Waraka Maalum kuhusu URAIS kwa Wajumbe wa Kamati Kuu CHADEMA

Wao watangaze kuwania Urais, wengine waendelee na M4C na tuone mwisho wa siku nani atapeperusha bendera ya Chadema 2015. Ikulu ni mahali patakatifu. Ikulu ni mzigo. Ukimuona mtu anakimbilia Ikulu tena kwa gharama kubwa muogope kama ukoma.
 
Hilo jambo ila nashauri kamati kuu kuendelea kunyamaza kimya na wala isimjibu yeyote as long as no one among them ameenda nje ya kanuni za chama. CHAMA KIDNDELEE KUJIIMARISHA MIAKA MITATU SI MICHACHE KWA WATANZANIA KUBADILISHWA MAWAZO NA MAGAMBA hadi CHAMA kibweteke na kuanza kuongelea swala la URAIS.
 
Mkuu Takalani,tunataka Kamati Kuu itupe mwongozo wa hili jambo.
 
Hilo jambo ila nashauri kamati kuu kuendelea kunyamaza kimya na wala isimjibu yeyote as long as no one among them ameenda nje ya kanuni za chama. CHAMA KIDNDELEE KUJIIMARISHA MIAKA MITATU SI MICHACHE KWA WATANZANIA KUBADILISHWA MAWAZO NA MAGAMBA hadi CHAMA kibweteke na kuanza kuongelea swala la URAIS.

Mkuu hatuombi chama kimjibu mtu Hapana.Tunachoomba tu ni mwongozo wa chama kuelekea 2015
 
ungewashauri wamchukulie hatua yule msaliti mkubwa zitto kabwe kwa kuanzisha upuuzi huu,nani asiyejua kuwa huyo jamaa anatumiwa na ccm ili kuvuruga chama chetu,kama hatumiwi atuambie anaongea nini na dhaifu wanapokaa kitu kimoja kwenda wanakokwendaga

Sipingi Zitto au mwanachama mwingine yetote kutangaza nia ya kugombea urais, tatizo langu liko kwenye timing. Sidhani kuwa huu ulikuwa muda mwafaka ukizingatia kuwa chama kiko kwenye harakati kubwa ya kujitangaza vijijini. Hii ndiyo iwe agenda kuu ya chama kwa sasa. Suala la nani atapeperusha bendera ya chama liachwe kwa sasa, pamoja na kwamba hakuna kanuni inayonzuia mwanchama kutangaza nia.
 
Ushauri wako ni makini sana mkuu.
 
Mkuu Molemo, wazo lako ni zuri japo linahitaji umakini mkubwa kwa chombo husika kutafakari. Wanajamvi watakumbuka kuwa baada ya Mzee Lyatonga Mrema kushindwa urais mwaka 1995 alitamani aendelee kugombea mwaka 2000. Alienda mbele zaidi kwa kutaka awe akitambulishwa kama 'Mgombea Urais wa Mwaka 2000'. Nadhani wenzake kwenye vyombo vya maamuzi hawakulifurahia hilo, matokeo yalikuwa ni mitafaruku mikubwa iliyokuwa chanzo cha kifo cha NCCR- Mageuzi. Lakini lililo wazi ni kuwa ukichunguza kwa makini utagundua mkono wa CCM kupitia serikali yake kuhakikisha upenyo huo unaisambaratisha NCCR ingawa hawawezi kukubaliana na hilo.
Sasa kwa CDM, wenye kuijua historia hiyo wanapaswa kuwa makini wakitafuta ushauri wa wajumbe wake kama Mzee Marando, japo yale aliyoyasema Mzee Mtei ndio njia sahihi kwa Chama kufuata. Hatuwezi kuwa na Chama cha watafuta vyeo wasiotumia busara na tafakuri hata ya kupambanua historia ya kile kilichoisambaratisha nccr. CCM ni adui anayetamalaki, akitafuta nafasi ya kuvamia kama simba. Ni lazima tujihadhari!
 
