DAFU NA NDIMU
JF-Expert Member
- Aug 20, 2016
- 3,497
- 5,088
Asante mkuu kwa mawazo kuntu. Shida ya serikali hii elimu bure inawapa kiungulia. Wanaacha kutafuta vyanzo mbadala vya hela wanabaki kuondoa pesa za mambo ya msingi.Ukienda kwenye hii kazi maalum una haki ya kulipiwa nauli na kulipwa hela ya kujikimu. Hili nafikiri halina mjadala na sidhani kama hii ndio posho anayo ongea Ndalichako vinginevyo sitamuelewa. Utata unakuja kwenye ile kazi maalum ya kusahihisha-je inastahili mtu alipwe posho au la? Kwa hili nafikiri serikali iwe na msimamo mmoja juu ya aina za kazi zinazo stahili posho. Na pia kuna vyuo vingine (siyo mitihani ya kitaifa walimu/lecturers hulipwa mzigo ukipita uzito fulani). Mitihani ya kitaifa ni jukumu la NECTA na sidhani kama ni jukumu ambalo kila mwalimu anategemewa kulibeba kama mitihani ya kawaida-kama ni mzigo wa ziada wanastahili posho hili linaongoleka. Mshahara wa mwalimu haukupangwa na hili (kusahihisha mitihani ya taifa) likiwa limezingatiwa. On the other hand wabunge (akiwemo waziri) wanalipwa kwa kufanya kazi yao na sio kazi maalum.
They'll have to count me out.