Waraka Maalum kuhusu URAIS kwa Wajumbe wa Kamati Kuu CHADEMA

Kwani akisema atagombea urais wa tz ndo itakua hivyo.simnajua hua kuna ndoto za mchana waachen waote wakiamka wataacha na wataelewa sasa watagombeaje urais bila kura za maon za chama?na wamejipaje uhalali wa kuwakilisha chama?waachen na kamati kuku msipoteze muda wenu kujadili swala laki jinga.wananch wata jaj wao endeleen na majukumu mengine,wanabanwa na katiba kuusu umr nk.
 
Molemo taitakya moghaka, wewe unajua vizuri kuwa hili halitaji kukurupuka, no room for discusing the dead issue, hebu unataka akina MBATIA, LIPUMBA NA NAPE wapate la kusema? waache wafu wazikane wenyewe. tafakari sana hilo Molemo, acha watz wawahukumu wenyewe hao waliotangaza nia, kwa sasa majority tujielekeze for M4C. Chadema kwa sasa ni chama zaidi ya chama, je umenielewa? punguza munkali kamanda, hebu unakumbuka issue ya ndg yetu chacha wangwe? Mungu yuko pamoja na watz wanyonge, hata hili litapita

Mura IsayaMwita naiona hoja yako ni ya msingi sana.
Lakini kama nimemuelewa vizuri kamanda Molemo, anachopendekeza yeye ni kamati kuu kutoa mwongozo juu ya suala hili la uraisi ili kukiepusha chama na minyukano na makundi yasiyokuwa na tija kwa ustawi wa chama.

Chama hakiwezi kufanya maamuzi kwa kuhofia propaganda za ccm, cuf na nccr. Mkuu kwani umesahau ni mambo/maamuzi mangapi yamefanywa na kamati kuu tena mengine yakionekana kutishia uhai wa chama lakini bado tunasonga mbele? Maamuzi yoyote yanayofanywa kwa ajili ya mustakabali mwema wa chama siku zote wanachama wanayaunga mkono.

Hapa kinachotakiwa ni mwongozo tu si kinginecho, hata hao ccm,cuf na nccr unaowahofia hakuna mwanachama wao hata mmoja aliyetangaza hadharani kugombea uraisi, bado wanasubiri kuoteshwa!!
 
Mkuu Molemo
Leo umekiri waliotangaza urai hawajafunga kipengele cha katiba ya Chadema; bado sijaelewa hawa wanachama wa Kishapu uliokuwa umewanukuu wanaona chama kitaharibika kwa misingi ya watu watatu kutangaza nia yao au kwa misingi ya Chadema kuheshimu Demokrasi? Bado hujafunguka kinaogopwa kitu gani

Chama
Gongo la mboto DSM

Mkuu Chama,habari za siku.Samahani Kidogo huu waraka nadhani Molemo alilenga Kamati Kuu ya chama chake hivyo nadhani haukuhusu wewe mkuu kwa sababu mnafurahia sana makundi kwenye vyama vya siasa.
 
Nimetumiwa na rafiki lakini samahani nimeshindwa kuicopy

Naomba akili ya kuufungua huu waraka Mkuu BigMan.
Tangu jana nafanikiwa ku-download lakini haufunguki. Kunani?
Hebu nipe akili nitaufunguaje huu waraka Mkuu....
 
Nami naunga mkono wote ambao wanaona mawazo ya Molemo yanavyojenga ustawi wa Chama, hivyo kama wale walio kwenye ngazi ya kamati kuu walizungumze lakini kwa TAHADHALI kubwa maana hawa jamaa watajwao wanatumia katiba ya nchi kutaka kugombea. lakini wana hatari kubwa kwenye chama chetu maana wanatumiwa na IKULU, wanataka CDM iparaganyike wawe kwenye eneo zuri la kushinda.
 
Mkuu nashukuru.Nadhani wadau waelewe mapana ya waraka wangu.Si lazima kila kitu tuseme ni Upepo tu Utapita.
 
Jukwaa limekuwa lakumdiscuss zitto badala ya hoja ya molemo.

Mkuu nakushukuru kuliona hilo.Tafadhali tujadili waraka na si mtu.Isitoshe waliotangaza rasmi mpaka sasa ni watatu.
 
Zitto ni kama Tingatinga barabara ikishaisha haruhusiwi kupita tena yanapita magari ya kawaida.
 