Nikiamini wajumbe wa Kamati Kuu wanapita hapa mara kwa mara ninaamini wamekusoma.
 
Mkuu Chama,habari za siku.Samahani Kidogo huu waraka nadhani Molemo alilenga Kamati Kuu ya chama chake hivyo nadhani haukuhusu wewe mkuu kwa sababu mnafurahia sana makundi kwenye vyama vya siasa.

Mkuu fmpiganaji:
tunahoji tu yaliyojiri kwenye chama makini kama Chadema

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mimi naona kwa sasa ni bora kamati kuu ikae kimya kana kwamba hakuna kinachoendelea na ionekane kwamba kila mwanachama ana uhuru wa kutangaza kugombea ili mradi awe na sifa zinazotakiwa na katiba ya chama na ya nchi.

Mkianza kutafutana mtakuwa mna-play on ZZK tunes maana lengo la kujitangaza kwake ni kuleta mgogoro ili baadaye chama kisambaratike ijulikane kuwa akina Wassira ni watabiri kumbe ndio mastermind wa mpango mzima. Kwa CDM kukaa kimya inakuwa sawa na mwanaume anayemfumania mkewe halafu anakaa kimya hamsemeshi kitu na kumpa mate so makubwa ya kuwaza nini kitafuata. Zitto ametumwa na magamba kupeleka mgogoro ndani ya CDM na dawa yake ni kumchunia hivi hivi.

"mwanagu ni mbishi na hashauriki" nanukuu kauli ya mama yake mzazi wa Zitto. Kizuri tutakachopata toka kwa Zito akiwa rais ni First Lady Wema Sepetu lakini maendeleo tusahau kwani mafisadi wanaomtumia hawana nia na maendeleo ya hii nchi.

Umenichekesha sana, kwa hiyo Wema Sepetu hafai kuwa first lady? Tatizo si nani atamuoa bali je ni sahihi kwa mazingira ya Chadema ya sasa kuanza kugombania nafasi ya uraisi? Chama chenyewe bado kina changamoto nyingi Zitto angeheshimika na kukubalika zaidi angetumia muda na umaarufu wake miongoni mwa vijana kujenga chama. amevunja kanuni isiyoandikwa. Si kila kanuni lazima iandikwe. Zito na wenzake walioanza kutangaza kuwania urais kwa ticket ya chadema wamevunja kanuni isiyoandikwa. Kila mtu mwenye mapenzi mema na chama hiki kukuu cha upinzani analiona hilo. Wengekuwa watulivu tu warudi kujenga chama badala ya malumbano yasiyo na hoja.
 
Ha ha haa, niliona headline kwenye magazeti ya udaku wakimshauri Zitto amuoe Wema Sepetu, nami nikaunga mkono hoja and she will make a very good First Lady...
 
ungewashauri wamchukulie hatua yule msaliti mkubwa zitto kabwe kwa kuanzisha upuuzi huu,nani asiyejua kuwa huyo jamaa anatumiwa na ccm ili kuvuruga chama chetu,kama hatumiwi atuambie anaongea nini na dhaifu wanapokaa kitu kimoja kwenda wanakokwendaga

Mkuu Zitto ni mnafiki mkubwa, hana nguvu ndani ya chama anymore. Anachofanya ni kuvuruga mipango kwa manufaa ya CCM, Hili tulitarajie kwani katika msafara wa mambo na kenge wamo tushamjua tumuache ili malengo yake yashindwe.
CCM hawawezi kumchukua wanapenda kumtumia akiwa CDM, hata yeye anajua akihamia CCM atakufa kifo cha kisiasa kama Kaborou, Hizza, Lamwai N.k. Anapata guts hizi kwa kuwa yupo katika chama kikubwa kinachoungwa mkono na Watanganyika kwa mamilioni. Kama ana ubavu wa kisiasa then atoke aende kwa magamba aone shubiri yake. CDM ni mkombozi wa taifa hili so hatutaki kuwatoa magamba kuingiza gamba tena work done will be equal to zero
 
Lengo la waraka wako ni nini. Nauliza haya kwa as you seem to contradict yourself. Unasema
"Ni ukweli ulio dhahiri kuwa wanachama hawa watatu waliotangaza rasmi nia zao hawajavunja Katiba wala kanuni yoyote ya chama.."
Pamoja na kutambua kwako hivyo bado unaitaka kamati kuu. Unataka kamati kuu ikae ijadili nini? Nakuuliza haya nikiamini we ni mwanachama hai wa CDM,kama sio kumradhi.
 
