Wilaya nzima (Bukoba Vijijini) Hakuna CHADEMA!

Ta Muganyizi, tatizo la aina hiyo haliko Bukoba Vijijini tu hata Muleba Kaskazini ni hivyo hivyo. Mimi natokea Kamachumu.Kule tangu Mzee Christopher Ngaiza afariki, pamekosekana kiongozi dhabiti wa CDM. No meetings held at all at least to addess the pressing issues of the day and get the wananchi there usher their opinions as how to resolve them. Haonekani mtu kule anaweza kuongea lugha ya wananchi na kuwapatia ufumbuzi. Kuna tatizo la over satisfaction ambalo Jenerali Ulimwengu aliwahi kulielezea kuwa Waafrika moja ya sifa tulokuwa nayo ni kulidhika kuliko pitiliza tena kwa mafanikio ya siku moja. Nina wasiwasi CDM wengi wasije wakalewa sifa za jumla za mikutanoni na kwenye maandamano na labda pengine wakafikiri kuwa kwa kuwa Dr.Slaa anafanya kazi mchana na usiku kukieneza chama basi nao watatbebwa na sifa hizo. Si hivyo, wale ambao are aspiring for leadership come 2015 wanatakiwa kufanya penetration to the masses. Walipo viongozi wa CDM amabao watapata kuona uzi huu kule Muleba Kaskazini tunaomba mbadala wa Balozi Ngaiza who did an excellent job worthy emulation. Mbali na kukijenga chama bali alenda mbali kwa kuetengeza ajira nyingi kupitia hotel-Kamachumu Inn, Kiwanda cha kutengeneza maji ya kunywa na bakery facility. Watu wengi waewekeza nje ya Kagera lakini aliona charity ianzie nyumbani. Namna ya kumwenzi ni kutupatia mtu mbadala

Ninachokiona kwako Bigaraone, ni kwamba Okalobela (hujaenda nyumbani muda mrefu, au huendi mara akwa mara). Hujui kinachoendelea kwa sasa hasa kwenye grassroot. Pia wachangiaji wengi wa mjadala huu wa Ta Muganyizi, ni cynics watupu. Wanaishi mtandaoni, hawajui kinachoendelea.
Wengine hawajui kwamba Opereshi Sangara ilikwenda Bukoba Januari- February 2011. Eti hakuna kiongozi mkuu aliyewaji kwemnda Bukoba! Hawajui kazi inayofanywa na Mbunge Conchesta Rwamlaza kujenga chama Bk Vijijini. Majuzi tu kafanya mikutano zaidi ya 10.
Hawajui kazi ya mwaka mzima iliyofanyika Muleba Kaskazini kuamsha chama. Eti hakuna hata mikutano. Kumbe hata mikutano ya John Heche hawajaiona! Hata Muleba Kusini, kwa mwezi mzima uliopita kuna kazi imefanywa, kwa udhamini wa Kashasira, anayelenga kugombea huko 2015.
Ni kweli vibrance ni ndogo, lakini kazi imeanza.
Pili, ni kweli Ngaiza alifanya kazi, lakini yeye alijenga jina lake zaidi kuliko Chadema. ndo maana alipokufa chama "kikafa", kama unavyodai. Nitakuletea picha baadaye uone jinsi ulivyosahau nyumbani.
 
Aisee dada Hoyce umenichekesha...sasa jamani hata Publicity hamna. Hongera sana kwa hizo information.Mimi niko hapa mjini nazungukia vijijini kila mara lakini huo moto siouoni.
 
Unatarajia kuona moto kama wa M4C ambayo haijafika? Au kama vile ni kipindi cha uchaguzi? Ulinzia mtandao wa chama hadi ngazi ya chini, ulinzia uelewa wa watu na maoni yao dhidi ya mbunge? Ulinzia maandalizi na shughuli za wanaotaka kuwania ubunge katika Jimbo, na mengine/...
 
