Mifumo ya teuzi ndani ya vyama Tanzania ni kikwazo kwa demokrasia. Lowassa na Slaa ni mifano muhimu rejea

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,620
46,264
Nikirejea namna vyama vikubwa viwili Tanzania vinavyoteua wagombea wake wa nafasi za uchaguzi hasa za Urais ni wazi vigogo wachache wa vyama wamehodhi mchakato wa kupitisha wagombea wao badala ya wanachama.

Utaratibu sahihi wa uteuzi katika demokrasia halisi na zilizokamaa ni chaguzi za wagombea kupitia wanachama wote au wajumbe walio wengi.

Kinachofanyika ndani ya CCM na CHADEMA cha zinazoitwa kamati za maadili na kamati kuu kuchuja wagombea kabla hawajapigwa kura na wanachama au wajumbe walio wengi mfano katika mkutano mkuu au Halmashauri kuu ni sawa na kutanguliza mkokoteni mbele ya Punda anayeuvuta au kuanza kuweka unga kwenye sufuria kisha maji ya kusonga ugali baadaye, kitakachopatikana hapo kitakuwa ni kituko tu.

Haya mambo ndio yaliyosababisha Lowassa kuwa muathirika mara kadhaa ndani ya chama chake akinyimwa fursa ya kuchaguliwa bila kupewa sababu, Mwenyekiti na kamati yake ya maadili hawapaswi kuwa na nguvu kubwa kiasi hicho cha kuamua nani atapata fursa ya kupigiwa au kutokupigiwa kura na wajumbe.

Pia hili jambo ndilo lililoivuruga CHADEMA wakati Lowassa alipohamia huko. Kama Lowassa angeshindanishwa kwa kura za wanachama wote au wajumbe walio wengi kwanza dhidi ya wagombea wote akiwemo Slaa CHADEMA ingeenda katika uchaguzi kikiwa chama tulivu kwa sababu mchakato unegeonekana huru bila vigogo wa chama kumbeba mtu.
 
Maamuzi ya KK za chama ndio yanawakilisha maoni ya wanachama, kama utataka wanachama wahusishwe kwenye hii michakato kuanzia mwanzo mpaka mwisho, basi lazima pawepo na muda mrefu utakaowawezesha wanachama kutoa maoni yao.

Jambo hili kama likifanyika, linaweza kuja kukosa uhalali mbele ya safari kabla ya kufanyika uchaguzi, kwasababu ya nature ya siasa zetu, mnaweza kumuandaa mgombea wenu kwa muda mrefu, halafu ghafla upepo ukaja kumuendea tofauti akapoteza mvuto kwa wapiga kura.

Mfano mzuri wa kuthibitisha hili ni hapo hapo kwa Lowassa, aliondoka CCM akaenda Chadema akiwa red hot favourite, kwa namna ile hata kama Chadema wangekuwa tayari na mgombea wao wameshamuandaa, bado tukubaliane bila unafiki, asingeweza kupata uungwaji mkono mkubwa kama ule alioupata Lowassa wakati ule.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Kamati Kuu za vyama haziwakilishi maoni ya wanachama na ushahidi ni jinsi wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM walivyoleta tafrani baada ya kutoliona jina lake.

Muda unatosha kabisa, kama uchaguzi mkuu wa nchi nzima huwa unafanyika ndani ya miezi mitatu wa chama unaweza kufanyika ndani ya mwezi mmoja au miwili ukakamilika, Zamani CCM walikuwa wanachagua wagombea ubunge wao kwa kura za wanachama wote kabla ya Magufuli kubadilisha na kufanya wajumbe ndio wapiga kura za wagombea. Siku hiyo hiyo wanachama wote au wajumbe wanapoenda kuchagua wagombea udiwani na ubunge wa chama chao wangeweza/wanaweza kupiga pia kura za kumchagua mgombea wao wa Urais wanayemtaka.
Maamuzi ya KK za chama ndio yanawakilisha maoni ya wanachama, kama utataka wanachama wahusishwe kwenye hii michakato kuanzia mwanzo mpaka mwisho, basi lazima pawepo na muda mrefu utakaowawezesha wanachama kutoa maoni yao.

Jambo hili kama likifanyika, linaweza kuja kukosa uhalali mbele ya safari kabla ya kufanyika uchaguzi, kwasababu ya nature ya siasa zetu, mnaweza kumuandaa mgombea wenu kwa muda mrefu, halafu ghafla upepo ukaja kumuendea tofauti akapoteza mvuto kwa wapiga kura.

Mfano mzuri wa kuthibitisha hili ni hapo hapo kwa Lowassa, aliondoka CCM akaenda Chadema akiwa red hot favourite, kwa namna ile hata kama Chadema wangekuwa tayari na mgombea wao wameshamuandaa, bado tukubaliane bila unafiki, asingeweza kupata uungwaji mkono mkubwa kama ule alioupata Lowassa wakati ule.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
CHADEMA badala ya kutuuzia sera zao na jinsi au namna gani inaweza kutatua na kumsaidia Mwananchi anayesumbuka mtaani, wao wamejikita kwenye siasa za utengano, visasi ,vinyongo na misimango.
 
CHADEMA badala ya kutuuzia sera zao na jinsi au namna gani inaweza kutatua na kumsaidia Mwananchi anayesumbuka mtaani, wao wamejikita kwenye siasa za utengano, visasi ,vinyongo na misimango.
Shida ya Tanzania sio sera, ni mfumo wa kujitawala usioleta uwajibikaji
 
Back
Top Bottom