Wema Sepetu, nakushauri fanya maamuzi ya kuasili mtoto

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
17,446
21,140
Kiukweli miongoni mwa mambo ambayo anashauku nayo Wema Sepetu basi ni kupata mtoto.

Wema ameshajaribu kila namna kupata mtoto lakini anaambulia patupu zaidi na zaidi alichobakisha sasa hivi ni kungojea tu kudra za Mwenyezi Mungu aweze kumbariki na yeye siku moja aitwe mama.

Lakini kiuhalisi ni ngumu sana kwa yeye kupata ujauzito ,kwanza kitendo tu cha yeye kukata utumbo ili kutengeneza figure anayoitaka yeye ni sababu tosha kwa yeye kushika ujauzito pia lifestyle analoishi na vitu vileeeeeeee anavyotumia vinazidi kuleta ugumu kwa yeye kushika ujauzito .

Sasa kitu pekee ambacho nachoweza kumshauri ni kumuasili mtoto kisheria awe mtoto wake na hilo ni jambo la kawaida sana kwa mastaa ajaribu kuangalia hata mastaa wa nje ambao waliona hawataweza kupata watoto basi waliamua kuwaasili watoto na mpaka leo wanatambulika rasmi kama watoto wao.

Kama ni starehe Wema ameshakula sana ,sasa kilichobaki ni kulea maana umri unazidi kumtupa mkono kuendelea kuishi maisha ya kisichana kunamshushia brand yake kimtindo.

Uamuzi wa kuasili mtoto ndio utakuwa uamuzi sahihi zaidi kwake kuliko kuhangaika na hiko ki Manunu na kukichukulia kama binadamu

-369157417.jpg
 
Kuasili mtoto ni mchakato wenye changamoto zake. Hapa chini ni baadhi ya hatari zinazoweza kujitokeza katika mchakato huo:

Changamoto za Kihisia: Kuasili mtoto kunaweza kuwa na athari kihisia kwa wazazi wanaoasili na mtoto mwenyewe. Wazazi wanaweza kukabiliana na hisia za wasiwasi, hatia, au hofu ya kukosa uhusiano wa kina na mtoto wao.

Changamoto za Kimahusiano: Kuasili mtoto kunaweza kuathiri uhusiano wa familia na watu wa karibu. Familia inaweza kukabiliana na upinzani au kutokuwepo kwa uelewa kutoka kwa ndugu au marafiki.

Changamoto za Kisheria na Utawala: Mchakato wa kuasili mtoto unahitaji kukidhi taratibu za kisheria na utawala, ambazo zinaweza kuwa ngumu na kuchukua muda mrefu. Hii inaweza kusababisha usumbufu na wasiwasi kwa wazazi wanaotaka kuasili.

Changamoto za Kifedha: Kuasili mtoto kunahusisha gharama, pamoja na ada za kisheria, gharama za matibabu, na mahitaji ya kila siku ya mtoto. Hii inaweza kuwa mzigo wa kifedha kwa familia.

Changamoto za Kulea: Kuasili mtoto kunaweza kuja na changamoto za kulea na malezi. Kulea mtoto aliyeasiliwa kunaweza kuhitaji ustadi maalum, kujenga uhusiano wa kuaminiana, na kutatua masuala ambayo yanaweza kutokea kutokana na historia ya mtoto.
 
Mnavyosema kajaribu kila njia hajapata mtoto.

Je kanijaribu na mimi, isiwe anakutana na watu wana matatizo,
Mshauri aje kwangu asipopata ujauzito ndio tutaamini kweli ana mushkeli, hashiki mimba😂😂😂🤣🤣😂🤣🤣🤣
 
Ana kipato gani cha kuasili mtoto?

Mtoto wa kuasili bila kipato cha maana atakukimbia tuu...

Yani uniasili kisha ukanipigishe jua? Si bora nijirudie kwetu tuu?
Kwani mtoto anakula nini ambacho Wema atashindwa kukimudu?

Wema ana nyota ,inbox ya Wema madanga yamejaa yanapigana vikumbo.

Kama anaweza kulilea zee zima Whozu ndo ashindwe kummudu mtoto?
 
Kuasili mtoto ni mchakato wenye changamoto zake. Hapa chini ni baadhi ya hatari zinazoweza kujitokeza katika mchakato huo:

Changamoto za Kihisia: Kuasili mtoto kunaweza kuwa na athari kihisia kwa wazazi wanaoasili na mtoto mwenyewe. Wazazi wanaweza kukabiliana na hisia za wasiwasi, hatia, au hofu ya kukosa uhusiano wa kina na mtoto wao.

Changamoto za Kimahusiano: Kuasili mtoto kunaweza kuathiri uhusiano wa familia na watu wa karibu. Familia inaweza kukabiliana na upinzani au kutokuwepo kwa uelewa kutoka kwa ndugu au marafiki.

Changamoto za Kisheria na Utawala: Mchakato wa kuasili mtoto unahitaji kukidhi taratibu za kisheria na utawala, ambazo zinaweza kuwa ngumu na kuchukua muda mrefu. Hii inaweza kusababisha usumbufu na wasiwasi kwa wazazi wanaotaka kuasili.

Changamoto za Kifedha: Kuasili mtoto kunahusisha gharama, pamoja na ada za kisheria, gharama za matibabu, na mahitaji ya kila siku ya mtoto. Hii inaweza kuwa mzigo wa kifedha kwa familia.

Changamoto za Kulea: Kuasili mtoto kunaweza kuja na changamoto za kulea na malezi. Kulea mtoto aliyeasiliwa kunaweza kuhitaji ustadi maalum, kujenga uhusiano wa kuaminiana, na kutatua masuala ambayo yanaweza kutokea kutokana na historia ya mtoto.
Watoto yatima kibao wamejaa,sio lazima kuasili mtoto mwenye wazazi wake .
 
Back
Top Bottom