Ta muganyizi yuko right, nshomile tumelala sanaaaana. Rwakatale amelewa majukumu ya kitaifa na kusahau kuwa charity begins at home. Wana Mleba trumeamua kujikomboa wenyewe bila hata kuomba msaada wa viongozi wa mkoa make hata ukifanya mawasiliano responses inakuwa negative. So jamani chonde chonde CHADEMA mkoa mnatuhaibisha
 
Ta Muganyizi, ndiyo maana baadhi ya wachangiaji hapa, akiwamo dada Hoyce wamesema kwamba baadhi yetu mnakuwa too cynic about practical political work done by Chadema. Na alilisitiza kwamba wengine mnajadili siasa za Bukoba kwa kutumia mtandao tu, hamwendi field. Mimi binafsi nipo Bukoba sasa, na ninajua kuwa miongoni mwa majimbo yaliyochangamka kisiasa kwa sasa ni Muleba Kaskazini, ambayo ssa imeambukiza Muleba Kusini, na maeneo mengine.

Kwa sasa siasa za Bukona hazimtegemei tena Lwakatare. Kazi kubwa inafanywa na Mbunge wa Viti Maalumu ambaye pia ni katibu wa mkoa, Concesta Rwamlaza. Kule Muleba Kaskazini sasa hivi mhimili wake ni Ansbert Ngurumo, yule mwandishi mwanaharakati wanayeandika Maswali Magumu kila Jumapili katika Tanzania Daima. Amefanya kazi kubwa sana kwa mwaka mzima, akafufua Chadema iliyokuwa imefifia kabisa baada ya kifo cha Balozo Ngaiza. Ametengeneza chama kwenye grassroot level, na katika maeneo mengi kimeanza kuonekana tishio. Mbunge wa kule, Charles Mwijage, tayari ameingiwa nan kiwewe, na sasa ameanza jitihada za kumdhulumu Ngurumo kwa vitimbi na mapandikizi kwenye Chadema.

Lakini mwezi uliopita, Ngurumo, ambaye BAVICHA jimboni waliomba awe mshauri wao, aliaandaa mikutano mitano ya hadhara katika maeneo tofauti jimbo zima, akamwalika John Heche (Mwenyekiti wa Bavicha Taifa). Mikutano ilichangamka kweli, na uhai wa Chadema unaonekana sasa. Na majimbo mengine yameanza kuiga kwa Muleba Kaskazini, sasa chama kinaanza kuamka.

Tatizo ni kwamba katika majimbo mengine, hawajitokezi watu wa aina ya Ngurumo wa kuanza kujenga chama mapema. Lakini yawezekana moto aliouwasha ngurumo utaamsha wengine nao waanze kazi mapema. Naamini kwamba baada ya 2014/15 Kagera haitakuwa ile ya sasa.

Kwa haya yaliyotokea kwenye uchaguzi wa madiwani, vi vema tusubiri tamko rasmi la Chadema, lakini hata kabla hawajatamka, sisi wengine tunajua mambo kadhaa. Kwa mfano:
1. Wapiga kura waliotumika niw ale wale wa mwaka 2010. NEC ilikataa kuandikisha wapiga kura wapya, hasa vijana ambao wakati ule walikuwa na mima 17-18, ambao ndio mashabiki wakuu wa Chadema sasa.

2. Waliojitokeza kupiga kura ni asilimia ndogo sana ya waliojiandikisha. Maeneo mengi ni asilimia 20-35. Hapo ni dhahiri kuna hujuma ya wazi ya kimfumo.

3. NEC imekataa kutangaza uchaguzi katika maeneo ambako Chadema kimeshafanya harakati za M4C. Ndiyo maana hata zile kata za madiwani wa Chadema wa Arusha waliofukuzwa, hazikufanya uchaguzi. Zipo zaidi ya kata 12 zimerukwa kwa sababu CCM ilijua kuwa katika maeneo ambako Chadema wamepita, haiwezi kuambulia kitu. Walifanya hivyo kuhadaa umma na kujidanganya kisaikolojia.