Huo ni waraka hao malalamiko yako wewe binafsi dhidi ya wagombea urais kupitia Chadema kupitia mabandiko yako humu JF umekuwa ukimshambulia Zitto, na kusema ametumwa na CCM saizi tena unakuja na waraka feki.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu chama,
Makundi ndani ya Chadema yanaanza kuonekana.
 
Last edited by a moderator:
Wajumbe Kamati Kuu,

Kwa heshima kubwa nawaandikia waraka huu mfupi kuhusu jambo moja ambalo ni la msingi kabisa na ambalo wanachama wa kawaida kabisa wangependa ufafanuzi mapema iwezekanavyo. Nimeona nitumie njia hii ya kupitia mtandao wa Kijamii wa JF nikiamini ndiyo njia bora zaidi kwa sasa na wajumbe wote wa kamati kuu kwa namna moja au nyingine ni watumiaji wa mtandao huu maarufu wa JF.

Kwanza niwapongeze wajumbe wote wa Kamati Kuu na wanachama wote kwa ujumla kwa juhudi kubwa mnazofanya kwa pamoja kupitia Vuguvugu la Mabadiliko-M4C ambalo kwa kiasi kikubwa limewekiweka chama chetu katika nafasi nzuri sana hasa katika maeneo ambako vuguvugu hili limepita.

Ni takribani miezi mitatu sasa tangu kuanza kwa mjadala mpana hasa kupitia vyombo vya habari,mitandao ya kijamii na mijadala ya kawaida mitaani kuhusu UGOMBEA WA URAIS NDANI YA CHADEMA.

Ikumbukwe kwamba mpaka sasa wanachama WATATU wa CHADEMA wameshatangaza Rasmi nia zao za kugombea URAIS wa Tanzania kupitia CHADEMA mwaka 2015.Wanachama ambao wameshatangaza nia zao ni Mhe. John Magale Shibuda (Mbunge wa Maswa), Deogratius Kisandu(Katibu wa BAVICHA-Tanga) na Mhe. Zitto Zubeir Kabwe(Naibu Katibu Mkuu Bara- CHADEMA)

Ni ukweli ulio dhahiri kuwa wanachama hawa watatu waliotangaza rasmi nia zao hawajavunja Katiba wala kanuni yoyote ya chama lakini pia ni wazi kutangaza kwao kumesababisha sintofahamu kubwa ndani ya chama.

Athari kubwa zinazoonekana za wazi mpaka sasa ni:

* Kabla ya wanachama hawa kutangaza nia zao mijadala mbalimbali katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ilitawaliwa zaidi na Harakati za chama katika kujiimarisha kupitia Vuguvugu la M4C lakini sasa mijadala hiyo imehamia kujadili URAIS ndani ya CHADEMA kitu ambacho ni furaha kuu kwa maadui wa CHADEMA.

*
Makundi ndani ya Chama - Ifahamike kwamba CHADEMA inapaswa kuepuka kwa kila hali makundi ya aina yoyote ili kujitofautisha na vyama vingine vyenye makundi na yanayohatarisha uhai wa vyama hivyo. Tutakuwa tunajidanganya sana tukidhani kwamba hakuna watu wanaowaunga mkono wanachama hawa watatu ambao kwa lugha rahisi watakuwa tayari wanaunda mtandao wa watu watakaowapigania ndani ya chama ili majina yao yapitishwe na vikao wakati ukifika. Tufahamu kwamba hata kama watakuwa wanaungwa mkono na watu watano watano kila mmoja wao basi tayari hayo ni makundi na tayari hiyo ni mitandao. Tufahamu kwamba takriban bado miaka mitatu kufikia uchaguzi mkuu ujao!!

