Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako afuta posho za kusahisha mitihani ya Mock na NECTA

Nauli ya kwenda na kurudi utapatiwa mwalimu. Pia naomba ufahamu kuwa serikali imeamua kubana matumizi na kupeleka pesa itakayopatikana kwenye miradi yaa maendeleo. Naomba tuwe wavumilivu na tuunge mkono nia njema ya serikali yetu. Naomba ifahamike kuwa nia na malengo ya serikali mema kabisa. Inachofanya serikali si yo ukatili kama baadhi yenu mnavyofikiria. Serikali inataka kila mtanzania afaidike na matunda ya serikali yake. Wakati utaongea. Mtayaona hayo matunda kwa macho yenu. Asanteni.
Dah we ndo huna point kabisa ndugu yaani posho za watu kufanya kazi zao nazo wanyimwe coz ya kubana matumizi vipi hao wabunge wanaolipana posho ile sio kazi yao? ebu tujaribu kuwaza tuache uvivu
 
Mtu anaeunga mkono kufutwa hiyo posho kwa mwalimu sijui anajisikiaje.
Apigie kelele kwanza wabunge wasilipwe hata senti tano ya vikao vya bunge cz ni sehemu ya kazi yao pia. Akifanikisha hilo aje ujumbe wake hapa!
 
Hiyo mitihani wawe wanapewa wakiwa kwenye vituo vyao vya kazi ili waisahihishe hapo itakuwa sawa kuwanyima posho, ila kuwatoa kituo cha kazi kwenda kingine bila malipo, hata huyu Ndalichako nae anakuwa na uprofesa kama wa lipumba, sio fare kabisa.
 
ndalichako hapo umezingua na hii ni kwasababu mlikurupuka kuchukua sera ya ukawa ya elimu bure pasipokujipanga kwasbb hela ya kusahisha mitihani ilikua inachangwa na wanafunz wa vidato vya mitihani sasa mda wa walimu kwenda kusahisha umefka hamna hela ndo mnahamua kuja na ajenda hii
 
Tanzania mpya lazima ipatikane tu...

hiii awamu ina balaaa sana na ina dhamira ya dhati kusuka nchiiii
Kweli kabisa,serikali ya awamu ya 5 ina nia ya dhati ya kuwaboreshea walimu maslahi yao.Acheni uchochezi.
Huu ni mwanzo tu wa neema kwa walimu.
 
dah sasa sisi tuliopo vyuoni tunasoma ualimu tunaona bora kuacha tu iv ayo maamuz anaamua tu au vipi? km vipi wafute posho zote hata wabunge ikiwezekana hata wao wafutiwe posho...dah jk kikwete alisema mtanikumbuka kweli tumekumic sana kikwete
 
Hiyo mitihani wawe wanapewa wakiwa kwenye vituo vyao vya kazi ili waisahihishe hapo itakuwa sawa kuwanyima posho, ila kuwatoa kituo cha kazi kwenda kingine bila malipo, hata huyu Ndalichako nae anakuwa na uprofesa kama wa lipumba, sio fare kabisa.
Hata wakisahihishia vyumbani mwao bado watapaswa walipwe!
 
Nikilazimishwa Kwenda marking wanafunzi watanitambua ukiandika 5 inayofanana na 3 siangalii Mara mbili, spelling mistakes sitavumilia Dawa ya moto.......
 
Nauli ya kwenda na kurudi utapatiwa mwalimu. Pia naomba ufahamu kuwa serikali imeamua kubana matumizi na kupeleka pesa itakayopatikana kwenye miradi yaa maendeleo. Naomba tuwe wavumilivu na tuunge mkono nia njema ya serikali yetu. Naomba ifahamike kuwa nia na malengo ya serikali mema kabisa. Inachofanya serikali si yo ukatili kama baadhi yenu mnavyofikiria. Serikali inataka kila mtanzania afaidike na matunda ya serikali yake. Wakati utaongea. Mtayaona hayo matunda kwa macho yenu. Asanteni.
Mmmmh, sidhani kama mtafika kwa kuondoa vitu muhimu. Ningewaona mnajali kama serikali na BUNGE mge-review posho na mishahara ya wabunge, mishahara na posho za mawaziri, makatibu wakuu, wakurugenzi mashirika ya umma na serikalini. Vyombo vyao vya usafiri na running costs zao, makazi nk. Huko ndiko kwenye matumizi makubwa ya kutisha na yenye impact kubwa kwa walala hoi. Vinginevyo kukwepa kutekeleza hayo kama rais alivyo wahi kuahidi kushusha mishahara ya wakurungenzi nk, ni kutotimiza si tu wajibu wenu bali kutotimiza hata yale yanayo toka vinywani mwenu.....
 
Back
Top Bottom