Hata hivyo, uchaguzi huu umekipa Chadema fursa ya kufika kule ambako kilikuwa hakijaenda. Idadi ya kura imeongezeka. Zaidi ya yote, kimebakiza viti vyake, na kimezoa vingine vya CCM. Chadema kimeongeza viti, CCM kimepoteza!
 
Mkuu Ta Muganyizi,

At times, though CHADEMA inaangaliwa kama chama cha kuikomboa Tanzania hasa kuisaidia kimaendeleo, we do overestimate it's power!!

Ingawa CHADEMA kina wabunge na viongozi wengine wengi makini, siamini na siko tayari kuamini kuwa viongozi wote wa CHAFEMA ni makini! Tunahitaji Tanzania yenye mabadiliko, regardless uko chama gani ukiwa mpenda maendeleo and above all MTAFUTAJI wa hayo maendeleo, uko katika familia hiyo.

So, maeneo mengine ambayo CHADEMA haijafika/kuonekana inawezekana wapo viongozi wengine(wa vyama vingine tofauti na CHADEMA) ambao kwa ushirikiano wanaweza kuifikisha Tanzania inayohitajika.

Pili, ukubali wa wananchi ukoje kwa Chama fulani?..kama wananchi wenyewe wako self motivated with different attitude(GOOD ATTITUDE) waweza kufika mahali fulani tunapohitaji..lakini kama wananchi kwa kiburi cha kuona wameridhika na hakuna haja ya mabadiliko ni ngumu kuwahamasisha hata kwa uamsho wowote ule!
 
Right km kuna kiongozi yeyote wa CDM angemfikishia rwakatare ujumbe huu make sina imani km rwakatare anaingiaga kwenye mtandao huu. This is constructive idea Ta muganyizi anataka tujenge kilicho chetu. Ila nimkosoe ofisi ya CDM haiko ijuganyondo bali iko Mtaa wa Kashabo hamgembe karibu ha hotel mpya ya sea breeze. ingawa muda mwingi hukaa imefungwa. Non- leaders wa CDM tunajitahidi kuomba support ktk kwa viongozi ili tuwe hata na mkutano wa wanachama wote kwa ajili ya kufaamiana na kuweka mikakati lkn wahusika hawatuuingi mkono. Jamani chondechonde tuamke
 
Ninachokiona kwako Bigaraone, ni kwamba Okalobela (hujaenda nyumbani muda mrefu, au huendi mara akwa mara). Hujui kinachoendelea kwa sasa hasa kwenye grassroot. Pia wachangiaji wengi wa mjadala huu wa Ta Muganyizi, ni cynics watupu. Wanaishi mtandaoni, hawajui kinachoendelea.
Wengine hawajui kwamba Opereshi Sangara ilikwenda Bukoba Januari- February 2011. Eti hakuna kiongozi mkuu aliyewaji kwemnda Bukoba! Hawajui kazi inayofanywa na Mbunge Conchesta Rwamlaza kujenga chama Bk Vijijini. Majuzi tu kafanya mikutano zaidi ya 10.
Hawajui kazi ya mwaka mzima iliyofanyika Muleba Kaskazini kuamsha chama. Eti hakuna hata mikutano. Kumbe hata mikutano ya John Heche hawajaiona! Hata Muleba Kusini, kwa mwezi mzima uliopita kuna kazi imefanywa, kwa udhamini wa Kashasira, anayelenga kugombea huko 2015.
Ni kweli vibrance ni ndogo, lakini kazi imeanza.
Pili, ni kweli Ngaiza alifanya kazi, lakini yeye alijenga jina lake zaidi kuliko Chadema. ndo maana alipokufa chama "kikafa", kama unavyodai. Nitakuletea picha baadaye uone jinsi ulivyosahau nyumbani.

