Kigarama
JF-Expert Member
- Apr 23, 2007
- 2,492
- 1,230
kuna kisa kimoja cha kweli kabisa (lakini msikitungie Script) kinamhusu dada mmoja ninayemfahu.King'asti ubarikiwe sana haya mambo sijui lini watu watayaacha
Huyo dada baba yake alikufa yeye akiwa na miaka 13 na mama yake akiwa na miaka 27. Kwao walizaliwa watoto watatu yeye akiwa ni wa kwanza kuzaliwa. Baba yao alikuwa na wake wanne na mama yao alikuwa ni mama wa nyumbani anayetegemea kila kitu kutoka kwa baba yao. Siku ya kufa baba yao wao walikuwa wamepangishiwa nyumba kwa sababu mama yao alikuwa ni mke wa mwisho kuolewa kwa baba yao.
Kisa cha mama yao kuolewa na huyo baba ni kuwa alikwenda kutibiwa maradhi ya tumbo. Baada ya baba yao kufariki binti akiwa na miaka 13 na miezi kadhaa alianza kufanya biashara za kwenda minadani ambako alikutana na Tingo wa gari la mnadani na akiwa na miaka 14 na ushee akajifungua mtoto wake wa kwanza na kuhamia kwa huyo tingo. Tangu hapo ndipo mateso yalipoanza.
Akiwa na mimba ya mtoto wake wa pili aliwahi kupigwa kama mbwa na kutumbukizwa kwenye mfereji wa maji machafu mchana wa jua kali,kisa chenyewe eti mumewe alikuwa anamlazimisha awataje wapenzi wake wa zamani wakati kwa maelezo ya huyo binti jamaa ndiye aliiyefungua mlango wa "nyumba"
kuna wakati akiwa mjamzito alikuwa anashindia maji kwani jamaa alikuwa anasafiri hata kwa wiki mbili wakati siku ya kuondoka anajua ameacha buku mbili za matumizi lakini mwanamke akiomba hata maharage kwa jirani jamaa akijua hicho kipondo chake kama mwizi eti mwanamke anamdhalilisha na kumwaibisha.
Keshawahi kupasuliwa kichwani kwa chupa, mwilini ana mialama kibao ya kupigwa na kuchanwachanwa ama kwa kisu au viwembe. Jamii nzima inayowazunguka walifikia kuamini kwamba hayo ni mambo ya mapenzi ya watu wawili, Hata mwanamke apige kelele mara ngapi hakuna anayeingilia. mwanaume akaamini maisha ndiyo haya.
Siku moja jamaa karudi zake kutoka kwenye safari zake na nguo zake za Grease mwanamke kakaa kizingitini mwanaume akaanza kutuhumu "wewe jana umelala wapi? mwanamke kashangaa tuu "mbona mimi jana sikutoka kabisa kwenda popote tumbo lilikuwa linaniuma" jamaa kamwambia mwanamke aingie ndani. mwanamke katimua mbio, jamaa kufukuzia kwa nyuma hakumuona kumbe wasamaria wema wanawake wenzake wa jirani wamemficha chumbani kwao.Kaka mmoja mpangaji kwenye nyumba aliyokimbilia kuulizia na kuhadithiwa tukio zima akachukua jukumu la kumpangishia chumba siku hiyo hiyo na kumpa godoro na 100,000 ya kuanzia maisha.
miezi minne baadaye jamaa akaenda kumfanyia fujo kwenye nyumba ambayo amepanga na binti akaenda polisi jamaa akakamatwa na kuwekwa ndani. tangu siku hiyo adabu na heshima No fujo No kufuatiliana. Hatimaye binti kaolewa na bwana mwingine (siyo yule mpangaji) na sasa wana mtoto wa miaka 3 na wale aliozaa na yule bwana Bouncer wa kwanza mwenye miaka 19 yuko kwa baba yake na wa pili mwenye miaka 14 ni binti yuko kwa mama yake. Bouncer tangu waachane na huyu binti keshaoa na kuacha mara sita, Believe Me!!