Mura IsayaMwita naiona hoja yako ni ya msingi sana.
Lakini kama nimemuelewa vizuri kamanda Molemo, anachopendekeza yeye ni kamati kuu kutoa mwongozo juu ya suala hili la uraisi ili kukiepusha chama na minyukano na makundi yasiyokuwa na tija kwa ustawi wa chama.

Chama hakiwezi kufanya maamuzi kwa kuhofia propaganda za ccm, cuf na nccr. Mkuu kwani umesahau ni mambo/maamuzi mangapi yamefanywa na kamati kuu tena mengine yakionekana kutishia uhai wa chama lakini bado tunasonga mbele? Maamuzi yoyote yanayofanywa kwa ajili ya mustakabali mwema wa chama siku zote wanachama wanayaunga mkono.

Hapa kinachotakiwa ni mwongozo tu si kinginecho, hata hao ccm,cuf na nccr unaowahofia hakuna mwanachama wao hata mmoja aliyetangaza hadharani kugombea uraisi, bado wanasubiri kuoteshwa!!

Mkuu wangu Mwita Maranya,
Heshima kubwa kwako.Hakika umeuelewa vizuri sana waraka wangu kwa Kamati Kuu.Pia umeelewa vizuri lengo langu.
Ni lazima mambo ya msingi kama haya yazungumzwe haraka sana na kutolewa miongozo.CDM tuachane na yale mambo ya kusema ni Upepo tu Utapita.Ni lazima nidhamu ilindwe kwa kila hali ndani ya chama.
Mkuu asante sana kwa kuunga mkono hoja.
 
Molemo,,angalia post ya Ulukolokwitanga, Imemaliza kila kitu. Hapana haja kuanza kutoana macho,unataka kamati kuu iingize kwenye katiba kuzuia watu kutangaza nia? Imeshafahamika wazi hawa wanaotangazatangaza wakati wenzao wanaimarisha mshikamano kichama kuelekea 2015 wanatumiwa tu na hakika hawana nia ya urais wala urahisi. Hakuna haja kuanza kujibizana nao! Its ur good observation,lkn namna nzuri ni kuachana nao na kuendelea na mikakati ya kusamabaza elimu kwa raia

Mkuu wangu
Kutoa mwongozo kwa jambo fulani si kosa hata kidogo.Hayo ndiyo majukumu ya kamati kuu.Tuachane na habari za ni Upepo tu utapita.
 
Mkuu Molemo.
Umeongea mengi ya msingi ambayo mimi nayatafsiri kama maswala mtambuka kwenye kipindi cha mhemko wa uhuru na demokrasia ya kuwaza na kuutamani uraisi kwenye vyombo vya habari bila kujali uzito wa nafasi ya uraisi jinsi utakavyopatikana kwa chama pinzani ambacho kinahitaji kupata mtaji wa kuungwana mkono vijinini na pia ndio kwanza kinafanya maandalizi makubwa ya kung'oa mizizi minene ya mbuyu wenye miaka 50 kwenye historia ya vyama pinzania hapa Tanzania.

Naomba tutambue yafuatayo.

1. Kutangaza nia na kuwa na idadi kubwa au ndogo ya watangaza nia ya uraisi si dhambi maana ni kutimiza takwa la kidemokrasia na la kiasili kibinadamu (kutamani)

2. Hakuna kanuni yoyote iliyo kiukwa kwenye katiba ya chama kwa wote walio tangaza nia. Hapa hatupaswi kuwaona wachawi maana mazingira ya kichawi ya kukiuka kanuni hayapo.

3. Waliotangaza nia kupitia vyombo vya habari wamesukumwa na matamanio na matakwa yao binafsi na sio msukumo kutoka kwa wanachama wanaopenda ustawi wa chama kwenye maeneo mbalimbali ambayo hayafikiwa na kuyakubali mabadiliko.

Baada ya kutambua mambo 3 hapo juu. Tuweke kwenye mizani na haya hapa chini.

1. Je waliowahi kutamani na kutangaza nia ya kugombea uraisi kupitia chama chetu ni watu ambao tuna waamini na wanaamika kuwa watatuvusha tunako taka kwenda au ni watu ambao tuna aina ya mashaka nao?!

2. Muda huu ambao makamanda wako busy kukisambaza na kukieneza chama vijijini kwa ajili ya 2015, ni sahihi wengine kuwa kwenye media kutangaza nia badala ya kuunganisha nguvu?

3. Miongoni mwa watu waliokwisha tangaza nia kwa vyovyote watakuwa/wako busy kufikiria kutengeneza mitandao ya kuwaunga mkono ili wapate nafasi wanazo tamani kwa udi na uvumba, je nia zao na mitandao yao inakitakia mema chama kuelekea 2015 kwamba watapambana huku chama kikiwa salama bila mipasuko?!