Nashukuru sana Hoyce kuni brand kuwa Nkarobela lakini naona huku ni kufanya conclusion ambayo ni biased na haiko based kwenye findings. Kwa mara ya mwisho kuwa Kagera hasa wilaya sehemu ulizotaja ni mwezi 8 mwaka huu. Ingawa umejaribu kujiliwaza na haya ambayo yamefanyika lakini it's just a drop in an ocean of political and social problems. Hakuna aliyesema Operation Sangara haikwenda. Sawa ilienda but did it hatch into expected results? To no and if that is something to walk majestics it was and is abbortive struggle. Operation Sangara and other movements thereafter were supposed to bear fruits by putting party institutions in place na usingekuwa unatutajia mama mmoja mbunge ungekuwa unatutajia think tanks ambao CDM inawatumia kule na hawa wangekuwa wanaongea lugha ambayo watu wa kule wanapaswa kusikia-matatizo ya kilimo/zao la mgomba (staple food) that is now going extinct. Wabunge tena wengine mawaziri wamebaki wanakimbizana na majangiri uchwara huku wanaowafadhili wapo na tembo wanaendelea kuuawa.Badala ya kuunganisha nguvu na kuleta wataalamu waliomaliza SUA anvyuo vingine kuja kuangalia janga la mkoa wanabaki Dar es Salaam. Bei ndogo ya kahawa tena kwa kukopwa tatizo kubwa.Uharibifu wa mazingira nenda kaangalie kila open space imejaa pine tree and ecalyptus that are not envioronmental friendly. Miembe na miti mingine ya asili imekatwa halafu wanapanda miti inayoharibu vyanzo vya maji. Ziwa Victoria lilikuwa ni chanzo cha kipato kwa vijana wengi leu subutu uingize mguu utakiona. Kama kweli CDM ipo na operations ni consistent mbona hatusikii wana address matatizo haya? CCM na serikali wameshindwa na walishashindwa hata kabla ya matatizo haya sasa serikali mbadala iko wapi. Tunasema mambo haya Hoyce through observation, survey, discusion, interviews and regular follow up na sio kuwa tuna negative attitude. Tunatumwa na uzalendo na mapenzi yetu kwa CDM as the only way that can bring Tanzania back to its feet and to its previous glory. Kumbuka ktk research ya Uwezo kwa elimu kipimo shule za msingi za EAC save Rwanda and Burundi, Bukoba Vijijini is among the last three districts in Tanzania. Inahitaji kukombolewa na Bukoba was among the best region in yester days of Tanzania katika eneo la elimu. Hakuna mkombozi wala mbadala ni CDM ndio maana Ta Muganyizi analia na hali
 
Nimekusoma kaka yangu, KWELI, hata hizo ni siasa, lakini zimejikita zaidi katika uanaharakati wa mazingira. Hata hicho chama ambacho mleta hoja alikitaja kuwa ndicho kilichopo kwenye halmashauri ya Bukuba Rural, (pengine na Muleba na wilaya nyingine, hakijaadress mambo unayotaka wewe, na mnasema bado walau kinakubalika. Hata hivyo, nadhani hatujachelewa, tunaweza kuyaingiza taratibu, lakini si rahisi hayo yakawa ndo agenda kuu ya kumbeba mtu kisiasa.... Nilikuwa najaribu kukuwekea picha, naona mtandao wangu uko down, nikiweza nitakufanya hivyo.
 
Ta Muganyizi, usikatae. Rudia kusoma michango ya watu humu, utagundua kuwa YUPO aliyesema kwamba hakuna hata kiongozi mmoja wa juu aliyefika Bukoba, na ndiyo maana Hoyce akataja majina ya baadhi ya watu. Haimaanishi kwamba ndio pekee wanaofanya kazi hiyo, lakini alitaka kujibu hoja ya huyo cynic.

Vile vile, mwezi mzima ni muda mrefu sana katika siasa. Halafu lazima tujue hapa, hivi mnapozungumzia Chadema hawajafanya hiki au kile, mnatarajia watoke wapi hao Chadema? Hivi nyie mnaokaa humu mtandanoni kulalama, kila mmoja wenu amejiuliza aliwahi kuchangia jambo gani PHYSICALLY la kuleta hayo mabadiliko?

