WOWOWO
JF-Expert Member
- Aug 3, 2011
- 590
- 430
Tukubali kwamba kuwafahamu watu wanaoutaka urais mapema ni afya kwa maslahi ya taifa maana tutapata fursa ya kuwafahamu kwa undani, kuwafuatilia, kuwapima lakini pia kuhoji uhalali wao kabla. Ndiyo maana toka mwanzo kabisa mimi ni moja wa watu ambao naunga mkono hoja ya watu wenye sifa kwa mujibu wa katiba (Msisitizo wenye Sifa) kutangaza nia.
Kwa sasa CDM haina mfumo wa kikatiba wala wa kikanuni wa kutangaza nia ya kugombea urais (Kitila Mkumbo-Raia Mwema 10/10/2012) hivyo, yeyote anayefanya hivyo ukianza na John Magale Shibuda, Deogratius Mushi na Zitto Zuberi Kabwe hakiuki chochote na hivyo kuwa na defense dhidi ya maamuzi yoyote ya Kamati Kuu au vinginevyo. Kwa maneno mengine kuwapinga akina Zitto & Co na nia zao za kugombea urais ni kutumia upepo tu badala ya katiba na Kanuni za CDM.
Kwangu mimi, Shibuda na Mushi (Sifahamu exactly umri wa Mushi lakini nahisi atakuwa amefikisha miaka 40 mwaka 2015) wana haki zote za kikatiba kutangaza nia zao za kugombea urais kupitia CDM. Sioni sababu yeyote ya kuwapinga bali wanachama wa CDM wenyewe watachuja pumba na mchele. Lakini kwa Zitto Kabwe ni habari tofauti. Katiba kwa kigezo cha umri haitamruhusu kugombea urais hiyo mwaka 2015. Tegemeo lake ni majaaliwa ya Katiba mpya ambayo hatuna uhakika kama kweli itaaccomodate umri wake au laa. Huyu anaweza kupingwa, maana kuna grounds za kumpinga.
Hoja kwamba, kutangaza nia mapema ni kukigawa chama inategemea na utashi wa anayetangaza nia na nini analenga. Kama utashi, hitaji na busara zake zinamtuma kutangaza nia ya kugombea (na 'haoni' athari zozote ndani ya chama au malengo yake yatatimia) hakuna kitu kinachozuia maana hakuna atakachokiuka ndani ya chama. Katika hili la kutangaza urais ndani ya CDM ni utashi binafsi na si suala la kikatiba wala kikanuni.That is wahy Zitto alikuwa na nguvu ya kumjibu Mzee Edwin Mtei alipomkanya juu ya kutangaza kwake nia maana kwa mujibu wa utashi, busara na hitaji lake haoni tatizo katika hilo.
Swali moja la kujiuliza ni Je Kamati Kuu itawaonya au kuwaadhibu watu hawa wanaotangaza nia ya kugombea urais kwa kanuni zipi za Chama? Hili ndilo ombwe linalotumiwa na wanaotangaza nia.Sasa CDM walizibe? Nini hatma ya Demokrasia kama likizibwa?