sulphadoxine
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 2,257
- 645
Tutafika tu tuendakooooooooooooooooo
Mtowa mada anapima joto, si muende BRELA tu mkapate official search! Nawashangaa, wakati vitu vipo wazi!
mi naona kama tunachelewa hii MIJIZI inamaliza nchi!Tutafika tu tuendakooooooooooooooooo
Wadau,
Sidhani kama anachokizungumza Sitta kinaweza kukubalika kwa Watanzania walio wengi. Ni abiria anayesafiri kwenye meli ya ufisadi. Hivyo ndivyo ninavyoamini mimi.Dhana ya kuwa na chakula kisafi kwenye sahani chafu huenda sambamba na mtazamo wa kuendelea kupiga kelele kwenye boti linalozama badala ya kutafuta njia ya kujiokoa. Sitta yupo ndani ya mfumo huu kwa muda mrefu na anajua wazi mambo yanavyofanyika. Nina wasiwasi na tamko lake. Yawezekana ni kutaka kutuchanganya wananchi tuliopoteza matumaini ya maisha haya na kumtafuta hata malaika mmoja anayeweza kutuvuta mkono. Tunamkubali kwa kudhani kuwa Sitta ni mkombozi aliyedondoka kwa ajili ya kutubadilishia mfumo wa maisha tunayoyalilia. Hizo ni mbwembwe tu,hana nafasi ya kufanya maamuzi. Analeta propaganda kwa kuwa naye ana machungu yake mengi aliyoyabeba moyoni. Tunapaswa kujiuliza: Je, kelele za Dowans na Richmond zimeanza leo? Alikuwa wapi siku zote?
Kila nikiona Mtanzania mwenzangu anatoa such comments...... Huwa nakata tamaa kabisa, na kuona Safari bado ni ndefu sana... Na huenda hatutafika in any near future
Mkerio unasema Mh. Sitta ni mzalendo!!!
Sijui, binafsi sina uhakika!! Ila ningependa kukutahadhalisha kuwa tegemea kuona mengi sana kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015. Viongozi watakuja kwa sura za hadaa ili mradi wajitengenezee mazingira ya kuteuliwa kugombea Urais come 2015.
Jiulize yule yule Sitta aliyeizima na kuizika hoja ya Richmond (Dowarns) bungeni (tena akiwa na nguvu zaidi kama Spika wa Bunge la JMT leo anatoa nguvu wapi ya kusema Dowans ni ya Mafisadi wa Tanzania?
Nilitegemea kipindi kile akiwa Spika wa Bunge ndo alikuwa well placed kuonyesha uzalendo wake kwa Tanzania.
Kinyume na hapo........namuona msanii na mtu anayetafuta cheap populality mbele ya macho ya wadanganyika!!
Kwenye ile kesi ya CityWater na DAWASA kwenye mahakama hiyohiyo, DAWASA ilishinda na wakili alikuwa ni huyohuyo. Alilipwa over 5bn. Mara hii kwenye DOWANS/TANESCO, TANESCO imeshindwa. Anaijua sana mahakama ile.