Waziri Mkuu kukutana na madaktari kesho

Mkuu upo sawa kabisa, wananchi tunaandaliwa kisaikolojia na maamuzi yatakayofuatia. Na wakifukuzwa hata yale wanayodaiyanakuwa yamepotea kimyakimya, badala yake wakae wakubaliane sasa. Huu mgomo uwe ndio baseline, wawape mda kama hawajatimiza wanajua walipoishia mara ya mwisho, wakifukuzwa maana nzima ya kugoma inapotea

Nimesoma wadau wengi wakiongelea hii option ya kuwafukuza madaktari ila haiingii kichwani mwangu.

Kwani baada ya kuwafukuza wanategemea kupata wengine kutoka wapi??
 
Kinachofanyika sasa ni maandalizi ya maamuzi magumu!!!,taarifa toka ofisi ya waziri mkuu inaonyesha kuwa tatizo ni madaktari na kunapost nilichangia kuwa madaktari wamejiandaaje wakizuiwa hiyo mikutano yao??sidhani kama hiyo kesho muafaka ukikwama kama watawaruhusu kukutana,hilo waliweke vichwani mwao,na hii itakuwa ni mbinu ya mwisho ya serikali wakiweza hapa serikali lazima inyanyue mikono,madaktari wakae wakijua kuwa mpaka sasa serikali haijakubali kuburuzwa.
 
wizara ya afya ifumuliwe hilo ni dai la kwanza na dai muhimu

Mkuu umenena, nilitegemea barua ya madai yetu ikiwemo hilo na uboreshaji Wa huduma kama wagonjwa kulala chini
Na hospitali nyingine Kama ya mkoa Kilimanjaro kutokuwa na chumba cha upasuaji zaidi ya mwaka sasa wananchi wanateseka, posho oncall na housing. Hao wanatakiwa kuachia
 
wizara ya afya ifumuliwe hilo ni dai la kwanza na dai muhimu

Mkuu umenena, nilitegemea barua ya madai yetu ikiwemo hilo na uboreshaji Wa huduma kama wagonjwa kulala chini
Na hospitali nyingine Kama ya mkoa Kilimanjaro kutokuwa na chumba cha upasuaji zaidi ya mwaka sasa wananchi wanateseka, posho oncall na housing. Hao wanatakiwa kuachia ngazi iwe amewawajibisha ndo aje kutuona
 
Mimi nadhani wapewe pesa zao .Pesa zipo sana .JK yuko juu anatanua , wabunge ni Pinda kapitisha posho zao leo iweke madaktari wakose posho zao .No way acheni mchezo hakika wepeni pesa jamaa warudi kazini .
Mkuu Lunyungu, kwa hiyo hao madaktari wapewe tuu just like that?!. Then wakifuatia walimu, then watumishi wa umma jee serikali yetu inauwezo huo?!.
 
Mkuu Lunyungu, kwa hiyo hao madaktari wapewe tuu just like that?!. Then wakifuatia walimu, then watumishi wa umma jee serikali yetu inauwezo huo?!.

Kwa wewe unashauri wasipewe maslahi bora kwa sababu walimu, na watumishi wengine nao watagoma?

Kwa nini usiwashauri wakatoa kwa watumishi wote ku-harmonize mishahara ya watumishi wa umma??
 
Mpaka PM atakapo zungumza nao itakuwa ni saa 36 ndani ya uvumilivu wa serikali kwa mgomo wao!. Mwisho wa uvumilivu ni saa 48!. Wanajf tuungane kuwabembeleza madaktari wamsikilize Waziri Mkuu na akiwaangukia wamkubalie warudi kazini!. Jumatatu patakuwa hapatoshi!.

Mkuu mbona saa 48 zimeshapita sana au wewe unahesabu siku ni saa 6!!!????????????
 
Yes PM anawahi makubaliano kabla ya J3 wauguzi wasije goma. Vema, kwani wakigoma ngoma itakuwa nzito kwa serikali.

Illi tujue hakuna unafiki kwenu msirudi kazini kama serikali haija overhaul wizara yenu kama mlivyodai. Waziri, Katibu Mkuu na Mganga mkuu OUT.

