Kigarama
JF-Expert Member
- Apr 23, 2007
- 2,492
- 1,230
visa vingi ninavyovijua pamoja na hicho nilichokisimulia kifundo chake ni kwamba familia nyingi zinajitengenezea mazingira ya kukataa kupokea watoto wao pindi wanapoolewa. Mtu akiolewa kwenye familia nyingine anaambiwa "Kitanda chako hapa hakipo tena" kwa hiyo akitendwa anajua kabisa nyumbani kwake ni pale alipoolewa au ukweni.Kwa kweli Chauro inasikitisha sana ni wachache sana wanaoweza kuelezea unyama wanaofanyiwa ndani ya ndoa wengi wao wamekuwa ni waoga sana wanaishi chini ya hicho kivuli huku wakiendelea kupigwa kila kukicha
Swala la umaskini si kweli kabisa kama linahusika kwenye tabia ya wanawake kuvumilia mateso toka kwa waume zao. bali makuzi yana mchango mkubwa sana. Binti tangu akiwa mtoto mdogo anatayarishwa kuoolewa, akipika chakula kimedoda anaambiwa "ukiolewa utampikia chakula kibaya mumeo. akikutana na Babu yake "Mchumba hujambo?" Akivunja ungo mama yake atamwambia "mwanangu umekuwa sasa jua iko siku utaolewa na kuniacha mama yako mkiwa" wakiwa na baba yake sebuleni mzee naye atafyatuka kimafumbo "Jane umepika chakula kizuri sana utakuwa mama mwema huko baadaye"
Yaani hatuwajengi binti zetu kufikiri kwamba wao wanaweza kuwa madaktari. mainjinia, wahandisi, waandishi nK, bali tunawajenga kwamba wao ni watu wa kuolewa na kuondoka nyumbani. Jamii yetu inaona ni sawa mtoto wa kiume akioa na kuishi na mkewe kwenye nyumba ya familia lakini hapo hapo mtoto wa kike akizalia nyumbani songombingo lake ni balaa.
Tatizo jingine ninaloliona ni kwamba wanawake wenyewe ni chanzo cha wanawake wenzao kunyanyasika. ushabiki unaoonyeshwa wanawake mwenzao anapoachana na mumewa unatisha. Wanaowacheka wanawake wanaoachana na waume zao si wanaume bali ni wanawake. Wakati mwingine mwanamke anavumilia kubaki kwa mume wake kwa sababu tu anataka kuwaonyesha wanawake wenzie kwamba nyumba haijamshinda.