nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
14 March 2011
BARAZA la Wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shinyanga Mjini, limemshukia Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibroad Slaa kwa madai kuwa anaudanganya umma wa Watanzania.
Pia, limesema hatua yake ya kumzushia kifo mbele ya mkutano wa hadhara Mkuu wa mkoa Shinyanga, Dk. Yohana Balele, ilikuwa na lengo la kuwachanganya na kuwadhoofisha wananchi.
Baraza hilo la wazee limesema siasa za kuwazushia vifo viongozi wanaohehishimika mbele ya jamii, zimepitwa na wakati na kwamba, ni sawa na siasa za majitaka.
"Tunalaani uzushi wa Dk. Slaa wa kudai kuwa Dk. Balele amefariki wakati siyo kweli, Chadema na viongozi wake wafanye siasa safi na waache siasa chafu," lilisema tamko la wazee hao.
Mbali na kumshukia Dk. Slaa, Baraza hilo pia limempongeza rais Jakaya Kikwete kwa kukemea upandaji holela wa bei za vyakula nchini.
Aidha, limeunga mkono uamuzi wa serikali wa kufuta kodi ya sukari inayotoka nje ya nchi ili kuhakikisha bei inashuka na kutoa nafuu kwa watumiaji.
Pongezi hizo zilitolewa juzi ikiwa ni sehemu ya tamko la kuwapongeza wagombea wa CCM mkoani hapa, waliopata ushindi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Baraza la wazee hao lilisema serikali haina budi kuchukua hatua za makusudi ili bei za vyakula na bidhaa nyingine muhimu nchini zishuke.
Lilisema kushuka kwa bidhaa hizo kutatoa ahueni kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa na uzalishaji mali, tofauti na ilivyo sasa ambapo maisha yameonekana kupanda na kuwafanya watu kutumia muda mwingi kutafuta njia mbadala za kuishi.
Pia, limeshauri serikali kumaliza tatizo la mgawo wa umeme unaoendelea katika maeneo mbalimbali nchini.
"Tunahitaji kuwa na umeme wa uhakika kwa kuwa ndiyo msingi wa uchumi wetu," walisema wazee hao.