*
Nilikuwa katika safari zangu za kibiashara huko Kishapu na nilishangaa kukuta wanachama wa kawaida kabisa wanaokaa vijiweni wakilalamikia hatari inayonyemelea chama chao kwa kile walichodai ni malumbano ya kusaka madaraka.Wakawa na hofu kwamba chama chao kitaishia kama NCCR ya wakati huo.Nilishtuka na sikuamini kusikia hayo kutoka kwa wanachama wadogo kabisa wa kule Kishapu.

Nimalizie waraka wangu huu kuiomba Kamati Kuu ya CHADEMA pindi itakapokutana ijadiliane hili swala kwa uhuru kabisa na kujaribu kutizama athari zilizoko mbele ya chama endapo kama hali hii itaachwa iendelee ingawa hakuna kanuni wala katiba iliyovunjwa.

Kamati Kuu ijiulize swali:
Je, Viongozi kama kumi kila mmoja akitangaza nia hiyo miaka 3 kabla ya uchaguzi mkuu umoja wa chama kweli utalindwa
? Je, kunaweza kuwa na watangaza nia kumi kwa mfano halafu wasiunde mitandao ya kuwaunga mkono ili wapitishwe na vikao vya juu?

Si kazi yangu kutoa majibu ya maswali haya bali kwa niaba ya wanachama wengi na wapenzi wa CHADEMA tunaomba Kamati Kuu ije na majibu ya maswali haya na mwongozo kwa ujumla kuelekea 2015.

Naomba kuwasilisha.

Molemo.
kimsingi Molemo uko juu.kwa mara ya kwanza mwezi huu nimekaa na kuingia net.Safari yangu ya muda mrefu nje ya nchi inaniunganisha sana na ukweli wa CDM kuchukua nchi 2015.Watu wengi wa huku ulaya bado hawana taarifa sana za siasa ya Tz lakini kwa bahati nzuri wanataarifa za kutosha juu ya CDM.Kwamba tunawakati mgumu wa kumpata mgombea wa urais kupitia CDM kwa umbali naona kama kuna ukweli.Mimi ni mzaliwa wa Njombe,na kwa kweli kule kwa sasa tuna imani kubwa na uongozi wa juu wa CDM lakini kiukweli wabena na wahehe na makabila yanayowazunguka wanatabia ya uwoga pale ambapo hali ya usaliti inapoanza kujitokeza.Naamini watu kujitangaza kugombea wana haki lakini kwa muda ambaye kimsingi yuko nafasi za juu kama ZZK HATARI! Kila chama kina utamaduni ambao kwa vyovyote haujaandikwa popote lakini ni muhimu sana kuheshimiwa.Pamoja na hofu yangu kwa yanayotokea CDM bado naamini kwamba hiki ni chama makini sana na kwamba kwa karne hii hakuna kama CDM Tz.Kamanda Mbowe na Dr.Slaa tuwe tayari kuwasaidia ni viongozi wetu bora kabisa duniani.Miaka mitano tu ya uongozi katika nchi tutakuwa nchi bora duniani.Mungu tuepushe na fikira mbaya dhidi ya CDM:
 
Mremo we ni jembe kamati kuu isipoliangalia hili chama chetu kinaweza tusambararika. Kwani hawa watu wana nia lengo gani kutangaza nia sasa hivi? si wasubiri muda ukifika na sasa wajikite kwenye kukijenga chama? Kamati kuu fanya kazi na mtupe majibu mara moja
 
Lengo la waraka wako ni nini. Nauliza haya kwa as you seem to contradict yourself. Unasema Pamoja na kutambua kwako hivyo bado unaitaka kamati kuu. Unataka kamati kuu ikae ijadili nini? Nakuuliza haya nikiamini we ni mwanachama hai wa CDM,kama sio kumradhi.

Waraka wangu nimeuelekeza Kamati kuu ya CDM.Wewe hauhusiki.Samahani sana.
 
Back
Top Bottom