Hitimisho.
Kwangu mimi nikiweka kwenye mizani naona mambo matatu ya kwanza yanazidiwa uzito na mambo matatu ya pili. Tuendelee kukijenga chama, sisi wanachama ndio twenye uamuzi wa nani anafaa na nani hafai kupeperusha bendera ya chama, waliowahi kutangaza wamelivuka daraja kabla ya kulifikia maana hawaja jua kuwa umri utashushwa au utabaki palepale, lakini pia wanatamani uraisi kwenye vyombo vya habari wakati wanategemea wengine wawa andalie mazingira kwenye m4c.

Sent from BlackBerry 8520 authorized by JamiiForums.
 
Mimi naona kwa sasa ni bora kamati kuu ikae kimya kana kwamba hakuna kinachoendelea na ionekane kwamba kila mwanachama ana uhuru wa kutangaza kugombea ili mradi awe na sifa zinazotakiwa na katiba ya chama na ya nchi.

Mkianza kutafutana mtakuwa mna-play on ZZK tunes maana lengo la kujitangaza kwake ni kuleta mgogoro ili baadaye chama kisambaratike ijulikane kuwa akina Wassira ni watabiri kumbe ndio mastermind wa mpango mzima. Kwa CDM kukaa kimya inakuwa sawa na mwanaume anayemfumania mkewe halafu anakaa kimya hamsemeshi kitu na kumpa mate so makubwa ya kuwaza nini kitafuata. Zitto ametumwa na magamba kupeleka mgogoro ndani ya CDM na dawa yake ni kumchunia hivi hivi.

"mwanagu ni mbishi na hashauriki" nanukuu kauli ya mama yake mzazi wa Zitto. Kizuri tutakachopata toka kwa Zito akiwa rais ni First Lady Wema Sepetu lakini maendeleo tusahau kwani mafisadi wanaomtumia hawana nia na maendeleo ya hii nchi.
Naunga mkono hoja. Huku kunyamaza kwa viongozi wa juu wa chama ni pigo tosha kwa huyu puppet Zitto. Ikitokea viongozi au kamati kuu ya chama ikasema chochote kile chenye kuonyesha kupingana na haya wanayofanya akina Zitto na washirika wake, basi hicho kinaweza kuwa kisingizio kwa zitto kupita akibwaka mitaani kuelezea ubaya wa chadema. Na hivyo kupelekea kusambaratika. Ni lazima ijulikane kwamba Zitto pia ana kundi kubwa la watu linalomuunga mkono. So kusema chochote kinyume naye kinaweza kuibua jambo lisilotarajiwa.
Dawa ya makelele ya mwehu ni kumpuuza. Maana ukianza kubishana naye tu atapata mengine mengi ya kusema na mwisho wa siku atakuvua nguo.
 
Mura IsayaMwita naiona hoja yako ni ya msingi sana.
Lakini kama nimemuelewa vizuri kamanda Molemo, anachopendekeza yeye ni kamati kuu kutoa mwongozo juu ya suala hili la uraisi ili kukiepusha chama na minyukano na makundi yasiyokuwa na tija kwa ustawi wa chama.

Chama hakiwezi kufanya maamuzi kwa kuhofia propaganda za ccm, cuf na nccr. Mkuu kwani umesahau ni mambo/maamuzi mangapi yamefanywa na kamati kuu tena mengine yakionekana kutishia uhai wa chama lakini bado tunasonga mbele? Maamuzi yoyote yanayofanywa kwa ajili ya mustakabali mwema wa chama siku zote wanachama wanayaunga mkono.

Hapa kinachotakiwa ni mwongozo tu si kinginecho, hata hao ccm,cuf na nccr unaowahofia hakuna mwanachama wao hata mmoja aliyetangaza hadharani kugombea uraisi, bado wanasubiri kuoteshwa!!

Ni kweli, Isaya Mwita ni kamanda mzuri wa CDM ila ktk hili hajaelewa vizuri nia ya Molemo. Molema ana hoja nzuri sana kwa mustakabali wa chama chetu.Siyo leo tu hata miaka 50 ijayo kama CDM itakuwepo, lazima kuwe na mwongozo ktk jambo hili. Kama haupo uwekwe.

