Siasa za CCM ndio zinapelekea tatizo la Umeme lisiishe nchini

Feb 3, 2023
52
25
Siasa za CCM ndio zinapelekea tatizo la Umeme nchini lisiishe kwani maamuzi makubwa na ya kitaalamu yanaamriwa kisasa, na mpaka sasa CCM hawajawahi na hawatawahi kumaliza kabisa tatizo la umeme.

Ukiangalia kwa makini maamuzi makubwa na ya kitaalamu yaliyoamriwa kisiasa ni pale miaka ya 90 CCM walipoamua kuruhusu wazalishaji binafsi (Independent power producer) kuzalisha umeme na kuiuzia TANESCO kwa bei kubwa kuliko na kusababisha Shirika hilo kuyumba na kushindwa kukarabati miundombinu yake baadhi ya makampuni yaliyoingia kwenye Siasa hizo za CCM ni IPTL, RICHMOND, DOWANS nk, Siasa zilizohusishwa na kashfa ya Rushwa ndani ya CCM na Serikali yake na kupelekea aliyekuwa Waziri Mkuu wa wakati huo kujiuzuru kwa kashfa ya Rushwa.

Kufanikisha kuondoa au kupunguza kukatika katika kwa umeme na kwenda kwenye viwango vya kimataifa vya kukatika kwa umeme kusizidi mara nne kwa mwaka ni kuliondolea mzigo mzito Shirika la TANESCO kwa kuligawa Shirika hilo katika makampuni/Mashirika mengine kuligana na majukumu ya kazi zao kama;

1) Uzalishaji wa umeme
2) Usambazaji wa umeme
3) Ugavi wa umeme kwa watumiaji
4) Uchoraji ukarabati ujenzi wa miundo mbinu mikubwa ya umme na sio kulibinafsisha

TANESCO wabaki na usambazaji wa Umeme majumbani lakini pia TANESCO iweze kushitakiwa mahakamani kwa;

1) Kuchukua hela za mteja bila huduma ya uhakika
2) Hasara wanazopata wateja kwenye kadhia ya kukatika kwa umeme mara kwa mara hii itaongeza umakini na uzalendo kwa Shirika.
 
Back
Top Bottom