Onyesheni njia sisi tupo nyuma yenu.

lakini fahamuni atawabembeleza na kuwatisha. Hii ni serikali leglege ni sawa nakupigana na mwoga bwana atakutisha atachukua kitu chochote kukupiga nacho wakati yupo mguu sawa kukimbia. Sitashangaa wakileta polisi na silaha ya kilaaina au wakiwaweka standby.

Nitatunga wimbo kwaheri serikali yangu leglege
 
Mkuu Lunyungu, kwa hiyo hao madaktari wapewe tuu just like that?!. Then wakifuatia walimu, then watumishi wa umma jee serikali yetu inauwezo huo?!.

Nadhani madaktari wawachukia kwa kuwa hukufanikiwa kuwa daktari. Kuna wakati huwa sielewi rangi yako.
 
Wasipokubali unafikiri ni nini kitafuata? amini usiamini, PM atawaambia serikali itayafanyia kazi madai yao, sioni jibu la tofauti. Madai mengi ni ya kisera zaidi na yanahusu na watumishi wengine pia. Huwezi kuongeza mishahara kiholela bila kuamsha madai kwingine. Mimi ningewashauri wakubaliane naye kuwa baada ya miezi 4-6 wanatarajia kuona utofauti katika yale wanayodai. Migomo ni migumu kuisustain kwa sababu ya tofauti nyingi zilizopo kati ya wagomaji, kuna wengine kati ya madaktari wameshachoka sasa wanatamani tu kurudi kazini, kuna wengine bado ari iko juu. Subiri uone baada ya kesho watakavyogawanyika.

Wakimkatalia PM tu wataambiwa wanaokubaliana na serikali warudi kazini wasiokubali waendelee kugoma. Waziri mkuu ndio serikali yenyewe na wanatakiwa walitambue hilo. Wakipewa option hizo mbili mgomo ndio umekwisha hivyo. Wawe wastaarabu na kukubaliana deal fulani na PM then waendelee kufuatilia kwa ukaribu, kama Ulimboka unasoma hii msg nafikiri utanielewa what to do. PM hawezi kumfukuza waziri au secretary wa wizara kienyeji enyeji, lazima wamlinde na kumuondoa ili kuondoa taswira ya kushinikizwa. Ni hilo tu.
Mkuu huo ndio ukweli hata kama watu hawataki. Mambo mengi ni ya kisera.
 
Mkuu Lunyungu, kwa hiyo hao madaktari wapewe tuu just like that?!. Then wakifuatia walimu, then watumishi wa umma jee serikali yetu inauwezo huo?!.
Serikali inalijua hilo. Ikikubali itakuwa ndio mwanzo wa mwisho wake.
 
Madaktari walianza game vizuri lakini wanaonekana kuboronga sasa. PM ndio serikali, akiwaita ukumbi fulani wakikataa ni kosa, hawawezi kumpangia kamwe, yeye ndio serikali sasa wamelewa sifa wanafikiri serikali itaendelea kuvumulia! watatimuliwa wote tusubiri tu, sasa hivi wanatakiwa kuwa na hekima zaidi kuliko kusukumwa na mob psychology.

duh! do you mean doctors act by mob psychology??
mh! hayawe yawezekana wewe wajua sana psychology kuliko wao, ongera.
 
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda kesho (Jumapili, Januari 29, 2012) atakutana na madaktari waliofanya mgomo kwenye ukumbi wa Karimjee kuanzia saa 4:00 asubuhi.

Madaktari hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wanaomba kuonana na Waziri Mkuu na mara zote Waziri Mkuu amekubali kuonana nao lakini hawakutokea. Pamoja na kukubali huko kwa Waziri Mkuu, tarehe 25 Januari 2012 katika Mkutano wake na Wahariri wa Vyombo vya Habari aliwaomba Madaktari kuwa alikuwa tayari kuonana nao lakini hawakutokea.

Ili kuendeleza jitihada za kutaka kuonana na madaktari hao, Waziri Mkuu alituma Uongozi wa Serikali ukiongozwa na Mawaziri wa Afya na Ustawi wa Jamii; na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kuonana na Madaktari kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Starlight tarehe 27 Januari 2012. Kwenye Mkutano huo madaktari waliwasilisha malalamiko yao na kuomba kuonana na Waziri Mkuu. Kufuatia maombi hayo, Waziri Mkuu amewaandikia madaktari hao barua ya kuwataka kuonana nao Kesho, tarehe 29 Januari 2012 kwenye Ukumbi wa Karimjee, saa 4:00 asubuhi.