Hapo juu nimetoa majina ya baadhi ya wanaojihusisha na harakati za kujenga chama, watu ambao wamedhanikwamba maneno yanatosha, sasa ni wakati wa vitendo. Nadhani hii ndiyo njia pekee ya kuongeza nguvu kwa hao ambao wameshajitolea na wanaoendelea kujitosa. Ta Muganyizi, ondoka kwenye kompyuta. Njoo Bukoba tufanye kazi ya ukombozi!
 
Yaa Umenena jitihada zinahitajika,inabidi hao Viongozi wamanispaa wapige chachu hapo Bukoba vijijini ili waamke na kuwa na Viongozi wao.
 
Ta Muganyizi, usikatae. Rudia kusoma michango ya watu humu, utagundua kuwa YUPO aliyesema kwamba hakuna hata kiongozi mmoja wa juu aliyefika Bukoba, na ndiyo maana Hoyce akataja majina ya baadhi ya watu. Haimaanishi kwamba ndio pekee wanaofanya kazi hiyo, lakini alitaka kujibu hoja ya huyo cynic.

Vile vile, mwezi mzima ni muda mrefu sana katika siasa. Halafu lazima tujue hapa, hivi mnapozungumzia Chadema hawajafanya hiki au kile, mnatarajia watoke wapi hao Chadema? Hivi nyie mnaokaa humu mtandanoni kulalama, kila mmoja wenu amejiuliza aliwahi kuchangia jambo gani PHYSICALLY la kuleta hayo mabadiliko?

Hapo juu nimetoa majina ya baadhi ya wanaojihusisha na harakati za kujenga chama, watu ambao wamedhanikwamba maneno yanatosha, sasa ni wakati wa vitendo. Nadhani hii ndiyo njia pekee ya kuongeza nguvu kwa hao ambao wameshajitolea na wanaoendelea kujitosa. Ta Muganyizi, ondoka kwenye kompyuta. Njoo Bukoba tufanye kazi ya ukombozi!

Uko bukoba sehemu gani wewe mie naongea nikiwa Bukoba. Hadi naandika haya....nimetoka kijijini .....mie nilitarajia michango ya watu hapa ikanushe kuwa chadema Bukoba Kijijini chadema imejaa lakini aliyekanusha.
 
Ni vizuri ukaanza kujifunza siasa kwanza kabla ya kuja kupost humu JF, maana ulichoandika ni zaidi ya utumbo.
Kabla hujaliona jua mimi nilikuwa nimekaa darasani miaka minne nikisoma siasa na niliifanyia mtihani wa taifa na kufaulu vizuri,majibu yako ya product ya utumbo yapeleke huko huko mitaani kwenu Ubungo kama ulivyosema mwenyewe,
 
Pamoja na maneno mazuri ya faraja kuwa Tanzania karibia inakombolewa...bado napata mashaka na mbinu za Ukombozi tulizonazo. Huwezi Kuamini kinachoendelea katika baadhi ya Wilaya nchini.....ambapo yaani hata harufu ya CDM kuisikia ni kwa machale.

Nilibahatika kuingia katika kikao cha Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba (Rural) yenye kata 29 nilisikitika kuona kuwa kati ya hizo kata 29, kata 28 zinaongozwa na CCM na kata moja tu ya Katoro inaongozwa na CUF. Yaani hapa upinzani umeoneshwa na CUF pekee japokuwa bado na yenyewe haitoshi.

Wakati kikao kianendelea Viongozi wa Vyama vya upinzani walikuwa wanakribishwa kuhudhuria kikao hicho. Waliokaribishwa ni Viongozi wa CCM na CUF kwa siku ya kwanza. Siku ya Pili alihudhuria wa CCM na NCCR Mageuzi na CUF. Ikabidi niulize; imekuwaje NCCR Mageuzi wamefika hapa wakati hawana hata Kata moja? Jibu nililopewa ni kuwa "angalau NCCR wanaonekana as chama cha Upinzani, hata kama hawana kata hata moja wao ni "ACTIVE" maeneo haya. Baada ya hapo nikajiuliza inakuwa je Chama kinachopigiwa chapuo kuchukua nchi hakina jitihada yoyote ili kijihakikishie ushindi?

