Wema Sepetu adai kuwa mama yake amemtia aibu!

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931


Wema-akimuongoza-swahiba-wake-Omotola-kuelekea-kwenye-gari.jpg

Wema Isaac Sepetu na mama yake, Mariam Sepetu hawapo vizuri tangu yale mahojiano aliyoyafanya mzazi wake huyo runingani wiki mbili zilizopita akiwachana marafiki wa staa huyo mkubwa wa picha za Kibongo


Akizungumza na mtandao wa Global publisher katika mahojiano maalum juzi Alhamisi , Wema alisema kuwa hawezi kusahau siku mama yake alipofanya ‘intavyu' kwani aliposikia anaaza kutiririka ilibidi aipigie magoti runinga akiiomba inyamaze akidhani inamsikia.

"Kwanza sikuwepo wakati mama anafanya intavyu ‘so' sikutarajia kama angezungumza vitu vya namna ile.
"Ni kweli mama yangu kama mzazi alikuwa na kila sababu ya kunizungumzia, alikuwa na uchungu na mwanaye sawa! Lakini ‘mai mom' alipitiliza."



"Nadhani kuna vitu vilitakiwa kuondolewa kwa sababu mara baada ya kuzungumza, hali ilikuwa mbaya sana kuanzia kwenye mitandao ya kijamii na hata dada yangu alinipigia simu nikamweleza nilivyojisikia vibaya."


KANITIA AIBU!
"Nilijua mama kanitia aibu lakini nikajikaza kwa sababu utakumbuka ndo' kwanza nilikuwa kwenye maandalizi ya uzinduzi wa filamu yangu ya Super Star.


"Nilikaa kimya, nilijifanya kama hakuna kitu chochote kilichotokea lakini si unajua lazima moyo utakuuma tu hata kama ukijifanya kusahau.


"Baada ya kuona nipo kimya, siku iliyofuata alinitumia meseji mbaya na ninazo lakini hadi leo sikumjibu."



TUNAWEZA KUSEMA ALIKUDHALILISHA?
"Yaah…ukweli hali haikuwa nzuri. Meneja wangu Martin (Kadinda) alimpigia mama na kumsisitiza mwaliko niliokuwa nimempa wa kuhudhuria kwenye uzinduzi wa filamu yangu lakini amini usiamini mama yangu hakuhudhuria. Kwa upande wa baba naye hakufika lakini alinipa sababu za msingi kabisa nikamwelewa na pia alikuwa akifuatilia kila kitu kwa kuchati na dada yangu kwani alijua niko bize."



VIPI KUPELEKWA KWA WAGANGA?
"Sijui mama alipata wapi hiyo kitu ‘coz' sijawahi na wala sijui mambo ya waganga kama alivyozungumza yeye."



NISAMEHENI SANA
"Kwa yeyote aliyeguswa na mama kwa namna yoyote, naomba anisamehe sana."

http://freebongo.blogspot.com/2012/07/wema-sepetu-adai-kuwa-mama-yake-amemtia.html#_



 
haya mapya tena, mama na mwana hawaishiw drama, huyo wema angemchukuwa na mama yake kwenye izo filamu zake aigize naye maana naona anaweza sana.
 
Je mama ake alimwambia nini zaidi?? hebu aliye na news atukumbushe, maana mimi hili sakata lilinipita, nilikuwa pori!!!
 
wangemalizana wenyewe private,kwa vyovyote vile,yule ni mama yake.sio kila kitu mpitie kwenye media
 
Wema unamshushia mama yako heshima, usingepeleka kwa waandishi wa habari....
 
Wema muulize Kanumba yuko wapi sasa, keshaomba ubalozi wa nyumba kumi huko aliko naye alianza sokombingo kama hizi na mzazi wake.
 
So sad kwa Wema, alitakiwa amalizane na mamaye nyumbani si hadharani, angekubali yote tu jamii imuelewe hivi, lakini si kumsema mamaye, though huyu mama alikera sana.
 
Akimaliza hii drama, mama arudi aseme kuwa amesikitika kuwa mwanae kamkana. Yaani wasiiachie media ipumue, wera wera!
 
Akimaliza hii drama, mama arudi aseme kuwa amesikitika kuwa mwanae kamkana. Yaani wasiiachie media ipumue, wera wera!

bibi yake wema sijui yuko wapi,kuja kusema mama wema kamdhalilisha hakumfunda kutumia ushirikina kwa mjukuu wake..lol
 
haya mapya tena, mama na mwana hawaishiw drama, huyo wema angemchukuwa na mama yake kwenye izo filamu zake aigize naye maana naona anaweza sana.

Nashauri Mama kwenye movie awe Mganga....
Ili atuonyeshe jinsi ya kumtengeneza...
 
So sad kwa Wema, alitakiwa amalizane na mamaye nyumbani si hadharani, angekubali yote tu jamii imuelewe hivi, lakini si kumsema mamaye, though huyu mama alikera sana.

Hajamsema wala kumchamba...
Kamuanika tu mchana kweupeee...shuuuh
 
Back
Top Bottom