPUNI ya vinywaji baridi ya Coca Cola imetajwa kuwa miongoni mwa kampuni zisizolipa kodi.

Kutokana na hali hiyo, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewasilisha taarifa yake serikalini ili zichukuliwe hatua.

Taarifa hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Bodi ya TRA, Dk. Marcellina Chijoriga katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Fedha na Uchumi, baada ya baadhi ya wabunge kuhoji kuhusu taarifa kuwa baadhi ya kampuni hazilipi kodi.

Miongoni mwa wabunge hao, akiwamo Mbunge wa Kisarawe, Athuman Janguo (CCM) walitaka ufafanuzi kuhusu tetesi kuwa kampuni zote za simu za mkononi hazitozwi kodi ingawa zina mapato makubwa, jambo ambalo walisema siyo haki.

Akijibu, Chijoriga alizitaja kampuni kama vile Vodacom na Celtel kuwa zinalipa kiasi. “Wapo wengine ambao hawalipi kabisa,” alisema na kuongeza kuwa atazihifadhi majina kwa sasa.

Hata hivyo, baadhi ya wabunge, akiwamo Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF) ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, walimtaka ataje kwa kile walichomweleza kuwa analindwa na Kamati hiyo ya Bunge na ndipo akaitaja Kampuni ya Coca Cola kuwa ni miongoni.

Alisema kutokana na hali hiyo, amepeleka majina ya kampuni hizo ikiwamo Coca Cola kwa serikali ichukue hatua za kuzilazimisha kulipa kodi. Hata hivyo, hakutaja kampuni hiyo ya vinywaji baridi inadaiwa kiasi gani cha kodi.

ISHU YA SHERIA ZA MISAMAHA INAANZIA HAPA (article hiyo hiyo inaendelea)!


Wakati huo huo, serikali imeeleza kukerwa na misamaha ya kodi inayotolewa kwa taasisi mbalimbali na kushauri zitafutwe njia za kuipunguza kutokana na kile kilichoelezwa kupunguza wigo wa mapato.

Nayo TRA ilikiri kuwa ingawa misamaha hiyo ilikusudiwa kusaidia shughuli za jamii na kuhamasisha uwekezaji, lakini inamomonyoa wigo wa kutoza kodi na inazalisha mianya ya ukwepaji kodi.

Kauli hiyo ya TRA na Serikali, kupitia kwa Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Omar Yussuf Mzee, ilichangiwa na wabunge wengi wakitaka itolewe orodha ya kampuni zinazofaidika na pia kushauri sheria zinazoruhusu misamaha hiyo, zipitiwe upya na ikiwezekana, ziondolewe.

Mwenyekiti wa Bodi ya TRA. Marcellina Chijoriga alisema makusanyo halisi ya Idara ya Forodha, Bara, mwaka 2005/06 yalikuwa Sh bilioni 883.6 ambazo kati yake, Sh bilioni 385.5 sawa na asilimia 44, zilisamehewa. Pia mwaka 2006/07 makusanyo halisi Bara, yalikuwa Sh bilioni 1,132.4 na kati yake, Sh bilioni 390 sawa na asilimia 32, zilikuwa za msamaha wa kodi.

Katika kile kilichowashtua wabunge, ni takwimu kuhusu Zanzibar ambako ilionyeshwa kuwa mwaka 2006/07, kati ya Sh bilioni 20.4 zilizokusanywa, Sh 19.6 zilikuwa ni za msamaha.

“Hii inashtua. Zanzibar inakusanya bilioni 20, lakini bilioni 19 ni za msamaha. Hii kodi inamsaidiaje mwananchi? Tumejiandaa na hili kusimama kidete, tufahamu msamaha wa kodi unamsaidia mwananchi, mwekezaji au Serikali?” alisema Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF).

Mohamed ambaye ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni alisema lazima Bunge lichukue jukumu lake la kuhakikisha sheria zinazoruhusu misamaha hiyo zinapitiwa na kubaini kama zina ufanisi au la.

Kulingana na taarifa ya TRA, makundi yaliyopewa misamaha ya kodi Bara, ni wawekezaji binafsi chini ya TIC, taasisi za Serikali na Mashirika ya Umma, taasisi za dini na zisizo za serikali, miradi ya serikali na wengineo, ambavyo vyote kwa pamoja inafanya zifikie Sh bilioni 359.

http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?id=9473
______________________________


Kwa hiyo inamaanisha kuna ishu mbili tofauti:

1) yapo makampuni ambayo hayalipi kodi, na sio kwa sababu ya mianya au misamaha, bali wanavunja sheria. Vinginevyo TRA wasingesema wachukuliwe hatua.

2) ishu ya pili: sheria za misamaha zipo, lakini ni tofauti na kinachoongelewa kwenye ishu ya CocaCola, Vodacoma, na Celetel kutolipa kodi kama wanavyotakiwa.
 