Nimewahi kusema hapa kuwa CDM hapa Bukoba mjini haionekani.......hatuoni initiative zozote za kukipromote chama. Viongozi wa Mkoa wako wapi? Niliwahi kusema Chama kama chama kiitishe mkutano wa wanachama wake kioneshe mpango kazi wake kama tatizo ni la ki budget wanachama wenyewe tujipange na kukiwezesha kuwafikia wananchi lakini wapi. Ofisi au Makao makuu naambiwa ni Ijuganyondo.....pembeni mwa mji. Hata kutoonekana kwa ofisi mjini ni udhaifu........

Tatizo nini? Inawezekana kuna wilaya Nyingine CDM haina hata kata moja!! Naomba tena Uongozi wa CDM ueleze kinaga ubaga nini mpango wake wa Kukiimarisha chama Mkoani Kagera .,....Hususan Wilaya Hii ya Bukoba? Siwezi kuwasemea wengine hapa nchini. Naomba anayeona kulegalega kwa CDM mahali pake aombe ufafanuzi kwa viongozi ili watoe majibu ya pamoja. Nisipojibiwa kwa hili siongei tena.

Nasuburi maelezo hapa........tumejiuliza wengi ...tunasubiri majibu na makakati.

Viongozi cdm makao makuu tunaomba hili swala liangaliwe kwa mapana na kupatiwa ufumbuzi hasa hapo kwenye RED

Huu ni ushahidi tosha kuwa cdm ni chama cha kidini, ukanda wa kaskazini na ukoo. CDM yaonekana mikoa ya kaskazini zaidi, huko bukoba wafuate nn mkuu, amka na chukua hatua yakujivua gwanda

Pamoja na vurumai zote za zanzibar na Dar hujaacha ukabila na udini.Ugumu wa maisha na watoto kukosa madarasa na madawati ya kusomea miaka 50 hii tangu tupate uhuru, haina cha ukanda wala udini. Waliotumiwa meseji hii wanajua ninachomaanisha.
 
Mkoa wa Kagera

1. Bukoba Mjini CDM ina madiwani 2, CDM iliongoza kura za urais
2. Bukoba Vijijini CDM haina Kiti hata kimoja cha Udiwani, Urais 50%
3. Nkenge CDM haina kiti hata kimoja, iliongoza kura za Urais
(hapa kati juzi juzi tu chadema ilishinda kiti cha serikali ya kijiji cha BULUFANI-Kyaka licha ya uchaguzi huo kusimamiwa na kuhailishwa mara kwa mara na vyombo vya DOLA.

Nenda kwenye takwimu za tume ya uchaguzi utaona ni mkoa/wilaya gani zilikuwa na upinzani mkubwa kama sio Kagera na CDM.

Utashangaa nenda vijijini bendera na ofisi za CDM zipo na watu wapo, serikali za vijiji naweza sema CDM imejiimarisha sana kuliko mikoa mingi.

CCM wanajua.

Mkoa unaoongoza kuwa na wakuu wa mikoa/wilaya wanajeshi.
 
Katibu wa Jimbo.JPG
Katibu wa Jimbo Muleba Kaskazini akihutubia umati wa watu Nyakatanga

Kagoma.JPG
John Heche akiwa Kata ya Kagoma

Kamachumu.JPG
John Heche akiwa Uwanja wa Polisi, Kamachumu

View attachment 70228
Baadhi ya wanachama wa CCM wakirejesha kadi, anayepiga makofi ni Ansbert Ngurumo anayefanya maandalizi ya kuwania ubunge wa Jimbo la Muleba Kaskazin.
 
Back
Top Bottom