Dk. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Balozi wa India nchini Tanzania Mhe. Binaya Srikanta Pradhan Ikulu Zanzibar kumuaga

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
479
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Balozi wa India nchini Tanzania Mhe. Binaya Srikanta Pradhan Ikulu Zanzibar kumuaga baada ya kumaliza kipindi cha miaka mitatu ya utumishi nchini tarehe: 22 Desemba, 2023.

Rais Dk. Mwinyi amemshukuru kwa niaba ya Serikali ya India kwa kudumisha ushirikiano na uhusiano wa kidiplomasia katika kipindi chake cha uwakilishi ikiwemo upatikanaji wa fursa mbalimbali za ufadhili wa masomo India, kuanzishwa kwa Taasisi ya IIT Madras Zanzibar, miradi mbalimbali ya maendeleo, kujenga uwezo, pamoja na fursa za uwekezaji na biashara.

Naye, Balozi Mhe. Binaya Srikanta Pradhan amezungumzia kuhusu Serikali ya India kuwapeleka kikundi cha Zanzibar One Modern Taarab kutoka Zanzibar kushiriki Tamasha la Utamaduni nchini India mwezi Februari mwaka 2024.

Pia Balozi Mhe. Pradhan amemwalika Rais Dk. Mwinyi kuitembelea India, Rais Dk. Mwinyi amekubali mwaliko huo wa kuitembelea India.View attachment 2849776
IMG-20231222-WA0016.jpg
View attachment 2849778
IMG-20231222-WA0014.jpg
IMG-20231222-WA0013.jpg
IMG-20231222-WA0012.jpg
 
Back
Top Bottom