Heshima Mbele,

Ndugu watanzania wenzangu,Nimeona leo niwape taarifa ya Jambo muhimu sana na kabla ya Bajeti ya Sayansi Kupita inabidi tushinikize Bei za simu zibake pale pale au zishuke chini zaidi ya hapo.Kwa taarifa nilizozipata kutoka Kampuni zote za simu,wameshaambiwa kuanzia wiki ijayo waanze kutumia Bei Mpya Za simu kwa sababu serikali imeanza kutoka kodi ya Excise Duty kwa watumiaji wa Simu.

CHIMBUKO LA KODI YENYEWE
Baada ya TCRA kushindwa kuwashawishi waheshimiwa wabunge watanzania waanze kulipa kodi kwa ajili ya matumizi ya televisheni.Wameamua kuhamishia kodi hiyo katika matumizi ya simu.Na wameweza kuongeza kodi kutoka asilimia 7 hadi asilimia 10 kabla ya VAT kwa kila Huduma ya simu.Na kwa kuwa bajeti ilishapita tuwe tayari kuyapokea haya.

Rejea hotuba ya waziri wa fedha akisoma bajeti iliyopita katika kipengele cha sheria ya ushuru wa bidhaa kipengele cha tatu
Kurekebisha kiwango cha ushuru wa bidhaa katika huduma za simu za mkononi kutoka asilimia 7 ya gharama ya matumizi ya huduma, hadi asilimia 10 ya gharama hiyo. Sababu kubwa ya rekebisho hili ni kwenda sanjari na mfumuko wa bei (adjustment forinflation);


zamani kodi hiyo ilikuwa ikilipwa na makampuni ya simu,ila kwa sasa makampuni haya yatakuwa yakipeleka asilimia 10 hiyo ambayo itakuwa ikilipwa na Mwananchi Serikalini ili kuongeza mapato


Gharama Mpya
Gharama Mpya za simu kwa sasa itakuwa sh 7.62 kwa sekunde ,yaani 460 kwa dakika kwenda mitandao mingine.Huduma hizi zitaenda na sanjari na kupanda kwa huduma za SMS ambapo kwa sasa SMS itakuwa zaidi ya sh. 60.ukiachilia mbali na huduma zingine zinazotelewa na kampuni hizo ,Maarufu kama VALUE ADDED SERVICE ambzo zitapanda mara dufu has huduma za Intrenet.(hapa nimeangalia kampuni za kawaida tu ikiachilia mbali kampuni ya VODACOM).

Mfano,Kama wewe unatumia mtandao wowote na matumizi yako ni wastani wa sh. 1000 kwa siku basi utakuwa unalipa kodi kati ya sh 234 hadi 250 kwa kila 1000. ambayo ungeweza kuongea kwa dk 5 kama ungekuwa Kenya.

MY TAKE
Ukiachilia Mbali watu wa kodi kukosa ubunifu ,wameshindwa kuongeza kodi kw awatu wa madini,wameshindwa kwa wauza magogo sasa wameamua kuwakamua wananchi zaidi.Je tuko Tayari??

kila siku wanasema maendeleo ya Mwafrika yatachangiw kwa kiasi kukubwa na ukuaji wa Mawasiliano,ambayo ni ukeli.Sasa kama serikali inaamua kupandisha kodi kwa sababu ya infalation.Je inatutendea haki??Je serikali inatusaidia wapi?

1.Mafuta kodi juu?
2.Chakula kimepanda bei..
3.Soda na yenye we juu..
4.maji nayo juu


Nchi Jirani Je
Yaani serikali inapunguza kodi huku inaongeza kule wewe unazani umepata afadhali.Siye mandondocha kweli..tumefurahi kupunguzwa kwa kodi katika Mishahara ila bado unaongezewa gharama za juu katika mawasiliano.

Kenya kwa sasa,Kampuni ya Safaricom imeweza kushusha bei za simu and Consumers who are using mobile in Kenya can now make calls for as little as KSh3 a minute between networks—the lowest in the country’s history of telephony. (ambayo ni sh 51Ksh kwa dakika) muda wote na wala siyo muda wa chombeza. na Ksh 15 (ambayo ni 255) kwenda mitandao mingine.

Naomba kuwasilisha na naombeni sana wabunge muwasaidie watanzania katika hili hata kama wao ni mandondocha.Waendelee kuzitoza kodi hizi kampuni tu..na wiki ijayo kodi hizi zitaanza kutumika rasmi.

Wenu ambaye siyo Ndondocha,
Gembe


 
Last edited by a moderator:
Duh! Duniani kote gharama za simu zinashuka sisi ndio tunazidi kuzipaisha tena!!? Wengine tutaachana na masimu ya mikononi, tunabaki na email tu basi, by the way tutaepusha mengi ah!
 
Back
Top Bottom