BANDOKITITA
JF-Expert Member
- Oct 4, 2022
- 1,177
- 2,281
Ninaandika kwa masikitiko makubwa sana. Chondechonde Mkurugenzi wa TCRA na Waziri mwenye dhamana (NAPE NAUYE) wananchi tumechoka na huu wizi na uhuni unaofanywa na kampuni za simu Tanzania.
Kwanza kabisa kampuni za simu hapa Tanzania wamekuwa wakituibia wateja kwa kutuunga kwenye huduma zinazohusisha makato kimyakimya bila ridhaa ya mteja. Kinachotokea ni kwamba Kama unasalio kwenye muda wa maongezi ukawa haujajiunga na kifurushi chochote huwa wanakata taratibu na hatimaye usipokuwa unaangalia salio halisi mara kwa mara utakuta kwenye akauti hakuna hata senti. Km umeweka vocha ili ujiunge na vufurushi ndani ya sekunde moja kabla ya kujiunga utakuta salio halitoshi (wameishakata). Ukiwapigia mfano HALOTEL wanajibu tu "ulijiunga na huduma x mwenyewe" ingali wewe hujawahi kuomba kujiunga na huduma hiyo. Huu siyo tu ni wizi bali ni utakatishaji fedha jambo ambalo ni hatari kwa uchumi wa nchi.
Pili, mbaya zaidi kuna baadhi ya mitandao ya SIMU Kama VODACOM kile kipengele cha huduma kwa wateja ambapo mteja alikuwa anapata furusa ya kuwasilisha malalamiko au shida zake wamekifuta kabisa. Hapo mwanzo ili uweze kuongea na mhudumu kwa wateja ilikuwa kazi sana kuwapata ila kwa sasa wamefuta kabisa hicho kipengele. Utapiga 💯 lakini huwezi kupata sehemu ya kuongea na mhudumu.
Swali ni kwa nini wanaondoa au kuficha kipengele cha huduma kwa wateja. Jibu ni lile lile ni kuendelea kutuibia wateja kupitia huduma zao hizi za hovyohovyo za lazima kwa kuwaunga wateja.
NB.
Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana (NAPE NAUYE) kwa nyakati tofauti na muda mrefu Watanzania wamekuwa wakizilalamikia hizi KAMPUNI za SIMU kwa wizi wao uliokithiri kupitia bando na huduma za hovyo ambazo mteja huungwa bila ridhaa yake. Wewe km Waziri mwenye dhamana umekuwa ukisema sisi wenyewe watumiaji ndiyo hatujui namna ya kutumia simu zetu vizuri hasa katika bando. Sasa nikwambie tu kuwa Watanzania wana akili timamu, siyo wajinga, ukiona wamelalamikia jambo ujue kuna vijimambo. Hizi kampuni za simu wana wizi mwingi wa rejareja na unaumiza sana. Fikiria Tanzania wapo watu wangapi wanaotumia simu na kila mmoja akatwe 50tsh kila siku km wanavyofanya sasa kwa mwezi ni shilingi ngapi.
Siyo tu tukemee huu uhuni bali km wameshindwa kutoa huduma kwa wananchi kihalali basi wafunge kampuni zao, Tanzania siyo shamba la Bibi, watu kuja kuvuna kadri watakavyo. Viongozi mliopewa dhamana wahurumieni wananchi wenu tena wenye umaskini uliopitiliza ambao wengi wao wanaishi chini ya dola moja kwa siku. Ebu fikiria jinsi maisha yalivyo ghali kwa sasa kuanzia mafuta, vyakula, ujenzi nk alafu kampuni sinakuja tena kuwaongeza maumivu kwa makato ya kimyakimya ya huduma za hovyohovyo ambazo mteja hajaomba.
Inaumiza sana.