Kabla ya kufikia uamuzi huo, kulikuwa na mawasiliano kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Uongozi wa Medical Association of Tanzania (MAT) na baadaye Mwenyekiti wa Muda wa Kamati ya Madaktari kuhusu mgomo wa Madaktari unaoendelea.

Aidha, Viongozi mbalimbali wa Serikali wamefanya mazungumzo na Wawakilishi wa Madaktari na Madaktari wenyewe kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Starlight ili kuweza kupata ufumbuzi wa matatizo yaliyowasilishwa Ofisi ya Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu anawasihi Madaktari wote kuhudhuria mkutano.


IMETOLEWA NA:
OFISI YAWAZIRI MKUU
SLP 3021,
DAR ES SALAAM
JUMAMOSI, JANUARI 28, 2012

Wale waliosema serikali ya Tz ni legele wala hakukosea, wantazania wameteseka wiki nzima kwa kukosa huduma kwa ajili ya madaktari kugoma , badala ya kuchukua hatua mapema kiongozi mkuu anaamua kupima upepo kwanza. kuwachunia madaktari kukutana nao sikuzote maana yake ilikuwa nini?
 
Nimesoma wadau wengi wakiongelea hii option ya kuwafukuza madaktari ila haiingii kichwani mwangu.

Kwani baada ya kuwafukuza wanategemea kupata wengine kutoka wapi??
Mkuu tunaweza kwenda kumuomba Raul akatuletea Madaktari toka Cuba!
 
Hiyo taarifa haina ukweli wowote Invisible. Si kweli kuwa madaktari hawakwenda kuonana na Pinda alipowahitaji, Invisible una uhakika ni lini madaktari waliitwa wakagoma kwenda? hizo ni propaganda za wanasiasa, watu wasio na huruma na wananchi. Madaktar kwa muda wot huo wamekuwa wakiwaomba watawala waje kwenye vikao vyao na kujibu hoja zao lakini viongozi hao kuanzia kwa waziri wa afya na pinda mwenyewe walikuwa wakikimbilia kwenye vyombo vya habari. Hivi Madaktari wana hoja na wako kwenye ukumbi wewe unawakimbia unawaita waandishi wa habari na kuwaomba wakatibu wagonjwa wakati unajua hawana taaluma hiyo.
Huo mkutano wa kesho ni batili kwasababu madaktari wako kwenye vikao vyao na wamemwita Pinda star light yeye amekodi ukumbi wake wa Karimjee, mmmh, siasa noma!!!!!
Mkuu nadhani hii ni taarifa y ofisi y waziri mkuu na si habari ya invisible.

Naona madaktari wanakosa hekima. Kwani wakienda Karimjee kuna tatizo gani? Ingekuwa mkutano unafanyika Muhimbili sawa ila madaktari wanalazimisha ati waziri mkuu aende Star light. Nendeni mkamsikilize huko Karimjee
 
Mkuu tunaweza kwenda kumuomba Raul akatuletea Madaktari toka Cuba!


Atakuwa ametupa samaki au nyavu tukavue wenyewe??

Hata hivyo najuwa Watanzania wengi na serikali yao wana mtazamo kama huo...Serikali haiwezi kupingwa kwa lolote na wala haiwezi kushindwa kitu!!

Watakapogundua kinyume chake it will be really too late!!
 
Mkuu nadhani hii ni taarifa y ofisi y waziri mkuu na si habari ya invisible.

Naona madaktari wanakosa hekima. Kwani wakienda Karimjee kuna tatizo gani? Ingekuwa mkutano unafanyika Muhimbili sawa ila madaktari wanalazimisha ati waziri mkuu aende Star light. Nendeni mkamsikilize huko Karimjee

Na yeye PM alikuwa wapi siku zote??
 
Atakuwa ametupa samaki au nyavu tukavue wenyewe??

Hata hivyo najuwa Watanzania wengi na serikali yao wana mtazamo kama huo...Serikali haiwezi kupingwa kwa lolote na wala haiwezi kushindwa kitu!!

Watakapogundua kinyume chake it will be really too late!!
Atakuwa ametupatia samaki tule wakati tunaandaa nyavu!
 
Back
Top Bottom