Ni kweli kabisa.Nimeamua kuliweka hili wazi hasa baada kuzungumza na vijana wale wa Kishapu.Ninachotaka ni mwongozo wowote kutoka Kamati Kuu.Ninaamini Hekima ya wajumbe wa Kamati Kuu itatuvusha salama.
Mkuu hata kukaa kimya ni hekima pia.Manake wanaweza kusema neno mambo yakawa mabaya zaidi.Hukumbuki walivyommaliza she-buda?
 
Ni kweli, Isaya Mwita ni kamanda mzuri wa CDM ila ktk hili hajaelewa vizuri nia ya Molemo. Molema ana hoja nzuri sana kwa mustakabali wa chama chetu.Siyo leo tu hata miaka 50 ijayo kama CDM itakuwepo, lazima kuwe na mwongozo ktk jambo hili. Kama haupo uwekwe.

Ni kweli Kamanda Aweda,
Ni lazima tuanze sasa kuziba mianya inayoweza kuepusha mshikamano ndani ya chama kwa kuangalia mbele zaidi.
 
Mkuu Molemo.
Umeongea mengi ya msingi ambayo mimi nayatafsiri kama maswala mtambuka kwenye kipindi cha mhemko wa uhuru na demokrasia ya kuwaza na kuutamani uraisi kwenye vyombo vya habari bila kujali uzito wa nafasi ya uraisi jinsi utakavyopatikana kwa chama pinzani ambacho kinahitaji kupata mtaji wa kuungwana mkono vijinini na pia ndio kwanza kinafanya maandalizi makubwa ya kung'oa mizizi minene ya mbuyu wenye miaka 50 kwenye historia ya vyama pinzania hapa Tanzania.

Naomba tutambue yafuatayo.

1. Kutangaza nia na kuwa na idadi kubwa au ndogo ya watangaza nia ya uraisi si dhambi maana ni kutimiza takwa la kidemokrasia na la kiasili kibinadamu (kutamani)

2. Hakuna kanuni yoyote iliyo kiukwa kwenye katiba ya chama kwa wote walio tangaza nia. Hapa hatupaswi kuwaona wachawi maana mazingira ya kichawi ya kukiuka kanuni hayapo.

3. Waliotangaza nia kupitia vyombo vya habari wamesukumwa na matamanio na matakwa yao binafsi na sio msukumo kutoka kwa wanachama wanaopenda ustawi wa chama kwenye maeneo mbalimbali ambayo hayafikiwa na kuyakubali mabadiliko.

Baada ya kutambua mambo 3 hapo juu. Tuweke kwenye mizani na haya hapa chini.

1. Je waliowahi kutamani na kutangaza nia ya kugombea uraisi kupitia chama chetu ni watu ambao tuna waamini na wanaamika kuwa watatuvusha tunako taka kwenda au ni watu ambao tuna aina ya mashaka nao?!

2. Muda huu ambao makamanda wako busy kukisambaza na kukieneza chama vijijini kwa ajili ya 2015, ni sahihi wengine kuwa kwenye media kutangaza nia badala ya kuunganisha nguvu?

3. Miongoni mwa watu waliokwisha tangaza nia kwa vyovyote watakuwa/wako busy kufikiria kutengeneza mitandao ya kuwaunga mkono ili wapate nafasi wanazo tamani kwa udi na uvumba, je nia zao na mitandao yao inakitakia mema chama kuelekea 2015 kwamba watapambana huku chama kikiwa salama bila mipasuko?!

Hitimisho.
Kwangu mimi nikiweka kwenye mizani naona mambo matatu ya kwanza yanazidiwa uzito na mambo matatu ya pili. Tuendelee kukijenga chama, sisi wanachama ndio twenye uamuzi wa nani anafaa na nani hafai kupeperusha bendera ya chama, waliowahi kutangaza wamelivuka daraja kabla ya kulifikia maana hawaja jua kuwa umri utashushwa au utabaki palepale, lakini pia wanatamani uraisi kwenye vyombo vya habari wakati wanategemea wengine wawa andalie mazingira kwenye m4c.

Sent from BlackBerry 8520 authorized by JamiiForums.

Mkuu Mohamedi Mtoi Pamoja sana Kamanda.
Umeongezea nyama nyingi kwenye hoja yangu au waraka wangu kwa kamati kuu.Na kimsingi niwaombe wanaJukwaa wasijadili au kushambulia watu binafsi.Bali wajadili waraka wangu na kuangalia mustakabali wa chama miaka mingi ijayo.
 
Mungu wetu ni mwema,wanafiki na wazandiki watakwenda kuumbuka muda si mrefu......tuendeleze mapambano ya M4C raia waamke makamanda.
 
Back
Top Bottom